Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tabia Za watu Waliofanikiwa Katika Mahusiano

1.Wako pamoja kwa sababu sahihi

2.Wana matarajio ya kweli kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi

3.Kitu cha muhimu kwao sio mawasiliano bali ni Heshima kwa kila mmoja



4.Wako wazi, huongea kila kitu wazi , hasa yale mambo yanayowaumiza.

5.Mahusiano yenye afya yana husisha watu wawili wenye afya.

6.Hupeana nafasi

7.Wewe na mwenza wako mnakua na kubadilika kwa njia zisizotarajiwa. kumbatia hilo

8.Mnapita katika mazuri na mapigano.

9.Mnapita katika mazuri na magumu lakini mnasameheana.

10.Vitu vidogo vinaongeza vitu vikubwa.

11. Sex matters…a lot.

12.Hutengeneza kanuni za kwao za mahusiano

13.Hujifunza kuyapiga mawimbi .
To be honest Numbi ulipaswa kuwa host wa kile kipindi cha mahusiano
 
.
Screenshot_20181002-175220.jpeg
 
Date na mtu ambaye anaweza kuacha simu yake mezani na kwenda zake chumbani, na wewe huna muda wa kuigusa simu yake kwa ajili ya kuangalia meseji.

Akilini mwako unajua kabisa hakuna kibaya kilichopo ndani ya simu yake, unafahamu kwamba hana tabia ya kumtumia mtu mwingine meseji, Unafahamu kuwa kipo chumba ndani ya moyo wake kwa ajili yako tu.
 
Date na mtu ambaye hata akichelewa kutoka kazini , au kutoka kwa marafiki zake usiku, na unakuwa huna wasiwasi naye. Mtu unayejua kwamba hawezi kukusaliti, hata kama tumbo lake limejaa vinywaji, mtu ambaye anaweza kusema ukweli alikokuwa, kwa sababu hataweza kukudanganya kitu.

Date na mtu ambaye hata kama akiwatumia marafiki zake wa kike meseji hutaweza kuwa na wivu, hata kama atakuwa ni mzuri sana kuliko wewe. huna wasiwasi kwa sababu hawezi kukuibia kutokana na uaminifu wa huyo mtu uliyenaye. Kwa sababu utakuwa unajua kuwa alikuchagua wewe kwa sababu. utakuwa unatambua kama akikuambia hakuna kinachoendelea na mtu huyo.Unaelewa kuwa ni kweli.
 
Date na mtu ambaye hutaweza kuwa na ndoto ya kuwa atakusaliti. kwa sababu unafahamu kuwa hataweza kukuumiza , kwa sababu ni wako na wewe wa kwake.

Mtu ambaye hutaweza kumuwazia mabaya anapokuambia kuwa ana safari kikazi, hutawaza itakuwaje huko aendako, hutafikiria kuwa anaweza kutafuta mtu wa kuwa naye chumbani.
 
Date na mtu ambaye utamwamini kiasi cha kutosha . Mtu mkweli. mtu muwazi, mtu muadilifu na madhubuti.

Mtu ambaye hawezi kuona aibu kukupatia password ya emails zake, simu zake , account zake. mtu ambaye anaweza kukuachia computer yake utumie. mtu ambaye yuko tayari kushare kila kipande cha maisha yake na wewe kama vile na wewe ulivyokubali kufanya hivyo hivyo.
 
Date mtu ambaye hawezi kukufanya ujisikie kuwa hufai hata sekunde moja. mtu ambaye hawezi kujilaumu kwa kuwa na wewe, mtu ambaye haoni ubaya kwako.mtu ambaye hatakuacha ufanye kitu ambacho utajisikia vibaya. mtu ambaye atajiona kukamilika akiwa na wewe na ukalifahamu hilo.

Mtu mwenye kufurahia kuvaa pete hata akiwa kazini au katika mazingira yote. Ambaye ataweka picha yako mezani kwake akiwa na wewe, kila wakati anatazama .mtu ambaye anajisikia furaha kukuita rafiki yake, mke wake au mchumba wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom