
TUOMBE:Baba yetu na Mungu wetu tunakuja katika kiti chako cha enzi tukinyenyekea kwa shukurani kutuamsha salam leo Jumanne tarehe 9 Oktoba 2018..Asante Baba kwa wema wako na fadhili zako zisizo na mwisho ,wako wengi walitamani kuiona siku ya leo. Hawajaweza. Tunakuomba utusamehe yote tunayoenda kinyume na mapenzi yako uturehemu Baba maana tunakutegemea wewe tu.Bariki kuingia na kutoka kwetu,ponya wagonjwa miili na Roho zetu iwe salama.Walinde watoto na wajukuu zetu wawe salama ..wasafiri nchi kavu ,majini,angani waende na kurudi salama..Bariki familia ziwe na amani..wape faraja wafiwa na tumaini wajane,wagane na yatima .tusadie tuendelee kusema ndiyo kwako kwako Baba imarisha imani yetu ..Tunakuomba Baba onekana katika kila hatua ya maisha yetu na kila tunapokuwapo leo uwepo na utuimarishe katika mambo yote.Tujaze roho ya upendo na tutende yatupasayo kutenda kwa utukufu wa jina lako takatifu.Epusha ajali zote za miili na roho.Bariki kazi za mikono yetu zizae matunda ya kukupendeza..Bariki Nchi yetu imarisha Amani,Umoja na Mshikamano.Baba Asante maana utatenda sawa na mapenzi yako Roho Mtakatifu kaa nasi daima.. tunaomba na kuamini katika jina la Yesu Kristo Amen
JUMANNE NJEMA YA AMANI DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
