Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210316_085259.jpg
 
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watafiti kufanya utafiti kama kuna uwezekano wa kutumia ngozi ya kuku kuzalisha bidhaa mbalimbali za ngozi kama inavyofanyika kwa ngozi za ng’ombe, mbuzi n.k

Prof. Ole Gabriel ameyasema hayo wakati wa kuzindua mafunzo ya mnyororo wa thamani kwa Wadau wa ngozi Dar es Salaam.

“Kuku tunao Milioni 83.3 na wanataga mayai Bilioni 4 yenye thamani ya Tsh Bilioni 800, nguruwe tunao Milioni 2, ngozi, nyama na maziwa tukizitumia vizuri uchumi utakua, tusitupe kitu kwenye wanyama hata kwato, pembe, meno ya ng’ombe, mbuzi, kondoo hata punda yachangie uchumi”——->
20210316_191054.jpg
 
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ipo katika mchakato wa kuja na Sheria ya TEHAMA ambayo pindi itakapokamilika itaweza kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Sekta hiyo ikiwemo kupambana na uhalifu wa mtandaoni.

Akizungumza katika kikao cha Wadau kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusiana na Sheria hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo DK. Zainab Chaula amesema ujio wa Sheria hiyo utazidi kuimarisha Sekta ya Mawasiliano nchini kwa kuiunganisha mifumo yote ya mawasiliano.

Amesema kupitia Sheria hiyo, changamoto mbalimbali zilizopo katika mifumo mbalimbali ya kiteknolojia itaweza kutatuliwa na kutoa majibu na hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa juu kutokana na sekta hiyo kuwa na msukumo mkubwa katika biashara ikiendana na mapinduzi makubwa ya viwanda kupitia ubunifu.
20210316_191427.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe, ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Toangoma, pamoja na Uongozi wa Kata, kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo vya uvunjifu wa maadili vinavyodaiwa kukithiri katika Shule hiyo.

Gondwe ametoa maelekezo hayo alipotembelea Shuleni hapo kwa lengo la kupata ukweli wa kile kilichoripotiwa na Vyombo vya Habari kuhusu kukithiri kwa vitendo vya ngono ambapo ametoa siku saba kwa Uongozi wa Shule na wa Kata kuweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na Uongozi wa Mtaa ili kwa pamoja wakubaliane ni kwa namna gani vitendo hivyo vitakoma.

Gondwe ameagiza kufukuzwa Shule kwa Wanafunzi watatu ambao wamethibitika kuwa vinara wa vitendo hivyo viovu pia ameagiza kupigwa kwa kura ya siri kwa kila darasa ili kuwabaini wanafunzi wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na baada ya kuwabaini wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha tuhuma hizo.

Amesema baada ya kuthibitisha Wazazi wao waambiwe kwa uwazi na hatua stahiki za kitabibu zichukuliwe kwa wale walioathiriwa kiafya na kisaikolojia, na kwa wale vinara hatua kali za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuondolewa Shuleni.
20210316_191555.jpg
 
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka Wadau wa Viwanda Nchini Tanzania kuichangamkia sekta ya ngozi kwa kuipa thamani na kuongeza uzalishaji kwa kutumia Wanyama kama Mbwa ambao wapo zaidi ya milioni 3 huku wengi wao wakiwa Mkoani Iringa.

Prof. Gabriel ameyasema hayo wakati wa kuzindua mafunzo ya mnyororo wa thamani kwa Wadau wa ngozi Dar es Salaam.

“Tanzania tuna Ng’ombe milioni 33.4, Mbuzi milioni 21.29, Kondoo Mil 5.65 na Punda laki 6.57 pia tuna Mbwa milioni 3 ambao wengi wanatoka Iringa na tuna paka milioni 3.5, tutumie Wanyama hawa kuzalisha ngozi kwa wingi” ——— Profesa Gabriel.
20210316_191833.jpg
 
UNAAMBIWA Timothy Dean Alsip (50) wa Oregon Marekani aliwahi kuvamia Bank na kufanya tishio la kutaka kupora USD 1 (Tsh. 2319) alifanya hivyo makusudi ili ipigwe simu Polisi na kweli Benki waliipiga huku yeye akikaa kwenye sofa kuwasubiri.

Lengo lake lilikuwa afungwe Gerezani ili akapate msaada wa matibabu, Timoth alikuwa ni ombaomba mwenye maisha magumu ambaye hakuwa hata na pa kuishi, siku ya tukio Benki alimtishia Muhudumu ampe $ 1 na akigoma atampiga risasi, Muhudumu alikimbizwa Hospitali kwa presha na Timothy akahukumiwa miezi isiyozidi 12 Gerezani.

Akiwa Mahakamani licha ya kukiri kufanya hivyo makusudi ili aende Gerezani kwa nia ya kupata matibabu ya bure ya mgongo na miguu, aliiambia Mahakama kuwa kama kifungo kitakuwa kifupi akitoka atarudia tena kosa.
20210316_192054.jpg
 
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeamua kuahirisha utoaji wa chanjo dhidi ya covid-19 ambayo ilikua imepangwa kuanza kutolewa kuanzia leo Jumatatu, Wizara ya Afya imesema zoezi hilo litafanyika baada tu ya kukamilika kwa uchunguzi wao kuhusu athari za chanjo hiyo ya Astra Zeneca.

Kwa mujibu wa dw_kiswahili imepita wiki moja tangu Nchi hiyo ipokee dozi zaidi ya milioni moja na laki saba na hivyo kuwa moja ya Nchi za kwanza kwenye Bara la Afrika kupokea chanjo hizo zilizoidhinishwa na kusafirishwa chini ya mpango wa Covax, Sasa Viongozi wa Congo wameamua kuahirisha utoaji wa chanjo hiyo kama ilivyofanywa kwa baadhi ya nchi za Ulaya kutokana na ripoti kwamba Watu waliopewa chanjo hizo wanapata matatizo ya kuganda damu.
20210316_192256.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom