Makapuku Forum

Makapuku Forum

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida , Utakuwa unaficha hisia zako. Unacheza na ukweli. unakuwa unaonyesha kujali kidogo sana kuliko uwezo wako, kwa sababu sio mahali pa kudumu. Hautaki kuwa na nguvu kubwa hapo, kwa hio unakuwa unapretend.

Lakini kama upo kwenye mahusiao ya kweli, utaonyesha hisia zako bila ya kuficha .Utamwambia mtu huyo anapokuwa anavutia na kushangaza. Utamwambia unapotaka akukumbatie, akukiss, utamwambia jinsi gani unampenda. Utamfanyia anachostahili. Huwezi kuficha upendo ulionao kwake.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, unapima kila kitu mtu anapokuwa anafanya , hata kama ni kidogo. Hata kama atatuma ujumbe ambao hujaelewa, utaanza kulalamika, kila kitu unakichukulia tofauti, huna majibu . hata kama utaongea naye huwezi kujisikia vizuri.
 
Lakini unapokuwa kwenye serious relationship, utasema unachokimaanisha na kutegemea upande wa pili kusema vile vile.kama akikutumia ujumbe usioeleweka, utajiuliza ana maana gani. hautakuwa na shaka. utapata majibu sahihi, na mtaongea pamoja.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, unakuwa huelewi maana ya kuwa na huyo mtu.Kwa hio hutaweza kujua mipaka yake. Hutaweza kumwonyesha kwa watu, hutaweza kumpeleka nyumbani kwenu, hutaweza kukaa nae kwa muda mrefu usiku,Kwa sababu huna uhakika.
 
Lakini unapokuwa kwenye mahusiano ya kweli, unafahamu mipaka ya mwingine, na pia mipaka yako inakuwepo vizuri. utafahamu kitu gani wanakipenda na kipi hawakipendi. Utafahamu kabisa kuwa kuna kitu anatarajia kwako. unafahamu kabisa kuwa unahitaji kupata kitu cha furaha kutoka kwako.



Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, mara zote utakuwa huelewi. Maswali ya haraka, kutokuwa na uhakika wa hisia zako na hisia za mwingine, huna uhakika kama utaweza kuwa pamoja. huna uhakika kwa kila nguvu unayotumia kwa mtu huyo.
 
Lakini kama upo kwenye mahusiano ya kweli, Huna muda wa kuwa na shaka. Unajisikia vizuri kila unapokuwa naye.Kama vile ni mahali hasa ambapo ulitakiwa uwepo. Ni kama umefika nyumbani kwako.Mahali pa usalama.
 
Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida , Utakuwa unaficha hisia zako. Unacheza na ukweli. unakuwa unaonyesha kujali kidogo sana kuliko uwezo wako, kwa sababu sio mahali pa kudumu. Hautaki kuwa na nguvu kubwa hapo, kwa hio unakuwa unapretend.

Lakini kama upo kwenye mahusiao ya kweli, utaonyesha hisia zako bila ya kuficha .Utamwambia mtu huyo anapokuwa anavutia na kushangaza. Utamwambia unapotaka akukumbatie, akukiss, utamwambia jinsi gani unampenda. Utamfanyia anachostahili. Huwezi kuficha upendo ulionao kwake.

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kawaida, unapima kila kitu mtu anapokuwa anafanya , hata kama ni kidogo. Hata kama atatuma ujumbe ambao hujaelewa, utaanza kulalamika, kila kitu unakichukulia tofauti, huna majibu . hata kama utaongea naye huwezi kujisikia vizuri.
Shikamoo, umeongea point sana sana Numbi, hakuna future kwenye temporary ralationship ni kuzugana tu
 
Mahusiano ni sawa na kioo ,Mpasuko mdogo unaweza kuvunja kioo chote. Inahitaji umakini wa hali ya kipekee. Mahusiano yalio sahihi sio rahisi kudumu katika mafanikio.

Utahitaji kujikita na kujitolea kwa ajili ya hilo. Vitu vidogo ambavyo vinaleta kutokuelewana , ambavyo huwezi kushughulikia kwa urahisi vinaweza kuharibu mahusiano yako. Lakini wakati wowote inawezekana kuponya mahusiano yako, hata kama yalikuwa yanaelekea kuvunjika kabisa. kama hufanyi kitu , hakuna muujiza wowote ambao utakutokea ili uwe na mahusiano mazuri.

Wengi wetu tunajitahidi kila siku, iwe nyumbani , kazini , au katika masaa ya kati ukiwa popote . Mahusiano ni kipengele ambacho cha muhimu katika kila maisha ya mwanadamu. Jinsi gani utaweza kudumu katika mahusiano mazuri , ni katika majadiliano ya watu wawili.
 
Tabia Za watu Waliofanikiwa Katika Mahusiano

1.Wako pamoja kwa sababu sahihi

2.Wana matarajio ya kweli kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi

3.Kitu cha muhimu kwao sio mawasiliano bali ni Heshima kwa kila mmoja



4.Wako wazi, huongea kila kitu wazi , hasa yale mambo yanayowaumiza.

5.Mahusiano yenye afya yana husisha watu wawili wenye afya.

6.Hupeana nafasi

7.Wewe na mwenza wako mnakua na kubadilika kwa njia zisizotarajiwa. kumbatia hilo

8.Mnapita katika mazuri na mapigano.

9.Mnapita katika mazuri na magumu lakini mnasameheana.

10.Vitu vidogo vinaongeza vitu vikubwa.

11. Sex matters…a lot.

12.Hutengeneza kanuni za kwao za mahusiano

13.Hujifunza kuyapiga mawimbi .
 
Safisha Au ondoa Maji Yaliomo.

Mahusiano yanakuwa na maji pale mtu mmoja anapokuwa hawezi kuelewa au kukataa kukua, kutokana na kile walichojifunza,uzoefu au hisia zao. Mahusiano yalio na maji ni rahisi kuvunjika . Kunakuwa na uelewa mdogo, hakuna heshima, hawafurahii wenza wao, hata zile sifa za mwanzo zilizowafanya kuwa pamoja wanapoteza. Ukitazama kwa akili hawa watu wamebadilisha chujio lao la akili. Wanachukulia tofauti mitazamo , tabia na hisia za wenza wao. wanawafikiria tofauti kwa kila kitu.
 
Ili kuondoa maji yalioingia ndani ya mahusiano ,Itabidi wote wakubali mabadiliko na kukua kwa wenza wao, bila kujali mazingira.Kila mtu ajitahidi kwa upande wake.

Kumbuka kama mahusiano yako yameingia kwenye tatizo, haikutokea siku moja, unaweza kurekebisha, lakini itahitaji nguvu ya ziada, uvumilivu mkubwa na upendo wa kutosha ili kuponya mahusiano yako. Pamoja na kwamba , huenda kuna mmoja wenu amekata tamaa au hajakata tamaa, utahitaji ushauri wenye nguvu ili kurudi hali ya kawaida. Kwa sababu Upendo wa kweli unahitaji kupiganiwa.
 
Fanyia kazi vitu ambavyo unaona vinakusaidia kukuza mahusiano yako. Hasa katika vipengele vya Kiakili, kiroho, kimwili, kiuchumi. hivi ni vitu vya kuongea na mwenza wako wazi wazi . Usiogope kumweleza mwenza wako kitu ambacho hakileti furaha .Weka kipaumbele kwa kila mmoja wenu. Heshima ni kitu cha kwanza. Mshikilie mahusiano kwa pamoja, sio kumwachia mtu mmoja. Kujijali na kumjali mwenza wako. Kuaminiaina.Kuwa wazi. Ondoa mashaka.Kubali tofauti zenu. Mpende mwenza wako jinsi alivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom