Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210309_180254.jpg
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbas amesema Serikali ya Tanzania haiwezi kusema Tanzania hakuna Corona kwani Watu wanasafiri na wanaingia ila tu haiwezi kuwajaza Watu hofu "kwanza unajua takwimu za ugonjwa wa kwanza kuua ni upi? Kwa nini Watu hawaulizi takwimu za Malaria kila siku hata hiyo chanjo waendelee kujaribu, yaani ndio kwanza wanajaribu dawa nani yupo tayari hapa kujaribiwa?”

“Kwanza Tanzania ina historia ya kutengeneza chanjo yetu sisi wenyewe na kwenye hili Watafiti wetu wapo kazini na sisi tunatafuta chanjo vilevile, msimamo pia ni huo waendelee kuwajaribu wengine ikikubalika tutaona namna ya sisi kunufaika" - Dr. Abbas
20210309_180028.jpg
 
Baada ya ripoti za Wanafunzi wa Kunduchi Girls Secondary kugoma wakiulalamikia Uongozi mpya wa Shule hiyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)-Makao Makuu imesema inafanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Viongozi wa Taasisi ya MDI inayomiliki baadhi ya Shule ikiwemo Shule hiyo ambapo pamoja na mambo mengine imeshindwa kuwalipa mishahara na posho nyingine Walimu na Wafanyakazi wengine.

Malalamiko mengine ni Mkurugenzi kukataa kulipa madeni ya Walimu na Wafanyakazi wengine ambayo hadi Mwezi huu yamefikia zaidi ya Milioni 400, pia Mkurugenzi wa MDI na Mkurugenzi mpya wa Elimu wa Shule hiyo wamekuwa wakiingia mikataba mibovu na kuikodisha Shule kwa Wamiliki mbalimbali bila kufuata utaratibu.

“Uongozi wa MDI unakwepa kodi na kuisababishia hasara Serikali na pia umetangaza kuwaondoa Walimu na Wafanyakazi wote bila kuwalipa malipo yao kwa madai kuwa hiyo ni amri kutoka Uongozi wa Mkoa, na tangu mwaka 2017 inalalamikiwa kuwa Bodi ya Wadhamini inaongoza Shule hiyo bila kusajiliwa RITA”- TAKUKURU

TAKUKURU imesema imeshafanya mahojiano na baadhi ya Walalamikaji na wanaendelea kuwahoji walalamikiwa, leo wamemuhoji Mkurugenzi wa MDI, Ally Magoga lengo likiwa ni kufahamu ukweli wa malalamiko haya ili hatua zichukuliwe..
20210309_175142.jpg
 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kunduchi wamefanya mgomo kwa zaidi ya siku mbili wakimlalamikia Mkurugenzi mpya wa Shule Mwinyikombo Ayubu kwa madai ya kuvuruga taratibu zao za kila siku ikiwemo ratiba za masomo na chakula pamoja na kutishia kuwafukuza Walimu aliowakuta akiwemo HeadMaster na kuleta Walimu wapya na Wanafunzi wapya kutoka Shule nyingine.

Zimemtafuta Mwinyikombo ambaye alikuwa tayari kuzungumza lakini Polisi walifika na kuondoka nae kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kupunguza vurugu.

Wazazi wa Watoto hao wamefika Shuleni na kufanya Kikao cha pamoja na Walimu pamoja na Bodi ya Shule huku Wazazi wengine wakishauri Shule ifungwe kwa muda na waondoke na Watoto hao kwasababu za kiusalama.

Baada ya msuguano ulidoumu kwa zaidi ya saa tatu, Wazazi wamekubaliana kuwaacha Watoto Shuleni huku wakiwasihi kurejea darasani lakini wameiomba Serikali iwe nguvu zaidi ili kuumaliza mgogoro huo kwa haraka..
20210309_175239.jpg
 
Wafanyakazi wa Ndege moja Nchini Urusi walilazimika kumfunga Abiria mmoja kwa kamba kwenye kiti chake baada ya kuanza kuvua nguo ya ndani mbele ya Abiria wenzake wakati Ndege ikiwa angani.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 alianza kuvua nguo na kuivaa kisha kuivua na kuvaa tena mfululizo huku akizunguka ndani ya Ndege dakika 15 tu baada ya Ndege hiyo kupaa kutoka Vladivostok.

Alibaki amefungwa kwenye kiti chake mpaka Ndege ilipotua Tolmachevo Airport na Polisi walipompeleka kituoni alikiri kuwa alitumia dawa za kulevya kabla ya kupanda kwenye Ndege.
20210309_175759.jpg
 
Kocha Msaidizi wa zamani wa Yanga SC Juma Mwambusi ametangazwa leo kuwa ndio Kocha wa muda wa Yanga SC baada ya Cedric Kaze na benchi lake la ufundi kufutwa kazi.


Safari hii naona watafukuza wachezaji na kocha wao na mashabiki wao
20210309_173811.jpg
 
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (ADU) linatarajia kuwafikisha Mahakamani Watu wanne akiwemo Said Mbasha na wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi wake wawili akiwemo Mwanafunzi wa Chuo.

Watuhumiwa hao ni Mfanyabishara Joseph Dalidali (26), Mfanyabiashara Said Mbasha (24) na Mwanafunzi wa kike Allu John Murugwa ( 24), pamoja na Fatuma Shomari ( 24).

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya ACP Alhaj Kabaleke Salim Hassan amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

"Mtuhumiwa Allu ambaye ni Mwanafunzi amekiri kuwa dawa za kulevya aliletewa na Mpenzi wake Mbasha, pia baada ya Mbasha kukamatwa alikutwa akiwa na Fatuma ambaye alikiri kuwa ni mpenzi wake (Allu na Fatuma wote Wapenzi wa Mbasha) baada ya kuwafanyia upekuzi katika nyumba wanayoishi walikutwa na pesa USD 14, 000 , pia wamekutwa na TSh.Mil.12.3 pamoja na misokoto 3 ya bangi"
20210309_173555.jpg
 
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (ADU) linatarajia kuwafikisha Mahakamani Watu wanne akiwemo Said Mbasha na wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi wake wawili akiwemo Mwanafunzi wa Chuo.

Watuhumiwa hao ni Mfanyabishara Joseph Dalidali (26), Mfanyabiashara Said Mbasha (24) na Mwanafunzi wa kike Allu John Murugwa ( 24), pamoja na Fatuma Shomari ( 24).

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya ACP Alhaj Kabaleke Salim Hassan amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

"Mtuhumiwa Allu ambaye ni Mwanafunzi amekiri kuwa dawa za kulevya aliletewa na Mpenzi wake Mbasha, pia baada ya Mbasha kukamatwa alikutwa akiwa na Fatuma ambaye alikiri kuwa ni mpenzi wake (Allu na Fatuma wote Wapenzi wa Mbasha) baada ya kuwafanyia upekuzi katika nyumba wanayoishi walikutwa na pesa USD 14, 000 , pia wamekutwa na TSh.Mil.12.3 pamoja na misokoto 3 ya bangi"View attachment 1721061

Sembe Noma, huyo Denti kisha haribu fyucha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom