Makapuku Forum

Makapuku Forum

TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kutuamsha salama leo ALHAMIS Tarehe 11 oktoba 2018..Asante kwa pumzi hii Baba tunakuomba endelea kutulinda na kutusaidia tukutumikie Mfalme wa Amani maana wapo wengi walitamani kuiona siku ya leo wakiwa na mipango mingi na mizuri hawajaweza.Tunaomba Toba kwa yote tuliyoenda kinyume na Mapenzi yako kwa Mawazo Maneno na Matendo Uturehemu Eee Baba .Tunaomba Roho Mtakatifu Kaa nasi tufundishe kuwa wanafunzi wema tupiganie tuwe na mioyo safi ili siku ya mwisho tuingie Mbinguni.Asante kwa uponyaji wa wagonjwa Baba ..Endelea kutuimarisha miili na Roho zetu tuwe salama.Asante kwa Ufariji kwa wafiwa Baba endelea kuwa faraja kuu kwa wajane,wagane na yatima tupe tumaini lidumulo.Asante kwa Umoja,Upendo na Ushirikiano katika Mahusiano, familia na makundi mbalimbali Endelea kutupa moyo wa kuvumuliana na kumuona kila mmoja ni muhimu katika maisha haya.Bariki kazi za mikono yetu.Tunawafunika kwa damu Takatifu watoto na wajukuu wetu waendelee kuwa salama miili na Roho.Epusha wimbi la wizi wa watoto Baba Tunazifunga Roho zote za giza zinazoshiriki wizi huu ,zishindwe katika jina la Yesu Kristo na watoto wote waliopotea wawe salama na warudi kwao salama.
Baba Asante kwa Neema na Baraka zote unatugusa kwa namna ambayo hailezeki Asante kwa Upendo wa hali ya juu ambayo hauelezeki. Tunakushukuru kwa ajili ya Imani tuliyonayo kwako inatupa Amani na hakika Baba hatuna tunayemtegemea zaidi yako Yehova.Tunakabidhi kazi zetu,ratiba zetu ,mawazo yetu na kila tutakapo kuwa leo uwepo.Tunaomba kibali katika kika tufanyalo.
Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen

ALHAMIS NJEMA NA SHUKURANI KWA MUNGU KWA YOTE ANAYOTUTENDEA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
Ameeen
 
Asante Shunie kwa magazeti na Je, Wajua, shukrani kwako The Book kwa tetesi za soka nikujulishe tu Captein JT tayari kapewa mikoba ya ukocha msaidizi pale Aston Villa- jembe na beki kisiki.
Asante Numbisa kwa makala nzuri za ufahamu na hasa mambo yanayokera kwenye vyombo vvya usafiri.
Unakutana na mtu anatafuna jojo (bazoka-big g, aka chewing gum) utasema mtu mwenye tumbo la maji machafu

Asubuhi njmea wadau
Shikamoo binamu
 
He he eti huwezi ishi bila yy pumbavuuuuu jitu mmekutana ukubwani
2.Siwezi Kuishi Bila Yeye
Inaweza kuonekana ni ngumu lakini kila binadamu ameumbwa akiwa na utashi wake, na ukamilifu wa kuweza kuyaendesha maisha yake. Kinacholeta tofauti hapo ni namna gani umeuzoeza mwili/ mawazo yako kumtegemea mtu Fulani. Japokuwa siku zote tunaogopa kumkosa mtu huyo, cha ajabu ni kwamba, tunapomkosa tunakaa muda flani tu na kusahau yote licha ya kuvunjika moyo hapo kabla, na kuhisi moyo wako umenyofolewa kitu ambacho hakitarudi tena.
 
Acha mama aitwe mama
Huyu ndie Leleti Khumalo maarufu kama Sarafina ambae kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa Vitiligo unaoathiri ngozi yake, Sarafina aligundua ana tatizo hilo akiwa na miaka 24 na aliambiwa tatizo hilo lingekuwa kubwa akipata Mtoto ambapo alikubaliana na hali hiyo na kuamua kuzaa.View attachment 893679
 
.
Screenshot_20181011-102522.jpeg
 
. Idadi ya vijana wasiozidi umri miaka 25 wanaokunywa pombe imeshuka kwa kiwango kikubwa mno katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Utafiti uliojumuisha vijana 10,000 nchini Uingereza na kuchapishwa katika jarida la kiafya la BMC Public Health, umebaini kuwa Idadi ya vijana wa kati ya miaka 16 - 24 wasiobugia mvinyo imeongezeka kutoka asilimia 18% mwaka 2005 hadi 29% mwaka 2015.

Utafiti huu unathibitisha ushahidi wa awali kuwa idadi ya watu wanaojiburudisha kwa pombe inapungua kwa kasi nchini Uingereza.
Screenshot_20181011-110459.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom