
TUOMBE:Mungu wetu tuna kila sababu ya kushukuru kutuamsha salama leo Jumatano tarehe 3 Octoba 2018..wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza.Tunaomba toba kwa makosa yote tuliyotenda kwa mawazo maneno na matendo uturehemu twakusihi.Tunakabidhi ratiba zetu ..tunakabidhi familia zetu kaa nasi Baba.ponya wagonjwa,waliovunjika mioyo wafariji wafiwa ,wajane wagane na yatima wape tumaini.Tunaomba walinde watoto wetu na wajukuu wetu waepushe na pepo baya na wimbi la kuibiwa tunawafunika kwa damu takatifu ya Kristo nazifunga roho zote za giza.
Tunaomba walinde wasafiri wote majini ,nchi kavu,angani waende na kurudi salama ..tunaomba Amani na umoja katika Nchi yetu.
Roho Mtakatifu kaa nasi tufundishe na tuongoze katika kila hatua..Asante Baba maana wewe ni mwema utatenda sawa na mapenzi yako Amen...
JUMATANO NJEMA YA AMANI DAMU TAKATIFU YA KRISTO YESU ITUFUNIKE

