Badili mtazamo, hamisha nguvu na akili hiyo hiyo unayoitumia kwenye mambo ya ovyo yanayochochea MATUMIZI, Ipeleke nguvu hiyo kwenye mambo ya msingi yanayochochea UZALISHAJI. Change attitude. Nguvu unayoitumia kumshawishi mtu usiyemjua ili akukubalie kimahusiano, itumie nguvu hiyo hiyo, jitihada hizo hizo kutafuta na kuwashawishi wateja wanunue bidhaa yako na wanunue kwako siku zote wasikuache. Muda unaoutumia kuchati na wapenzi mitandaoni mara kwa Mara, utumie muda huo ku-close deal na wateja wako wa mtandaoni ili uzalishe pesa.Nguvu unayoitumia kubembeleza Mwenza asikuache tumia nguvu hiyo kuwabembeleza wateja wasiache kununua kwako. Your lifestyle is a full package of business requirements