Makapuku Forum

Makapuku Forum

....
Screenshot_20210328-131926_Twitter.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ametoa pongezi baada ya Serikali kuanzisha Tahasusi (Combination) mpya tano kwa ajili ya Wanafunzi wanaoingia kidato cha tano mwaka huu zikiwemo combination zenye masomo ya Michezo ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Wataalamu Nchini.

Combination zilizoongezwa hni Physics, Mathematics na Computer Studies (PMC), Kiswahili, French, Chinese (KFC), Kiswahili, English, Chinese (KEC), Physical Education, Biology ,Fine Art (PBF) na Physical Education, Geograph , Economic (PGE).

“Kufuatia vikao vya Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, OR TAMISEMI, na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, somo la michezo litafundishwa kama Tahasusi (Combination) kuanzia mwaka huu, nawapongeza sana Waziri Jafo na Waziri Prof. Joyce Ndalichako kwa ushirikiano wao, hili ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA ili kupitia mfumo huo tupate Walimu wabobezi wa kufundisha Vijana wetu Mashuleni_Bashungwa
20210329_175236.jpg
20210329_175257.jpg
 

Attachments

  • 20210329_175257.jpg
    20210329_175257.jpg
    51 KB · Views: 4
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amesema kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia kumekuwa na uhitaji wa Wataalamu wa fani mbalimbali hivyo Serikali imeanzisha Tahasusi (Combination) mpya tano kwa ajili ya Wanafunzi wanaoingia kidato cha tano mwaka huu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Wataalamu nchini.

Amezitaja combination hizo kuwa ni Physics, Mathematics na Computer Studies (PMC), Kiswahili, French, Chinese (KFC), Kiswahili, English, Chinese (KEC), Physical Education, Biology ,Fine Art (PBF) na Physical Education, Geograph , Economic (PGE).

Waziri Jafo amesema Combination ya PMC itatolewa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dodoma na Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Iyunga , KFC na KEC zitatolewa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Morogoro na ya Wavulana Usagara na PBF na PGE zitatolewa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Makambako, Shule ya Sekondari ya Wavulana Kibiti na Sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.

"Nchi yetu ilikosa kuwa na Wataalamu wa Michezo kutokana na kutokuwepo na Tahasusi (Combination) maalum, hivyo hili ni jambo jipya ambalo mwanzo halikuwepo”———Waziri Jafo
20210329_175558.jpg
 
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni Jambazi ameuawa baada ya kupigwa na risasi na wengine watano wamekimbia wakati genge la wahalifu hao likikabiliana na Polisi katika eneo la kagerankanda Wilayani kasulu Mkoani kigoma wakati Watuhumiwa wakijiandaa kuteka magari katika Barabara kuu.

RPC wa Kigoma James Manyama amesema katika tukio hilo la March 27,2021, wamekamata bunduki moja aina ya AK 47 na risasi 17, na kusema bado msako mkali unaendelea kuwatafuta waliokimbia.

"Polisi kasulu walipata taarifa kwamba Majamabazi sita walikua wamejipanga kuteka magari, Polisi waliweka mtego na kukaibuka majibizano ya risasi, Majambazi yalipoona yamezidiwa walifanikiwa kutoroka na kukimbilia porini”———RPC Manyama

“Mwili wa aliyeuawa kwenye tukio hilo umeifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi, huyu jambazi aliyeuawa mpaka Sasa hatujajua uraia wake, lakini kwa namba za bunduki tuliyonayo pamoja na kwamba ilikua inafukiwa chini inaonesha ni namba za silaha za kwetu haijatoka Nchi jirani"———RPC Manyama
20210329_175958.jpg
20210329_175937.jpg
 
Mkalimani Matungwa Mutatina ambaye alizua gumzo baada ya kutoa tafsiri iliyoonekana kuwa na kasoro wakati wa shughuli za kumuaga Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma amesema kiwango chake cha elimu ya ukalimani ni Degree na yupo kwenye taaluma hiyo kwa zaidi ya miaka 20.
20210329_180154.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom