Makapuku Forum

Makapuku Forum

Real Madrid: Julen Lopetegui nje !!
Screenshot_20181030-084323.jpeg
 
Binti wa mfalme wa Japan, Ayako amejivua cheo chake na kuacha maisha ya kifalme kwa kukukubali kuolewa na mpenzi wake ambaye si kutoka kwa jamii ya kifalme, Kei Moriya.

Sherehe hiyo ya kufana iliandaliwa katika hekalu la Meiji lililoko mjini Tokyo. Sheria za kifalme nchini Japan zinamhitaji yeyote atakayeoana na mtu asiyetoka kwenye kasri, aache ufalme
Screenshot_20181030-084543.jpeg
 
Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel hatatetea wadhfa wake kama kiongozi wa chama cha CDU katika kongamano la wajumbe linalopangiwa kufanyika mwezi Desemba. Bi Merkel amekiongoza chama hicho tangu mwaka 2000.

Aidha Kansela huyo pia amesema muhula utakaokamilika 2021 ndio wake wa mwisho kama kiongozi wa Ujerumani.

Merkel anasema anawajibika kufuatia matokeo duni katika uchaguzi uliodhihirisha kudorora kwa nguvu na umaarufu wake na chama chake CDU.
Screenshot_20181030-084656.jpeg
 
Msemaji wa waziri wa maswala ya ndani wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba amekiri video ya utupu inayosambaa katika mitandao ya kijamii iliibiwa kutoka kwa simu ya waziri huyo na maafisa wa usalama ambao baadaye waliwapa wanasiasa wa upinzani.

”Afisa mmoja wa usalama alijaribu kumshinikiza waziri awalipe la sivyo waiachie mitandaoni na alipokataa wakawapa wanasiasa wa upinzani” alisema Vuyo Mkhize.
Screenshot_20181030-084808.jpeg
 
Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi,
pamoja na wenzake watatu wameshinda tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mwaka huu wa 2018.

Rebeca na washindi wengine watatu wa mwaka huu watapatiwa tuzo yao mjini New York, Marekani tarehe 10 Desemba mwaka huu, wakati wa kilele cha tamko la haki za binadamu la umoja wa mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 70.
Screenshot_20181030-084917.jpeg
 
Watu 189 waliokuwa ndani ya ndege ya shirika la Lion ya Indonesia wanahofiwa kufarika baada ya ndege hiyo kuanguka baharini muda mchache tu baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta Indonesia.

Ndege hiyo mpya JT 610 aina ya Boeing 737 MAX 8 ilikuwa safarini kuelekea Pangkal Pinang, kwenye kisiwa cha Bangka Belitun ilipotoweka kwenye mitambo ya radar.
Screenshot_20181030-085049.jpeg
 
Kanisa la Full Combat Jerrycan ni kanisa linalohudhuriwa na walevi katika Kijiji cha California mjini Lodwar, Kaskazini mwa Kenya.

Kanisa hilo hufanya ibada zake chini ya mti, na waumini wake huhudhuria wakiwa walemewa baada ya akunywa pombe za kienyeji (Kaada)
Screenshot_20181030-085421.jpeg
 
Tanzania na Rwanda zitaanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka hadi Kigali Disemba mwaka huu, mradi ambao utagharimu TZS bilioni 5.7.

Wakati #Tanzaniaikitafuta mkopo kufadhili ujenzi huo, serikali ya Rwanda itashirikiana na sekta binafsi (PPP) kufadhili ujenzi huo.
Screenshot_20181030-085615.jpeg
 
Rais Dkt Magufuli amemteua Prof. Humphrey P. B. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani nchini (The Fair Competition Commission - FCC). Prof. Moshi ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Screenshot_20181030-085738.jpeg
 
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini #Uganda, Cyprian Kizito Lwanga amependekeza wafanyakazi ambao ni Wakristo wakatwe 10% kwenye mishahara yao kila mwezi kama fungu la kumi, na fedha hizo ziwasilishwe kanisani.


Screenshot_20181030-085859.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom