Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watafiti kufanya utafiti kama kuna uwezekano wa kutumia ngozi ya kuku kuzalisha bidhaa mbalimbali za ngozi kama inavyofanyika kwa ngozi za ng’ombe, mbuzi n.k

Prof. Ole Gabriel ameyasema hayo wakati wa kuzindua mafunzo ya mnyororo wa thamani kwa Wadau wa ngozi Dar es Salaam.

“Kuku tunao Milioni 83.3 na wanataga mayai Bilioni 4 yenye thamani ya Tsh Bilioni 800, nguruwe tunao Milioni 2, ngozi, nyama na maziwa tukizitumia vizuri uchumi utakua, tusitupe kitu kwenye wanyama hata kwato, pembe, meno ya ng’ombe, mbuzi, kondoo hata punda yachangie uchumi”——->View attachment 1727291
Asitujaze Nani aache Kula akauze ngozi? Kwa Bei gani. Labda ngozi iwe na bei kuliko kuku mwenyewe.
 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amehitimisha ziara yake Chato kwa kushiriki kwenye kuchimba msingi wa madarasa manne na ofisi mbili kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kitela ambayo Wananchi wameamua kuijenga ili kupunguza msongamano Shule ya Sekondari Chato yenye Wanafunzi zaidi ya 2000.

Akizungumza na Wananchi kwenye ujenzi wa Shule hiyo, RC Gabriel ameipongeza Wilaya ya Chato kwa kuanza kutekeleza maagizo yake mapema kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kuanza kutatua kero ya msongamano wa Wanafunzi kwa kuanzisha ujenzi kwa kushirikiana na Wananchi.

"Katika Wilaya zote nne nilizotembelea nilisema nitarudi kuzindua kampeni ya ujenzi wa miundombinu kwenye Zahanati na Shule zetu, Chato mmenifurahisha sana kabla sijaondoka nimeshazindua kazi hii hapa, nanyi Wananchi nawaomba tusirudi nyuma tuendelee na moyo huu”- RC Gabriel

RC Gabriel pamoja na mambo mengine amewataka Viongozi wa Wilaya ya Chato kupitia Idara ya Ardhi kuhakikisha wanamaliza migogoro yote ya ardhi kwa kupima maeneo ya vituo vya kutolea huduma za Afya wilayani humo na kutoa hati za umiliki kwa faida ya sasa na baadaye.
20210317_173456.jpg
 
Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dorothy Gwajima amesema Serikali imetenga Tsh. Bilioni 15.8 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mkoani Mtwara na unatarajiwa kukamilika mwezi March mwaka huu.

Gwajima ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara Mkoani Mtwara ambapo amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 90 hadi sasa.
20210317_174012.jpg
20210317_173953.jpg
20210317_173932.jpg
 
Mahakama ya Mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya Wanandoa Raymond Kulaya (44) na Magreth Silaeli (37) waliotengana kwa miaka 10 baada ya kukubaliana kila Mtu akatafute Watoto ‘anapopajua’ baada ya kuishi miaka mitano bila kupata Mtoto, kwa sasa Magreth amepata Watoto wanne na Mwanaume mwingine.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Matrona Luanda ambapo amesema Mahakama hiyo iliangalia viini vikuu vitatu ikiwemo kama ndoa ya wawili hao ni halali baada ya kutengana tangu mwaka 2011.

Katika kesi hiyo Magreth aliiomba Mahakama itoe hati ya talaka, ili aolewe na Mwanaume anayeishi nae sasa ambaye amezaa nae, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya, wawili hao walifunga ndoa ya Kikristo mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano na kudai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na Watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 Mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na Watoto na kumwomba watengane ili kila Mtu aende akatafute Watoto na kusema katika kipindi walichoishi pamoja, Familia ya Ndugu wa Mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na Watoto na kuwasababishia kukosa raha.

Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata Mtoto licha ya kwamba Mwanaume alikuwa na Watoto watatu kabla ya kumuoa Magreth.
20210317_174242.jpg
 
Msanii Staa wa Bongofleva harmonize_tz amethibitisha leo kupitia Leo Tena ya cloudsfmtz kuwa anaamini kajalafrida ni Mwanamke sahihi kwenye maisha yake, akiiibu swali la mwijaku, Harmonize amesema kuwa usahihi wa Kajala kwake ni 1000%.

"Mwanzoni mwa huu mwaka nilikuwa nakamilisha Album nimefanya sana kazi, kwahiyo nikahitaji kuwa na break na kuwapa nafasi Watu wengine waachie kazi, ndio maana nimekuwa na wakati mzuri wa kurefresh mind na Mpenzi wangu Kajala lakini sio kila sehemu lazima niwe nae”- Harmonize
20210317_174801.jpg
20210317_174743.jpg
20210317_174723.jpg
 
"Security ni life-style, lakini pia Mimi naichukulia kama platform ya kusaidia Vijana wenzangu, ukiangalia Vijana wenzangu wote (wa Konde Gang)nimefahamiana nao miaka kadhaa, kwahiyo naamini nikiwashika mkono nao wanaweza kusogea sehemu fulani”———harmonize_tz kwenye Leo Tena ya cloudsfmtz

“Mabaunsa wananisaidia sana, tunazunguka sehemu nyingi unaona kinachotokea, wanaokuja kunizunguka inawezekana 90% ni Mashabiki lakini 10% wanaweza kuwa na nia mbaya, hao Mabaunsa wanatusaidia sanasana”———HarmonizeView attachment 1728016
20210317_175059.jpg
 
"Mwanzoni mwa huu mwaka nilikuwa nakamilisha Album nimefanya sana kazi so, nikahitaji kuwa na break na kuwapa nafasi watu wengine waachie kazi, ndio maana nimekuwa na wakati mzuri wa kurefresh mind na mpenzi wangu kajalafrida lakini sio kila sehemu lazima niwe nae."

Majibu ya Harmonize kuhusu kuongozana na Kajala na mapicha picha yanayoendelea kwenye mitandao • LeoTena
20210317_175302.jpg
 
Harmonize amejibu swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi hasa baada ya kushamiri kwa penzi lake na muigizaji kajalafrida, ikiwa inafahamika wazi kuwa harmonize_tz alifunga ndoa ya halali na mrembo mwenye asili ya kizungu sarah__tz, vipi baada ya kuachana! Talaka alitoa!?

"Sarah ni mtu ambaye nimeishi nae kwa miakq minne kama vijana kuna mengi tumeyapitia kama changamoto ninachoshukuru ni kila mmoja yupo kwenye maisha mengine sasa hivi na ninamuombea Mungu amsaidie, talaka nimeandika" Harmonize_Tz • LeoTena
20210317_175411.jpg
 
Rais wa Marekani Joe Bidden kwenye Interview ambayo ameifanya Jumanne hii na ABC Marekani amesema kwa sasa taifa hilo liko kwenye harakati za kumaliza matatizo ya Wahamiaji yaliyotokea wakati wa utawala uliopita hivyo hashauri Wahamiaji wengine kuwa na mpango wa kuingia Marekani kwa sasa "nasema wazi kabisa usije, usiuache Mji wako, Jiji lako au Jamii yako kuja hapa"

Inaripotiwa baada ya Biden kuanza kuiongoza Marekani kama Rais mpya idadi ya Watu wanaotaka kuvuka mipaka na kuingia Marekani imeongezeka kwa sababu wanaamini sera zake sio kali kama zile za Donald Trump ambae aliwarudisha Wahamiaji makwao na kusababisha zaidi ya Watoto 4000 kubaki Nchini Marekani chini ya uangalizi wa Serikali inayofanya jitihada za kuwaunganisha na Wazazi wao.
20210317_175542.jpg
 
UNAAMBIWA Ernest Seton wa Uingereza alipofikisha umri wa miaka 21 Baba yake alimpa jumla ya gharama zote alizolip kumuhudumia tangu anazaliwa hadi wakati huo, hadi pesa aliyolipwa Daktari aliyemsaidia Mama yake kujifungua ilihesabiwa.

Jumla ilikuwa USD 537.50 (Tsh. Milioni 1.2 ) na Baba yake akaongeza na riba ya 6%, Seton alilipa deni hilo kisha akabadili jina lake na hakuwahi tena kuongea na Baba yake, Seton alikuwa Mtunzi wa vitabu aliezaliwa Uingereza August 14, 1860 na kufariki October 23 1946.

Je unadhani ungepewa Bili yako mpaka hapo ulipofikia ingekua bei gani Mazee?
20210317_175709.jpg
 
UNAAMBIWA Zipo mbinu nyingi zinazotumiwa Nchini Uingereza kulinda mazingira ambapo wamekuja na hii ya kukusanya vipisi vya sigara ambapo mtaani vimewekwa visanduku vya kupigia kura ambavyo kuna maswali yanawekwa na kipisi cha sigara ndio mfano wa karatasi ya kura.

Baadhi ya maswali ni kama “Messi na Ronaldo nani Mkali?” hapo Mvutaji sigara ambaye anapenda soka hawezi kukubali kutupa kipisi chini badala yake ataweka upande wa Mchezaji anayemkubali.

Hii imesaidia kutunza mazingira na kuepusha Watoto kuokota vipisi vya sigara na kuvuta, baadhi ya Nchi kama Marekani nao wanatumia pia visanduku hivi, ingetokea Mtaani kwako ungependa maswali yaweje Mazee?View attachment 1728041View attachment 1728042
20210317_175857.jpg
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mnasi Haji amejiwekea utaratibu wa kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi hadi saa moja na dakika 40 kupita darasani katika Shule mbalimbali zilizopo Makao Makuu ya Halmashauri hiyo na kuwafundisha Wanafunzi wa darasa la saba, anaifanya hii kila siku kabla ya kuendelea na majukumu mengine.

Amesema anafanya hivyo kwakuwa yeye Kitaaluma ni Mwalimu na Ualimu upo kwenye damu, licha ya kuwa na uwezo wa kufundisha masomo mengi kwa sasa hufundisha zaidi Hisabati, hizi picha ni akiwa Shule ya Msingi Nyerere Ileje.
20210317_180118.jpg
20210317_180058.jpg
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Faustine Ndugulile ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia namna ya kupunguza gharama za usajili wa Online TV ili kusaidia Vijana wengi kujiajiri.

Ndugulile ametoa maagizo hayo alipotembelea Ofisi za TCRA Kanda ya Kaskazini Arusha na kusema ———> “Natambua Vijana wengi mmejiajiri kwenye Online TV TCRA nendeni mkapitie hizi tozo, tunawatoza Vijana hela nyingi sana, Mimi nataka kama Waziri nitengeneze mazingira wezeshi ya Vijana Wabunifu”

Kwa sasa Blogu, Online Forum na Waombaji wapya wa Radio na Television Mtandaoni wasio na leseni ya Utangazaji unaotumia mitambo iliyosimikwa ardhini hulipia Laki moja ya gharama ya maombi ya usajili, ada ya kupatiwa leseni ni Tsh. Milioni moja, ada ya mwaka ya leseni ni Tsh. Milioni moja na gharama ya kuhuhusisha (Renew) leseni ni Tsh. Milioni moja.

Leseni zote ni za miaka mitatu ambapo baada ya muda huo itahitajika kuomba kuhuishwa na kupewa Leseni nyingine kwa anayekidhi vigezo husika.
20210317_180339.jpg
20210317_180313.jpg
 
UNAAMBIWA Usiwabishie Watu wakitaka kufanya kazi zao, hili gari unaloliona matairi yakiwa yameganda kwenye cement lilikua linauzwa na Jamaa mmoja mbishi huko Belo Horizonte Nchini Brazil aitwae Mark Drummond ambae wakati Mafundi ujenzi wakiendelea na ukarabati wa barabara kutanua eneo la watembea kwa miguu walimtaka aliondoe eneo hilo ili wafanye kazi yao lakini akagoma, Mafundi wakaendelea na kazi yao na ngoma ndio kama unavyoiona hapo.
20210317_180644.jpg
20210317_180626.jpg
20210317_180601.jpg
20210317_180543.jpg
 
Wanamgambo wa Kiislamu 'wawakata vichwa watoto' Msumbiji.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa linasema watoto wadogo wa hadi miaka 11 wanauawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa Kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.

Mwanamke mmoja ameliambia shirika la Save the Children kwamba alishuhudia mtoto wake aliyekua na umri wa miaka 12 akiuawa karibu na mahali alipokuwa amejificha na watoto wake wengine.

"Baada ya mwanangu kuuawa, tulibaini ni hatari kuendelea kuishi katika kijiji chetu,"alisema.

"Tulikimbili anyumbani kwa baba yangu katika kijiji kingine, lakini baada ya siku chache mashambulio yakaanza tena huko pia ."

Zaidi ya watu 2,500 wameuawa na wengine 700,000 wametoroka makwao katika mkoa wa Cabo Delgado ulio na utajiri mkubwa wa gesi na mafuta tangu mashambulio ya wanamgambo yalipoanza mwaka 2017
20210317_181639.jpg
 
Kanisa katoliki limetoa msimamo wake kuwa haliwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

"Haiwezekani kwa Mungu kubariki dhambi" ofisi inayokutana kutoa mafundisho imesema siku ya Jumatatu.

Jibu hilo la CDF lilitokana na jibu kutoka kwa swali lililoulizwa.
Je kanisa hilo lina uwezo kutoa baraka kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja? Lilijibu hapana.

Mkutano wa mafundisho hayo ulisema kwamba ndoa kati ya wanaume na wanawake ni sakramenti na hivyo basi baraka haziwezi kupewa kwa wapenzi wa jinsia.

“Padri anaweza wabariki watu hao endapo wanaishi maisha ya uaminifu lakini baraka yoyote yenye lengo la kufungisha ndoa ni haramu” taarifa ilifafanua

Siku ya Jumatatu papa Francis aliidhinisha jibu la mkutano wa mafundisho, akisema kwamba sio njia ya kuwabagua, badala yake ni ukweli.
20210317_182003.jpg
 
Mwanasiasa wa Uganda ambaye pia alikuwa mgombea urais wa chama cha upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala.

Wakati Bobi Wine anakamatwa, wakati anaongoza timu ya wabunge kutoka chama chake cha National Unity Platform, kufanya maandamano dhidi ya kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama chake katika kipindi cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari.

Vikosi vya usalama vilifyatua vitoza machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.

Inasemekana kwamba waliokamatwa ni pamoja na wabunge 15.
20210317_182225.jpg
20210317_182207.jpg
20210317_182148.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom