Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu ndie Leleti Khumalo maarufu kama Sarafina ambae kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa Vitiligo unaoathiri ngozi yake, Sarafina aligundua ana tatizo hilo akiwa na miaka 24 na aliambiwa tatizo hilo lingekuwa kubwa akipata Mtoto ambapo alikubaliana na hali hiyo na kuamua kuzaa.
42627481_244295052922403_7657914176185825737_n.jpg
 
KAMA UNAFANYA HAYA BASI WEWE NI MMOJA KATI YA WATU WANAOUDHI ZAIDI KWENYE DALADALA

1. Kulala ndani ya daladala na kumuegamia mtu wa jirani, unamkwepa anashtuka na baada ya dakika moja anakuegemea tena! Mbaya zaidi anatoa harufu mbaya kukohoa na kupiga chafya bila kujizuia.

2. Harufu mbaya. Umepanda gari ghafla anaingia mtu kabeba mzigo wa samaki. Anaingia nao ndani na kukaa karibu na wewe. Au umekaa na mtu pembeni anaimba/kuongea na anatoa harufu kali mdomoni!

3.Mtu anaongea sana na kukulazimisha umsikilize. Au anataka kila mtu ndani amsikilize yeye. Anaongea kwa sauti kubwa na wakati mwingine, mate yanatoka kinywani.


4. Mmefika kituoni, ghafla anatoka mtu kutoka nyuma anapita kwa nguvu na kumkanyaga kila mtu na hasemi/ hakusema kama anashuka.

5.Mtu anakukodolea macho toka mwanzo mpaka mwisho wa safari. Kumzuia mtu huyu, na wewe mtazame sehemu mojawapo ya mwili wake(isiwe usoni ). na atakosa ujasiri huo tena
 
6. Matusi. Uko kwenye usafiri na mzazi au mwanao, ghafla watu wanaanza kuporomosheana matusi ya nguoni. Kwa kweli watu hawa huudhi sana.

7.kuchunguza simu ya mtu mwingine. Umekaa kwenye siti kuna mtu amesimama nyuma yako anachunguza kila unachokifanya kwenye simu yako, ukisogeza pembeni nayeye yumo!

8.Kuongea na Simu kwa sauti ya juu na kuanza kuongea mambo yako ya ndani, kujisifu au kutishia. Si kila mtu anataka ajue siri zako au pengine uwezo wako.

9.kula kwenye daladala. Umepanda na mtu amenunua muhindi, karanga, miwa nk na anaanza kula na kusababisha baadhi ya mabaki kukuangukia


10. Muziki. Si kila mtu anapenda aina ya muziki unayopenda wewe. Inaudhi umekaa na mtu amefungulia simu yake muziki kwa sauti au mahubiri ya dini Fulani kwa sauti kwa lengo la kuwaudhi watu wa dini nyingine!
 
MAMBO KUMI TUNAYOJIDANGANYA KILA SIKU (UNAHITAJI KUBADILIKA)

1.Ningeweza kufanya kama Ningekuwa na pesa
Japokuwa asilimia kubwa ya sentensi nyingi zinazoanzia na hilo neno hapo juu huwa kweli,
(mfano: ningekuwa na fedha ningenunua kisiwa nikae huko na familia yangu) lakini Muda mwingi watu wengi tumekuwa tunasingizia kukosa fedha hata kama hatukutimiza wajibu wetu!
Wengi huamini fedha ndio kila kitu katika maisha yao. Hata kama wangekuwa na uwezo wa kufanya suala Fulani bila ya fedha, huliacha bila hata ya kujaribu na kuona haliwezekani bila ya fedha!
“Money without brains is always dangerous”
 
2.Siwezi Kuishi Bila Yeye
Inaweza kuonekana ni ngumu lakini kila binadamu ameumbwa akiwa na utashi wake, na ukamilifu wa kuweza kuyaendesha maisha yake. Kinacholeta tofauti hapo ni namna gani umeuzoeza mwili/ mawazo yako kumtegemea mtu Fulani. Japokuwa siku zote tunaogopa kumkosa mtu huyo, cha ajabu ni kwamba, tunapomkosa tunakaa muda flani tu na kusahau yote licha ya kuvunjika moyo hapo kabla, na kuhisi moyo wako umenyofolewa kitu ambacho hakitarudi tena.
 
3. Nimeshazeeka Siwezi kufanya hili/ Umri wangu Bado!
Kwa utafiti mdogo, Nimegundua kuwa waafrika wengi husubiri wafike miaka 30 ndipo waanze kuvaa majukumu mengi (mfano Kuwa na familia, kujenga, kununua ardhi, usafiri nk) Na je umegundua kwamba wakifika umri wa miaka 40 hujiona wazee na kukata tama na kutojihusisha na kujifunza vitu vipya? “mambo ya vijana hayo” Na watu wengi wenye miaka zaidi ya 50 hujiona wamechelewa na teknolojia imeshawapita, kumbe maisha yamerahisishwa! Kama uliweza kujifunza mambo mengi magumu ambayo mpaka unajisifu kwamba vijana wengi wa sasahivi hawayawezi, kwa nini uogope kujifunza kutumia kompyuta, mitandao au simu za kisasa? Hujachelewa anza sasa!
 
4. Ntajaribu/Ntaonja Kidogo Tuuu!

Shauri yako!



5.Laiti ningekuwa na muda ninge…
Pengine unayawaza haya huku umekaa sebuleni, ni asubuhi na bado unanguo za kulalia, unaangalia darini ukiwaza ungekuwa na muda ungefanya moja, mbili, tatu! Mara Nyingi Tumekuwa Tukipoteza Muda wetu mwingi Tukiandaa orodha ya mambo ambayo Tungeyafanya kama tungekuwa na Muda!
 
6.Mimi naliweza hili sio lile (am good at this, not that!)

Pengine Kwa kuogopa Kudhubutu Wengi wetu Huamini kwamba uwezo wetu ni katika mambo kadhaa tu, na aina Fulani ya majukumu ni kwa ajili ya watu Fulani. Na mimi naweza kitu Fulani mpaka awepo mtu Fulani!

7. Kesho
Hakuna neno la uongo kama neno “kesho” wengi wetu huwa wavivu na kujipa moyo kwa kuwa tu kuna kesho! Tutaacha viporo vya kazi, masomo n kusahau kwamba kesho bora ni ile itakayozalisha kitu chake na si itakayofanya mambo ya leo!
 
8. Kuhisi Mapungufu yetu tunayajua wenyewe!
Wajua mtu wako wa karibu sana anayajua mapungufu yako pengine kuliko wewe? Wengi wetu huwa tunajiona tuko sawa upande Fulani na kuhisi mapungufu yetu tunayajua wenyewe! Hii husababisha kutokukubali kama tumekosea na kwamba tunamapungufu katika hilo!. Ukweli ni kwamba, ukiona mtu zaidi ya mmoja anakueleza juu ya tatizo lako Fulani, hata kama unajihisi huna tatizo upande huo, jaribu kubadilika!
 
9. NAJUA NINACHOKIFANYA!!

Haya bwana!... Ndio unajua, niseme nini tena!







10. Sio Hadhi yangu!
Pengine kwa kuhisi unamapungufu Fulani basi huwezi hata kujaribu kufanya jambo Fulani au una uwezo Fulani basi kwa hili sio hadhi yangu, wanastahili hadhi ya chini sio mimi.!

SI KWELI. BADILIKA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom