Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210108_035919.jpg
 
Club ya Simba SC imetangaza rasmi kuwa imeachana na kocha wake Mkuu Raia wa Ubelgiji Sven Vanderbroeck ikiwa ni siku moja imepita toka aiwezeshe kufuzu hatua ya Makundi ya CAF Champions League kwa ushindi wa 4-0 vs FC Platinum, Simba bado hawajataja sababu kamili ya kuachana na Sven lakini imesema kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Selemani Matola atakaimu nafasi ya Sven kwa sasa hadi hapo atakapotangazwa kocha mpya ambapo Simba imesema ni ‘hivi karibuni’
20210108_040443.jpg
 
Boss wa SpaceX na Tesla, Elon Musk sasa ndio Tajiri namba moja duniani, hii ni baada ya kupanda kwa mauzo ya share za kampuni yake ya magari ya umeme (TESLA) leo Alhamisi, kabla ya hapo Tajiri namba 1 alikua Jeff Bezos.

Elon ambae ni Baba wa Watoto 7 (mmoja Marehemu) ana umri wa miaka 49 na ni mzaliwa wa Pretoria South Africa, utajiri wake leo umetajwa kufikia Dola za Kimarekani BILIONI 185.
20210108_040748.jpg
 
Jeshi la Polisi limewafukuza kazi Askari wake wanne kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu, ikiwemo kupokea rushwa, wizi na kukutwa na bangi na pombe haramu.

RPC Arusha, Salumu Hamduni amesema kuwa Askari hao walifikishwa kwenye Mahakama ya kijeshi na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa Mahakamani kama Watuhumiwa wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu.

Askari hao ni Heavenlight Mushi aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Kinondoni, Gasper Paul kitengo cha Intelijensia Makao Makuu na Bryton Murumbe aliyekuwa Askari wa kawaida Dodoma wanaotuhumiwa kumteka na kumuomba rushwa mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha,Sammy Mollel na kujipatia Tsh. Milion 10 .

Mwingine aliyefukuzwa kazi ni Koplo William Joseph Mkazi wa Muriet Arusha ambaye alikamatwa nyumbani kwake akiwa na misokoto ya bangi, pombe ya viroba, gongo na umeme wa wizi.
20210108_040925.jpg
 
Jeshi la Polisi limesema limebaini uwepo wa Wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kufungua Maduka madogo na wengine kufanya biashara zao kwenye maghala bila kulipa kodi hivyo Jeshi hilo kwa kushirikiana na TRA watafanya msako Nchi nzima wa wakwepa kodi na wanaokaidi kutumia mashine za EFD.

“Tutafanya msako pia kwenye maghala tukikuta Watu wanafanya biashara huko na kukwepa kodi watakabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi”
20210108_041413.jpg
 
Mgombea Urais Uganda Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) amewahakishia Watoto wake nje ya Nchi baada ya kupata taarifa kuwa kuna Watu wanapanga kuwateka, pia amesema kuelekea Uchaguzi Mkuu ameendelea kuimarisha ulinzi kwa kuvaa kofia ngumu na vazi la kuzuia risasi kwakuwa anawindwa.

Kuhusu Watoto, Bobi amesema aliambiwa kuhusu nafasi za kuwapeleka Watoto Ufaransa na Nchi nyingine za Ulaya baada ya Bobi Wine kudai kupata taarifa hizo.
20210108_041542.jpg
 
FB na Twitter wamezifungia kwa muda account za Trump na sasa hatoweza kupost chochote kutokana na kukiuka kanuni za Mitandao hiyo, adhabu hizi zimekuja baada ya Wafuasi wake kuvamia Bunge na fujo zilizosababisha vifo vinne.

Twitter wameifunga asiweze kupost kwa saa 12 na wamemuonya kuifunga kabisa akiendelea kukiuka kanuni za Mtandao huo,

Kampuni hiyo ya mawasiliano pia iliilazimu Timu ya Trump kufuta tweet tatu ikiwemo video fupi ambayo Trump aliwahimiza Wafuasi wake kwenda nyumbani lakini akirudia madai yake kuwa uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.
20210108_041918.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom