Makapuku Forum

Makapuku Forum

Je wajua kuwa saratani ya matiti huwaathiri wanaume pia? ”Niliona uvimbe mdogo kwenye titi langu la kulia, lakini ulikuwa mdogo na haukuwa na uchungu sikudhani kuwa ulikuwa na madhara yoyote kwa afya yangu.

Lakini baada ya muda, uvimbe huo ukawa mkubwa, hali iliyonilazimu kutafuta ushauri was daktari.

Hapo ndipo nikaelezwa ninasaratani ya Matiti.
Nilishtuka sana.” Moses Musonga, 67, ni mmoja wa wanaume wanaougua saratani ya matiti
Screenshot_20181011-110626.jpeg
 
Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Nhlanhla Nene alijiuzulu wadhifa wake hapo jana baada ya kukubali kuwa aliwahi kukutana na familia ya Gupta ambayo inakabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Rais Cyril Ramaphosa amekubali uamuzi wa waziri huyo ili kulinda maslahi ya serikali.

Nene alikutana na wanafamilia wa Gupta katika vikao vya biashara zao nyumbani kwao ndani ya mwaka 2009 na 2014. Je hii ni njia mpya ya kufanya mambo Afrika Kusini?
Screenshot_20181011-110738.jpeg
 
Usafiri wa basi za mwendo kasi jijini Dar es Salaam umekumbwa na vurugu katika siku chache zilizopita.

Tatizo hilo lilizidi hapo jana ambapo mabasi yaliadimika sana na yaliyopatikana abiria walilazimika kung'ang'ania nafasi ndani.

Baadhi walitumia madirisha badala la milango, mradi tu wajipate ndani ya mabasi hayo.
Screenshot_20181011-110907.jpeg
 
Magazeti nchini Uturuki yamechapisha picha za watu 15 wanadaiwa walihusika katika kutoweka kwa mwandishi mwenye asili ya Saudia Jamal Khashoggi ambaye kwa mara ya mwisho alikwenda katika majengo ya Ubalozi wa Saudia nchini Uturuki.

Baadhi ya vipande vya picha za kamera za CCTV zinathibitisha eneo ambalo linahusika moja kwa moja na upoteaji wake.

Je rais Donald Trump wa Marekani atamsulubisha mshirika wake mkuu katika Mashariki ya Kati ama atasimamia haki Istanbul ?
Screenshot_20181011-111022.jpeg
 
Liverpool na Manchester United zimeanza kupigana vikumbo kumuwania kiungo mshambulaiji wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27.(London Evening Standard)
 
Liverpool na Manchester United zimeanza kupigana vikumbo kumuwania kiungo mshambulaiji wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27.(London Evening Standard)
 
Arsenal na United zitakutana na ushindani kutoka Bayern Munich katika kumshawishi winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Bild, via Talksport)
 
Arsenal na United zitakutana na ushindani kutoka Bayern Munich katika kumshawishi winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Bild, via Talksport)
 
Klabu ya AC Milan imezishinda mbio vilabu vya Liverpool na United kumsainisha kinda wa wa Flamengo na Brazil, Lucas Paqueta,21. (Sun)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom