Habari zinazotufikia kutoka Magharibi mwa Kenya zinasema kuwa basi moja la uchukuzi wa umma limeanguka katika eneo la Fort Tenan lilipokuwa likielekea Kakamega.
Takriban watu 42 wamefariki.
Kilichosababisha ajali hii hakijabainika.
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini humo Bi Bella Bird kuzungumzia miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia.
Hata hivyo, utata bado unaendelea kuhusu msaada wa dola 50 milioni za Marekani ambazo benki hiyo ilikuwa inatarajiwa kutoa kwa taifa hilo.
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa UN Nikki Haley amejiuzulu takriban miaka miwili tangu achukue mikoba ya kumwakilisha rais Donald Trump na sera zake katika maswala ya kidiplomasia katika ulingo wa UN.
Trump amemsifu kwa ukakamavu wake na kumuahidi wadhfa wowote katika siku za usoni
"Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu.
Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Lulu Jemimah mwenye umri wa miaka 32 aliyejioa mwezi Agosti jijini Kampala na kudai kuwa kwa miaka kadhaa watu wamekuwa wakimuuliza kuwa lini angefunga ndoa.
Nada Zaelnoon Ahamed (raia wa Sudan Kusini) na Mohamed Belal (raia wa Syria) wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakisafirisha USD 70,000 na Paundi 3,410 za Sudan bila kufuata taratibu.
Sheria inataka ukiwa na fedha kuanzia USD 10,000 ujaze fomu ya maelezo kuhusu fedha hizo.
Watuhumiwa wote wawili wamezuiwa na hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zilizopo
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa, huenda Pancho Latino alizidiwa na pombe wakati akiogelea kwani walipoopoa mwili wake kutoka baharini na kuugandamiza, pombe nyingi ilitoka.
Imeelezwa, alikaa ndani ya maji kwa dakika 10, hali iliyowashtua watu, na walipomwendea akawa amefariki dunia
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.