Mandhari ya Barabara ya Shekilango Kilomita 3.7 iliyojengwa kwa njia 4, upana Mita 22, njia za watembea kwa miguu, taa za Kisasa, mitaro ya maji na bustani ili kupunguza msongamano wa magari kuanzia maungio ya Barabara ya Morogoro na kupita mitaa yote ya Sinza mpaka maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam, huu ni muonekano baada ya ujenzi wake kukamilika. (Swipe kuona picha nyingine)View attachment 1722120
Rais wa Marekani Joe Biden amewarudisha kwenye Makazi yake binafsi yaliyopo Wilmington, Delaware Mbwa wake wawili ambao alihamia nao Ikulu baada ya mbwa hao uanza tabia ya kuwarukia, kuwafokea na wakati mwingine kuwang’ata Walinzi wa Ikulu.
Mbwa hao wenye asili ya kijerumani aliwachukua mwaka 2018 kwenye kituo cha kufugia Wanyama na kuanza kuishi nao, mmoja anaitwa Major na ana umri wa miaka mitatu na mwingine anaitwa Champ mwenye miaka 14.
Maziko ya Dk. Haruna Chawala na Mkewe Neema Mwasanganga tayari yamefanyika katika kijiji cha Viwenge wilayani Kilolo mkoani Iringa, Wanandoa hao wameacha Watoto wawili wadogo.
Walifariki usiku wa kuamkia Jumapili March 7, 2021 baada ya gari lao kutumbukia katika Daraja la Shaban Robert lililopo wilayani Mpwapwa wakat Dk. Chawala alipokuwa akimpeleka Mkewe aliyekuwa mfanyakazi katika kitengo cha ugonjwa wa Kifua Kikuu Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.