Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga marufuku ya upigwaji wa ngoma za vigodoro pamoja ngoma ya kanga moja maarufu kama Kanga Moko katika Mkoa huo.

Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.

"Sio ruhusa kwa Wakazi wa Mkoa wa Kaskazini na Wananchi wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kuja kupiga ngoma na kucheza vigodoro na kanga moja "kanga moko"

Ameyasema haya wakati akitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu muelekeo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye miaka mitano ijayo Ofisini kwake Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
20210310_182209.jpg
20210310_182230.jpg
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio la Mgonjwa Piche Mkuja anayedaiwa kumchoma kisu Muuguzi wa Kituo Cha Kuhudumia Wagonjwa wa Ukoma Nazareti, Ifakara Wilaya ya Kilombero Agatha John (50), wakati Mgonjwa huyo alipofika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kupatiwa matibabu.

Amesema Muuguzi alifika katika eneo alikolazwa Mgonjwa huyo ili kukagua maendeleo yake ndipo baada ya kufika karibu, mgonjwa huyo alichomoa Kisu na kumchoma muuguzi tumboni hadi utumbo ukatoka nje kisha na yeye kujichoma sehemu za tumboni kwa lengo la kutaka kujiua .

Musilimu amesema baada ya tukio hilo Wafanyakazi wezake walimchukua Muuguzi huyo na kumpeleka Hospitali ya St.Francis ili kupatiwa matibabu ambapo muda mchache badae alifariki

"Hadi sasa upelelezi unaendelea kwani mara baada ya tukio Muuguzi alifariki, Mtuhumiwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Francis chini ya ulinzi mkali wa Polisi, taarifa za awali zinaonesha Mtuhumiwa ni mzima wa afya na wala hana tatizo la akili, tunachunguza kujua chanzo”- RPC
20210310_182047.jpg
 
Serikali ya Ufaransa imeahidi kutoa Euro milioni 150 (Tsh. Bilioni 413) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa awamu ya tano wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi, Dar es Salaam.

Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Frederic Clavier wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, ‘katika ofisi ndogo za Wizara Dar es Salaam.

Prof. Kabudi amesema kuwa mazungumzo yake na Clavie yalijikita katika utekelezaji wa mambo waliyokubaliana wakati alipofanya ziara ya kikazi mwezi February, Ufaransa.

“Katika mazungumzo yangu na Balozi tumejadili mambo mbalimbali likiwemo suala la Shirika la Maendeleo la Ufaransa kutoa fedha kwa ajali ya kuendeleza mradi wa awamu ya tano wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam”- Kabudi
20210310_182015.jpg
 
“Natoa wito kwa Wanahabari na Wananchi wetu kuendelea na utaratibu wa kupata taarifa kupitia vyanzo rasmi vya habari,kutumia rumours/uvumi kama habari rasmi ni kukiuka sheria zinazosimamia sekta ya habari, epukeni kusambaza habari ambazo mtawajibika nazo”-Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa
20210310_181744.jpg
 
Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza amejibu madai ya ubaguzi kutoka kwa mjukuu wake Mwanamfalme Harry na Mkewe Meghan, akielezea wasiwasi mkubwa na kuonesha huruma kuhusu matatizo wanayopitia ya maisha ya kifalme.

Taarifa kutoka Kasri la Buckingham imesema Familia nzima imehuzunishwa na habari za jinsi miaka kadhaa iliyopita ilivyokuwa migumu sana kwa Harry na Meghan na kusema masuala yaliyoibuliwa, na hasa kuhusu ubaguzi, ni ya kutia wasiwasi.

Malkia amesema mambo hayo yamechukuliwa kwa uzito mkubwa na yatashughulikiwa na Familia hiyo kwa njia ya faragha.

Kasri la Buckingham limekumbwa na shinikizo la kutaka lizungumzie madai yaliyotolewa kwenye mahojiano ya kipindi cha televisheni cha Oprah Winfrey kilichorushwa kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita, ambayo yalizusha mgogoro ambao haujaonekana tangu nyakati za Mama yake Harry, Dianna katika miaka ya 1990
20210310_181650.jpg
 
Msemaji wa Simba SC. HajisManara na Mtangazaji Maulid Kitenge wamemaliza tofauti zao zilizotokea hivi karibuni, wote kwa pamoja wamethibitisha kumaliza tofauti hizo wakisimamiwa na Baba wa Hajis, Mzee Sunday Manara.

“Sehemu yoyote ile yenye Wazee basi huwa mambo yanaenda sawasawa na hii yote ni kwasababu wao ndio Walimu wetu wakuu hasa katika maadili, Wazee wetu wameona si jambo jema vijana wao tukosane tena hadharani wakae kimya” ——— Kitenge.

“Leo kimefanyika kikao kizuri chini ya Baba yetu Sunday Manara na Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu na sasa najisikia amani kusema kwamba kikao kimefanikiwa kuzikata "TOFAUTI ZETU", tumerudi kuwa marafiki wazuri kama ilivyokuwa zaman” View attachment 1722137
20210310_181453.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga marufuku ya upigwaji wa ngoma za vigodoro pamoja ngoma ya kanga moja maarufu kama Kanga Moko katika Mkoa huo.

Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.

"Sio ruhusa kwa Wakazi wa Mkoa wa Kaskazini na Wananchi wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kuja kupiga ngoma na kucheza vigodoro na kanga moja "kanga moko"

Ameyasema haya wakati akitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu muelekeo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye miaka mitano ijayo Ofisini kwake Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja. View attachment 1722129View attachment 1722130
WaZanzibari haya mambo wawaachie wa bara...
 
Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi amempongeza Balozi Dkt. Bashiru Ally kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Tanzania na kumuahidi ushirikiano, Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo leo wakati Bashiru alipofika Ikulu, Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha.
20210310_181412.jpg
20210310_181340.jpg
 
Wanachama wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) Jumamosi iliyopita walifanya mkutano wa dharura Dar Es Salaam na kueleza kuwa kama changamoto za mfumo wa tiketi za mabasi za kimtandao hazitopatiwa ufumbuzi, basi leo Jumatano watasitisha kutoa huduma za usafirishaji.

Habari zilizo njema kwa Abiria leo ni kwamba TABOA wametoa tamko kuwa hawawezi kugoma tena baada ya kukaa kikao kirefu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

“Tunaishukuru sana Serikali yetu sikivu changamoto zetu zote zimechukuliwa, zipo TRA zinafanyiwa kazi na imeundwa Kamati, tunawaomba radhi Abiria kwa usumbufu” ——— Kaimu Katibu Mkuu wa TABOA
20210310_181147.jpg
 
Msemaji wa Simba SC. HajisManara na Mtangazaji Maulid Kitenge wamemaliza tofauti zao zilizotokea hivi karibuni, wote kwa pamoja wamethibitisha kumaliza tofauti hizo wakisimamiwa na Baba wa Hajis, Mzee Sunday Manara.

“Sehemu yoyote ile yenye Wazee basi huwa mambo yanaenda sawasawa na hii yote ni kwasababu wao ndio Walimu wetu wakuu hasa katika maadili, Wazee wetu wameona si jambo jema vijana wao tukosane tena hadharani wakae kimya” ——— Kitenge.

“Leo kimefanyika kikao kizuri chini ya Baba yetu Sunday Manara na Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu na sasa najisikia amani kusema kwamba kikao kimefanikiwa kuzikata "TOFAUTI ZETU", tumerudi kuwa marafiki wazuri kama ilivyokuwa zaman” View attachment 1722137View attachment 1722138
Niisema hawa mambo yao waachiwe wenyewe..
 
WaZanzibari yao Taarab...

iinye ndembe ndembe khanga moko laki si pesa million ya vocha...

Nayasikia tu... sometimes unaweza kua barabarani ukashangaa coster inapita aibu tupu...
Hahahha
Enzi za maisha club haujawahi kweli kwenda hata siku moja kuchungulia kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom