Makapuku Forum

Makapuku Forum

Idara ya Afya, Halmashauri ya Mji Masasi imepiga marufuku kwa watumishi kutumia neno "Boss" kuwaita viongozi, kwani neno hilo sio fasaha na halipaswi kutumiwa kwenye ofisi za umma.
Screenshot_20181012-110055.jpeg
 
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed akipiga 'push-ups' na wanajeshi walioandamana hadi ofisini kwake wakidai kuongezewa mshahara.

Kiongozi huyo aliwaambia, serikali haiwezi kulipa mishahara mikubwa, kwa sababu fedha zimeelekezwa kwenye shughuli za maendeleo.

Hahhahahhah kafanana na mwafulani kila kitu kimeekekezwa kwenye maendeleo
Screenshot_20181012-110156.jpeg
 
Serikali mpya ya Sierra Leone imesitisha mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mamamah uliopitishwa na serikali iliyokuwa madarakani.

Uwanja huo unaogharimu TZS bilioni 915, ulikuwa unafadhili na China. Serikali imesema haina uwezo wa kulipa mkopo huo.
Screenshot_20181012-110503.jpeg
 
Vijana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 25 wanaongoza kwa magonjwa ya akili nchini, kutokana na mitindo ya maisha, matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa pombe.

Dkt Enock Changalawe amesema, matatizo ya afya ya akili kwa asilimia kubwa huwakumba wanaume kuliko wanawake
Screenshot_20181012-110620.jpeg
 
Japan ndiyo nchi yenye pasi ya kusafiria (passport) yenye nguvu zaidi dunia. Ukiwa na pasi hiyo unaweza kutembelea nchi 190 bila visa au kupata visa unapofika.

Nafasi ya pili inashikwa na Singapore na Ujerumani ya tatu. Pasi ya Tanzania imeshika nafasi ya 74 kwa uimara duniani.
Screenshot_20181012-110806.jpeg
 
Corinne Hutton (48) ameweka historia baada ya kuwa mtu wa kwanza mwenye ulemavu wa mikono na miguu (amewekewa miguu ya bandia) kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Alipoteza mikono na miguu baada ya kuugua mwaka 2013. Alifika kileleni Oktoba 5 akitumia siku 5 kupanda
Screenshot_20181012-110918.jpeg
 
Idara ya ulinzi ya Marekani imesitisha operesheni zote za ndege aina ya F35B kufuatia ajali ya kwanza iliyohusisha ndege hiyo mwezi uliopita huko South Carolina.

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo huku ripoti moja ya seneti ikikisia kuwa mfumo wa kielektroniki ya ndege hiyo inaweza kudukuliwa kwa urahisi.

Ndege hiyo inayogharimu takriban dola milioni 100 ndiyo ghali zaidi duniani.
Screenshot_20181012-111101.jpeg
 
Takriban watu 40 wameripotiwa kufariki katika wilaya ya Bududa Mashariki mwa Uganda baada ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko kusababisha mto Tsuume kuvunja kingo zake na kusomba takriban nyumba 100.

Shughuli za uokoaji zinaendelea. Hii sio mara ya kwanza kwa maafa kama haya kukumba eneo hili, Mwaka wa 2010 takriban watu 300 waliofariki baada ya tope kufukia kijiji kimoja karibu na Mlima Elgon.
Screenshot_20181012-111206.jpeg
 
Ulimwengu unaenda wapi?
Watu wanne wamekamatwa na polisi nchini Indonesia baada ya akaunti moja ya mtandao wa Instagram waliokuwa wanamiliki kugunduliwa kuwa ilikuwa inauza watoto!

Picha za wanawake wajawazito, na picha za watoto zilitumika kunadi viumbe hivi vya mwenyezi Mungu. Mtoto mmoja alikuwa anauzwa kwa dola $985 za Marekani.
Screenshot_20181012-111319.jpeg
 
Serikali ya rais Paul Kagame wa Rwanda kwa ushirikiano na shirika linaloshughulikia wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR imeanza kutoa hati za kusafiria kwa wakimbizi waliomo ndani ya mipaka yake.

Hati hiyo ya kielektroniki inayokubalika kimataifa itawawezesha wakimbizi kusafiri nje ya nchi hiyo kwa urahisi.
Rwanda ni mwenyeji wa takriban wakimbizi elfu 150.
Screenshot_20181012-111439.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom