Makapuku Forum

Makapuku Forum

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha shughuli zote za soka kwa siku 14 ikiwemo mchezo wa kirafiki wa Kenya dhidi ya Tanzania uliyokuwa uchezwe leo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
RIPRaisMagufuli
20210318_180300.jpg
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia kifo cha Rais Magufuli na kufuatia kifo hicho amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurudi Dodoma.

Ndugai ameziagiza Kamati zote za Bunge zilizokuwa katika ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mikoani kurejea Bungeni Dodoma mara moja.
RIPRaisMagufuli
20210318_180419.jpg
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kitakuwa na maombolezo ya siku 21 sambamba na tangazo la Serikali kufuatia kifo cha Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho, uamuzi huo umetangazwa leo Dodoma na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
RIPRaisMagufuli
20210318_180529.jpg
 
Kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, Serikali Mkoani Mbeya imeandaa Ibada maalumu ya kumuombea pumziko la milele pamoja na kuliombea Taifa amani na utulivu wakati wote wa maombolezo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alipokuwa anazungumza kuhusu kifo cha JPM ambapo amesema maombi hayo yatafanyika kesho katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Chalamila amesema maombi hayo yatawahusisha Waumini wa Dini mbalimbali pamoja na Viongozi wa Mila.
20210318_180645.jpg
 
“Mimi nina uhakika kabisa Uongozi wa Mama Samia ambaye Mimi nimefanya nae kazi Mama Shupavu nina uhakika atatupeleka kwenye direction nzuri tu, na kuendeleza ile mikakati na mipango madhubuti ya kuliongoza Taifa la Tanzania” - CEO wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga josephkusaga
RIPRaisMagufuli
20210318_180816.jpg
 
“Watanzania kwenye shida tunakuwa pamoja, kwenye raha tunakuwa pamoja, tuondoe zile tofauti zetu za kidini, tuondoe tofauti zetu za kisiasa yale mazuri yote aliyoyafanya (Rais Magufuli) tuyatafakari zaidi na kuyaweka sawa” - CEO wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga

“Mimi nitamkumbuka (JPM) kwa kitu kinachoitwa uthubutu, nina uhakika maamuzi aliyokuwa anayafanya mengine yalikuwa yanawachukiza Watu, lakini alikuwa akifanya maamuzi ilikuwa ni kwa faida ya Watanzania” - KUSAGA RIPRaisMagufuli
20210318_180930.jpg
 
Baadhi ya Wasanii wamejikusanya na kuingia studio kuandaa wimbo wa pamoja wa kumuaga Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Wasanii hao ni pamoja na Diamond Platnumz, RayVanny, Jux, Marioo, Malkia Karen, Zuchu, Khadija Kopa, Christina Shusho, Gnako, Abbah, S2kyz na wengineo waliokutana katika studio za Wanene.
RIPRaisMagufuli
20210318_181128.jpg
20210318_181100.jpg
 
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza siku saba za maomboezo Nchini Kenya kufuatia kifo cha Rais Magufuli na bendera zitapepea nusu mlingoti, Kenyatta ametoa pole pia kwa Mama Janeth na Watanzania wote kwa ujumla.

“Nimempoteza Rafiki, nimempoteza Kiongozi mwenzangu na Kenya tunasimama imara na wenzetu Watanzania kwenye wakati huu mgumu, nimeongea na Mama Samia nimempa pole na kumuhakikishia tunasimama nae pamoja kwenye wakati huu mgumu” ——— Uhuru Kenyatta.
20210318_181341.jpg
 
"Tumempoteza Kiongozi wetu Shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli, alilazwa tarehe 6 March mwaka huu katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikua nalo kwa zaidi ya miaka 10”

“Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena, alilazwa March 06,2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa March 7 na kuendelea na majukumu yake”

“March 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta, Nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti” ——— Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu. RIPRaisMagufuli
20210318_181524.jpg
 
Mwimbaji wa siku nyingi kwenye Bongo Fleva Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice amenusurika kifo kwenye ajali ya gari Nchini Kenya baada ya gari dogo walilokua wakisafiria kugongwa la Lori kwenye eneo la Naivasha.

"Lori lilikua linakuja Nairobi likiwa limebeba maziwa, Dereva anavyosema ni kwamba gari lilikosa mwelekeo na kukosa breki ndio akaja kutugonga sisi, gari yangu ilibiringika na vioo vimeniingia sana kwenye mwili na sikio limekatika lakini nawashukuru Madokta wamenisaidia kulirudishia"

"Aliyekua anaendesha gari langu ni Rafiki yangu tulitoka pamoja Nairobi na nilikua nimekaa nyuma sababu nilikua nataka nilale ili nikifika tu niweze kufanya show iliyonipeleka huko, ilikua ajali mbaya sana jioni kama saa moja kasoro, kwenye eneo la ajali wengine walitusaidia wengine walituibia, naendelea vizuri kwa sasa” ——— Mr. Nice.
20210318_181634.jpg
 
Jeshi la Polisi Mjini Magharibi Zanzibar linamshikilia Mwanaume mmoja kwa tuhuma za kutaka kusababisha kifo cha Mke wake wa pili ambae amemuoa sio chini ya wiki mbili zilizopita.

Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Awadhi Juma Awadh amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema "Kijana anaitwa Yusufu Maulid Mussa (24) Mkazi wa Kwarara amemjeruhi Mke wake Asha Hassan Haji (28) Mkazi wa Kwarara pia na kumsababishia majeraha makubwa shingoni, Mwanamke amewaisha Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu"

"Mtuhumiwa tumeshamkamata yuko Mahabusu Kituo cha Mazizini kwa hatua zaidi, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.... taarifa nilizozipata hii ndoa bado ni changa sana nimeambiwa ni wiki mbili zilizopita wamefunga ndoa sasa nadhani Mapenzi yalikua bado motomoto na wivu sasa umepelekea hivyo" ——— RPC Awadhi Juma Awadh.
20210318_181746.jpg
 
Wananchi wa Kata ya Chang'ombe, Mtaa wa Chang'ombe Juu jijini Dodoma wameiomba Serikali kuwasaidia kuchunguza kuibuka kwa shimo lenye maji katikati ya Barabara ya Mtaa huo lililoibuka usiku wa kuamkia March 13 na kuzua taharuki kwa wakazi hao juu ya usalama wao.

Wananchi hao wamedai kuwa wamechukua jitihada za kujaribu kulifukia na mawe lakini mawe yote yalizama na hayakuonekana na hata walipojaribu kutumbukiza mti wa futi 20 ulizama, AyoTV inaendelea kuzitafuta Mamlaka ili kupata ufafanuzi zaidi.
20210318_181937.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom