Makapuku Forum

Makapuku Forum

.
Screenshot_20181012-102759.jpeg
Screenshot_20181012-102814.jpeg
 
Mariana Trench ndiyo sehemu yenye kina kirefu zaidi Duniani, jambo la kushangaza ni watu watatu tu ndiyo waliofanikiwa kutembelea sehemu hiyo akiwamo na James Cameroon muongozaji maarufu wa filamu Duniani (Titanic), mpaka sasa watu waliofika chini kabisa ya Mariana Trench ni wachache kuliko watu waliotembelea mwezi.
Screenshot_20181012-105550.jpeg
 
Chombo dada cha Voyager 1 kinachofahamika kama Voyager 2 nacho kipo mbioni kuungana na ndugu yake kwenye anga la ndani zaidi linalofahamika kama Intersteller Space.

Vifaa vilivyofungwa kwenye Voyager 2 vimeanza kupokea asilimia 5 ya miale ya cosmic, ambayo inapatikana kwenye ukingo wa mfumo wetu wa Jua unaofahamika kama Heliopause au kwa jina lingine Heliospere, kwa sasa chombo hicho kinatarajiwa kupita Heliospere na kuingia kwenye anga la ndani zaidi na kuagana na Jua letu kwa mara ya mwisho kikielekea ndugu yake alipo Voyager 1.

Kama ulikuwa haufahamu Voyager 1 na Voyager 2 ndiyo vyombo pekee kuwahi kutengenezwa na binadamu ambavyo vimetembea umbali mrefu zaidi kutoka Duniani, Voyager 1 na 2 vinatarajiwa kufikia umbali wa mwaka mmoja wa mwanga au sawa na kilometa trilioni 9 (maili trilioni 5) kutoka Duniani ndani ya miaka 40,000 ijayo na huenda vikaifikia nyota iliyopo karibu na Jua letu Alpha Centauri. Katika Voyager 1 kumewekwa CD ya dhahabu iliyowekwa rekodi za sauti za wanyama, watu, magari, ndege, n.k pamoja na ramani inayoelekeza Dunia yetu ilipo endapo kama itatokea chombo hicho kikatua mikononi mwa viumbe wengine (Aliens).
Screenshot_20181012-105757.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom