Makapuku Forum

Makapuku Forum

Diane Rwigara na mamake wako huru
Screenshot_20181005-183102.jpeg
 
Mahakama mjini Kigali Rwanda imeamua kumuachilia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani bi Diane Rwigara na mamake na watafwatiliwa wakiwa nje ya gereza.

Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi mahakama hati ya kusafiria mbali na kuwekewa kikwazo asivuke mipaka ya jiji la Kigali bila kibali maalumu.

Baada ya uwamuzi huo umati wa mashabiki wake na jamaa zao umeimba na kusherehekea mahakamani huku wakimsifu mwenyezimungu kwa uamuzi huo.

Diane na Mamake walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kugushi nyaraka. Wamekanusha madai hayo wakisema wakisema yana misingi ya kisiasa.
Screenshot_20181005-183313.jpeg
 
Wafanyakazi wa kampuni ya kuuza betri za gari nchini Kenya wamezua mjadala mkali mitandaoni baada ya kuvalia kama wanawake kazini kama sehemu ya kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya kiafya ya wanawake, na zaidi saratani.

Oktoba ni mwezi wa hamasa kuhusu saratani ya matiti.
Screenshot_20181005-183707.jpeg
 
Serikali ya Pakistan imeamuru mashirika yote ya kimataifa na yasio ya kiserikali kufungwa .

Mashirika hayo yameamrishwa kufunga virago vyao na kuondoka nchini humo katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Pakistan imekuwa na shauku kubwa dhidi ya mashirika haya tangu shirika la kijasusi la Marekani CIA kuendesha kampeini bandia ya kutoa chanjo iliyotumika kumnasa aliyekuwa kiongozi wa al Qaeda, Osama bin Laden mwaka wa 2011.
Screenshot_20181005-183836.jpeg
 
Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Johannesburg Afrika Kusini kuelekea Hong Kong katika ndege ya shirika la ndege la Afrika Kusini SA286 walilazimika kustahimili aibu ya kupekuliwa ndege hiyo ilipotua HongKong baada ya baadhi yao waliokuwa wamelala kuripoti kuwa mali zao za thamani zilikuwa zimetoweka angani !! Na baada ya msako mkali ulioendeshwa na polisi wa Hong Kong , saa na pesa zilipatikana zimefichwa. Hakuna aliyekamatwa.
Screenshot_20181005-184021.jpeg
 
Wafanyakazi wa kampuni ya kuuza betri za gari nchini Kenya wamezua mjadala mkali mitandaoni baada ya kuvalia kama wanawake kazini kama sehemu ya kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya kiafya ya wanawake, na zaidi saratani.

Oktoba ni mwezi wa hamasa kuhusu saratani ya matiti.View attachment 887665
Mwanaume ukose vya kuhamasisha ndo ujifananishe?
Zambi sana
 
Leo Oktoba 5 ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walimu.

Siku hii ilianzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kutambua mchango wa walimu na kushughulikia kero zinazowakabili.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni, "Haki ya elimu ina maanisha haki ya kuwa na mwalimu

Screenshot_20181005-184422.jpeg
 
"Gari la kubeba wagonjwa halipaswi kuendeshwa kwa mwendokasi, lakini inatokea hivyo kutokana na uchache wa magari hayo, pia madereva wengi kutofahamu taratibu za uendeshaji."- Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Upendo George.
Screenshot_20181005-184604.jpeg
 
Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe, kutokana na kuwa na mapungufu ya kisheria.

Viongozi hao walikuwa wanapinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu mwenendo wa kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Screenshot_20181005-184725.jpeg
 
Afya Yako:

Njia rahisi ya kupata mtoto wa jinsia uitakayo ni kufuatilia vizuri kalenda ya mzunguko wa hedhi ya mama.

Mara nyingi mtoto wa kiume hupatikana siku mwanamke ameanza uovuleshaji na anahamu na mwanaume.

Lakini upandikizaji wa mbegu ndio njia ya uhakika zaidi
Screenshot_20181005-184829.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom