Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 464,001
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema Serikali haina mpango wa kuziondoa au kuzuia Bajaji kusafirisha Abiria kupitia Barabara kuu na kusisitiza kuwa Bajaji na Daladala zote zina haki ya kubeba Abiria kwasababu Wamiliki wake wanalipa kodi za Serikali.
Chalamila ametoa kauli hiyo leo March 15,2020, Ofisini kwake wakati akitoa msimamimo wa Serikali baada ya Madereva Daladala kugoma Jijini Mbeya wakishinikiza Bajaji kuondolewa Barabara Kuu ambazo wanadai zimeidhinishwa kwa ajili ya Daladala pekee.
“Mkiendelea kugoma sitosita kutumia Mamlaka yangu, ninazo Taasisi nyingi, JWTZ, Magereza, Mahakama, na wana Mabasi ambayo yanaweza kubeba Abiria” -Chalamila