Makapuku Forum

Makapuku Forum

*Manahodha wa Mashua kwanini wakae nyuma??*

Hayuko asoyajua haya n'nayoyasema,
Vyombo vya kusafiria huenda mbele daima,
Nahodha twategemea, awe mbele akinema,
Manahodha wa mashua kwanini wakae nyuma?

Manahodha wa mashua na ngalawa mna dhima,
Sukani mwashikilia na hali mkiwa nyuma,
Ajali ikitokea nani ajibu lawama?

Kuwa mbele abiria nahodha akawa nyuma,
Ni kinyume cha sheria, kimwendo na usalama,
Nawaomba kuchungua ingawa ya tangu zama

Nahodha nakushauri uwe mbele sio nyuma,
Ndipo mimi n'takiri kuwa safari salama,
Bila hivyo sisafiri naichelea dhahama

Nahodha kakae mbele abiria tuwe nyuma,
Uvikwepe vipengele chombo kisiende mrama,
Tupige vigelegele tukishafika salama.. Salama!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom