Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kwakweli akakafute wa level za masai sasa kaka chige inabidi unipe laki 4 ninunue Peruvian hair
We ushamba sijui utakutoka lini... ndo maana unahongwa nywele za Kimasai! Unaponiomba Peruvian Hair unatakiwa kuniita binamu na unapotaka chips mayai ndo unaita kaka! Basi usikonde binamu, naja kwenu next week!
 
Pendezesha makalio yako kwa kufanya haya

Makalio yetu ndiyo yanayotoa shepu fulani kwa mwanamke katika vivazi na ukiyaachia ovyo yanaweza kukuletea mushkeli na kama ukiyatengeneza hata yale makalio yanayosifiwa sana.
Wanawake wengi kwa sasa wanapenda kurekebisha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa jinsi wao wanavyopenda.
 
Tatizo hili halipo hapa nchini lakini wapo walionitupia swali na sasa inabidi nikiri kuwa lipo sana Marekani na mpasuaji wa masuala ya urembo wa Miami Dk Constantino Mendieta amethibitisha.
Mtaalam huyu amezungumzia sana utunzaji wa makalio daraja la kwanza ndiyo yanayotakwa sana. Ni kama vile umeuchukua moyo halafu ukaugeuza chini juu,haya ndio dizaini ambayo Marekani wanalilia sana.
Watu wa huko wanajimwaga katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu, na anayewachengua sana.
Kama unataka kuwa na shepu bomba fuata hatua zifuatazo:


1. Fanya masaji na losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi nyororo katika mapaja yako,ukianzia chini ya makalio mara mbili kwa siku.
 
Ondoa miinuko midogo midogo isiyotakiwa nyuma yako kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki ukiwa na salt scrub.


Pamoja na matatizo ya michuchumio,ivae ili kukupata nafasi ya kutembea kwa miondoko ya twiga inayotoa nafasi nzuri kwa makalio kuwa na mvuto.


Tafuta namna nzuri ya kuficha michirizi ya kunyooka kwa misuli ya mwili.
 
Mazoezi yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi, pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na kisha chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu ya kiuno kwa kusukuma kwa ndani na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo unavyotaka.
Pia unaweza kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha kwamba unakula vyema na unakula lishe inayostahili.
 
Mwanaume kuwa na ngozi nzuri huleta furaha, kujiamini
HAIJALISHI unafanya kazi kwenye mazingira gani lakini cha muhimu ni kuzingatia unatunza vizuri ngozi yako ya uso ili kuboresha muonekano wake. Mwanaume kuwa na ngozi nzuri huleta, furaha na kujiamini pia . Muonekano mzuri usoni ni miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanatakiwa kuyazingatia na hili linawezekana kama utaijali ngozi yako na utanashati kwa jumla.
 
Kuna wanaume ambao hawana hata muda wa kujiangalia kwenye kioo labda kwa kudhani kuwa mambo hayo yanatakiwa kufanywa na wanawake jambo ambalo si sawa sawa. Kuna mambo mengi ambayo mwanaume anatakiwa kufanya ili aweze kuonekana na muonekano mzuri. Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha unasafisha uso na kutakata, hapa unaweza kutumia taulo laini kwa kupaka kidogo sabuni na kisha safisha uso taratibu na baadaye unasuuza uso na kuufuta.
 
Pia unaweza kutumia cleanser ambayo ni maaluma kwa ajili ya kusafisha uso. Si jambo la ajabu unapopita kwenye saluni na kukuta wanaume wakisafishwa uso au kufanya scrubing ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia kuondoa madoa usoni, mafuta na kufanya ngozi ipendeze.


Unaposafisha uso unaruhusu vitundu vya kutolea hewa kubaki wazi na hivyo kufanya ngozi kuwa na afya nzuri na hata muonekano wake kuwa bora zaidi. Jitahidi kusaifisha uso na kufanyia scub uso wako japo angalau mara mbili kwa wiki jambo hili kwa kiasi kikubwa husaidia kuondoa seli zilizokufa kwenye ngozi. Pia hufanya kuwa laini na ya kuvutia. Unaweza kupaka loshen au cream za kiume ambazo zipo madukani kwa ajili ya kuboresha zaidi ngozi yako.
 
UVAAJI wa sketi fupi mara nyingi hutegemea na matakwa ya mavaaji,



kwani mara ntingi sketi fupi huishia juu ya magoti na huwa na urefu usiozidi sentimita 10.
Vazi hili mara nyingi huvaliwa na wanawake wa nchi za magharibi pia utamaduni huu umeenea sana hapa nchini ambapo wanawake na wasichana wengi wamekuwa wakivaa aina hizi za nguo na kuonekana kuwa wanakiuka maadili ya Kitanzania.
 
Wataalam wa mavazi wanasema, chimbuko la sketi fupi ni huko London Uingereza katika miaka ya 1960 ambapo wanawake walikuwa wakivaa nguo hizo katika michezo mbalimbali na wakati huo nguo fupi zilikuwa zikijulikana kama nguo za michezo kwani zilikuwa zikivaliwa sana na wacheza tenisi.
 
Wengi wanaovaa aina hiyo ya nguo wamekuwa na sababu tofauti huku wengine wakidai kuwa vazi hili hufanya wajiamini zaidi huku wengine wakidai kuwa sketi fupi hufanya wajione bomba zaidi na kuonekana wanakwenda na wakati.
 
Sketi fupi zipo kwenye fasheni miaka nenda rudi japo watu wengine wamekuwa wakivaa nguo hizo zikiwa fupi sana na kuleta mtafaruku hata pale wanapokuwa wanapita barabarani.

Muhimu kuhakikisha kuwa unapochagua nguo ya kuvaa angalia kama inaendana na mazingira na utamaduni wa Mtanzania na je nguo yake umevaa mahali gani na kama unaona ni kero unapofanya hivyo basi unashauriwa kuacha kufanya hivyo.
Wengi wanavaa sketi fupi na viatu virefu huku wakitembea umbali mrefu hali inayosababisha kupoteza maana na heshima pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom