Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema amesema kitendo cha kufukuzwa kwa Profesa wa sheria na mtoa mihadhara maarufu kutoka Kenya, Prof PLO Lumumba kutoka Zambia kutokana na sababu za 'kiusalama ni cha aibu kwa Zambia na wazambia wote”. Prof Lumumba, alikuwa ameratibiwa kutoa hotuba kuhusu ushawishi wa China barani Afrika katika chuo kikuu
Screenshot_20181002-181535.jpeg
 
Dar es Salaam Tanzania ni salama kwa wanawake kuliko Nairobi Kenya na Kampala Uganda.

Ripoti kuhusu usalama wa wanawake na wasichana dhidi ya udhalilishaji katika miji mbalimbali duniani uliofanywa na shirika la Plan International inasema.

Je unakubaliana na Utafiti huu
Screenshot_20181002-181653.jpeg
 
Je wajua kuwa Marekani wakati mmoja ilitaka kuulipua Mwezi kwa kutumia bomu la nyuklia ?

Lengo lao lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa Marekani kuiwezesha kuitia kiwewe Urusi na washirika wake wakati wa vita baridi, hasa baada ya Muungano wa Usovieti kuongoza katika jitihada za kupeleleza na kutalii anga za juu, hasa baada ya kurusha satelaiti ya kwanza kwenye mzingo wa dunia, satelaiti ya Sputnik 1 mnamo 4 Oktoba 1957
Screenshot_20181002-181803.jpeg
 
Mwanamfalme William amekamilisha ziara ya siku 7 barani Afrika kwa mechi ya kandanda na wenyeji wa Laikipia eneo la kati Kenya.

Ametembelea Namibia Tanzania na Kenya kupigia debe mkutano wa mataifa yaliyoko mstari wa mbele kupambana na biashara haramu ya bidhaa zitokanazo na wanyama pori.
Screenshot_20181002-181947.jpeg
 
Nchini Rwanda sheria mpya ya makosa ya jinai imeanza kutumika.
Miongoni mwa makosa hayo ni kosa la kudhalilisha viongozi wa serikali kwa kutumia maandishi au kuchora vibonzo.

Mchoraji atahukumiwa kifungo cha hadi miaka miwili gerezani na faini ya dola takriban elfu moja na mia tano.

Kosa la kudhalilisha rais wa nchi hiyo mhusika atahukumiwa hadi miaka 7 gerezani na faini isiyopungua dola elfu 8.
Waandishi wa habari wameingiwa na wasi wasi.

Aiseeee role model wake mtu
Screenshot_20181002-182054.jpeg
 
Serikali ya Israeli imekubaliana na Rwanda kufungua ubalozi wake jijini Kigali hivi karibuni katika jitihada za kuimarisha mahusiano baina yao.

Kauli hii ilifikiwa katika mkutano wa faragha kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kandokando ya mkutano mkuu wa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa UN huko New York Marekani.
Screenshot_20181002-183051.jpeg
 
iTakriban watu 384 wamethibitishwa kufariki baada ya Tsunami kubwa iliyosababishwa na tetemeko la ardhi kuikumba pwani ya Indonesia .

Mashuhuda katika eneo la Sulawesi wanasema mawimbi yenye kimo cha mita tatu hivi yalikumba maeneo yakiyokaribu na ufukwe wa bahari na kusababisha uharibifu mkubwa kwa muundo mbinu.

Jeshi la taifa hilo limeanza kuandaa mikakati ya uokoaji huku idadi ya waliofariki ikitaraj
Screenshot_20181002-185044.jpeg
 
Kanye West amebadili jina lake na sasa anaitwa Ye ! Je nini kinaweza kusababisha ubadilishe jina alilokupa baba mzazi ?
Screenshot_20181002-185218.jpeg
 
Cardi B amejisalimisha kwa polisi ilkufanikisha uchunguzi wa tuhuma kuwa walipigana na Nicki Minaj mwezi uliopita wawili hao walipokutana katika maonyesho ya New York Fashion.
Screenshot_20181002-185321.jpeg
 
Polisi nchini Kenya wamekamata zaidi ya dola milioni 10 katika nyumba moja inayomilikiwa na raia wawili wa Chad Pesa hizo zinaaminika kuwa ni ghushi.

Akidhibitisha tukio hilo mkuu wa kitengo cha flying squad Musa Yego alisema Abdoulaye Tamba, na AbdallaTamba kutoka Chad wamekuwa wakiwapunja wateja wao kuwa wanaweza kuwaombea wapate
Screenshot_20181002-185413.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom