Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kuna familia ambazo hawana kabisa desturi ya kujali wengine. Familia zingine zinakuwa na watu wasomi kabisa, lakini hawana hekima hata kidogo. Ukiolewa au kuoa mtu ambaye ametoka katika moja ya familia hizo lazima uteseke.

Atachagua kuangalia mpira badala ya kuwa na muda na familia yake au mke wake. Yaani hajali kabisa muda wake. Hajui matumizi ya muda wake. Anachokijua yeye ni kwenda katika kazi ya kuajiriwa na wanaume wengine tu. Lakini hana muda na Mungu, Mke au mume, Watoto, Na wengine.
 
Tabia za mtu huyu ni kuwaumiza wengine kila mara. Hata hawezi kujali kama anamuumiza mtu kwa kitendo anachokifanya. Imani ya dini yake inamwambia kuwa mwanamke ni mtu dhaifu. Ndio maana haoni sababu ya kumjali. Ni mtu wa kuhukumu kila wakati, Anaweza akawa anafokea watoto, anafokea mke, hata mbwa anamfokea na kutumia lugha chafu.

Ukijaribu kumweleza kuhusu tabia yake , atakuambia umechanganyikiwa , na wala hujui unachokiongea. Hana hata chembe ndani ya moyo wake wa kujali watu , Kwa mtindo huo kama hawezi kumjali binadamu , atawezaje kujali mnyama.
 
Mtu wa aina hii , ndani ya mahusiano ni ngumu. mtu mwenye moyo mgumu, mtu wa kuumiza moyo wa mtu mwingine, mtu asiyejali. Ni kitu gani kinawafanya watu hawa wawe na moyo huo?

Inaweza kuwa ni mazingira aliyokulia, Kwa wazazi ambao hawakuwahi kumuonyesha upendo wowote. HUenda ni kwa sababu ya kuwa na shida nyingi, Huenda ni kutokuelewa, Hajafundishwa, Amesahau au karuka maandiko ndio maana akili hio inamtesa.
 
Mtu huyu atakuwa anahisi kutopendwa, kukataliwa, Hakuwahi kujua jinsi ya kumjali mtu mwingine. Au inaweza kuwa ubongo wake umeshambuliwa na mitandao ya kijamii na shughuli nyingi za kidunia. Makundi ya kidini au ya kisiasa, ndio maana hana wazo la kujijali ni mtu wa kuhitaji watu wa kumpongeza hata kama hajafanya kitu kizuri.

Watu hawa wana mioyo migumu, hutaweza kuishi nao kwa urahisi, maana hata ukilia, ukapiga kelele , ukamtishia , kitu atakachokuambia ni hiki. Acha kunishambulia. Acha kunipa presha. Hata ukionyesha kumjali atakugeuzia kibao na kukufanya ushindwe kujali.
 
Nafikiri umewahi kusikia kuwa katika mahusiano kuna mtoaji na mpokeaji. Lakini kama wote mtakuwa watoaji mahusiano yatajengeka vizuri. Kuna wanaotoa sana, kuna wanaopokea sana, Lakini inapokuja suala la kujali, wengi hupenda kupewa muda wa kutosha. kuwepo pale kwa ajili ya mwenzake anapomuhitaji. Bila shaka huo nao ni utoaji. ni katika hisia na kimwili .

Utafanyaje endapo umeingia kwenye mahusiano na mtu ambaye hukuchunguza tabia zake kwa undani , ni mtu asiyejali, ni mtu asiyewajibika. mtu ambaye ataanza kukulaumu kuwa umekuwa tatizo maana hutaki kumuacha peke yake? Ni vizuri uanze kujijali mwenyewe. unaweza kuwa unasaidia na kuwajali watu wengi kuliko unavyojijali mwenyewe. Lakini unahitaji kujijali , Acha kutaka kumbadilisha mtu, hutaweza. kwa sababu hatabadilika kwa ajili ya kutaka kwako. Chui wamezaliwa kuwa chui huwezi kuwabadilisha. Unaweza ukadharau tabia yake, acha kujiumiza kutokana na matendo yake. Angalia kitu cha muhimu unachoweza kufanya.
 
Fikiria Kitu Utakachoweza.

1.Unaweza kuamua kuondoka kidogo.

Kuna vitu vingi ambavyo vinamfanya mtu kukaa, huenda ndio maana bado upo hapo, Lakini maumivu ya kukosa penzi, kukosa mtu wa kukujali, hakuna mtu wa kukuambia kila kitu kitakuwa sawa, hicho ni zaidi. ni maumivu , ni magonjwa. Piga magoti, Omba toba kuhusu wewe kuingia kwenye mahusiano ambayo yanakutesa. Mungu atafanya njia. Uchaguzi ni wako. huo ndio ukweli.
 
2. Kama utaamua Kukaa.

Msamehe. tambua kuwa huyo mtu ametokea mahali ambapo hapakuwepo na upendo, mahali ambapo hawajali wengine, na sehemu kubwa zaidi hakuwahi kujua jinsi ya kumuhurumia mtu. Jaribu kuona ni kitu gani kinampa huzuni, kitu gani kinakosekana kwake. Usikubali hali ya kubakwa, yaani kulazimishwa kitu bila ridhaa yako. kumbuka kuwa huyo mtu kuna vitu vingi vimekosekana kwenye maisha yake. Ona ndani yake kuwa kuna kitu kizuri kimejificha
 
3.Tafuta msaada mahali.

Kama wewe ni mtoaji na ni mtu unayewapenda watu na kuwajali, tafuta sehemu , kama kutembelea Yatima, Wajane, Wazee na wafungwa , kaonyeshe huo upendo , kujali kwako wengine. Au watu ambao wanakubali upendo wako. Fanya hicho kitu ni kizuri kwako. Hudhuria semina mbalimbali, watu wanaofundisha kitu unachokipenda kukifanya maishani mwako. Kumbatia moyo wako. Linda moyo wako, maana huko ndiko uzima wako unakotokea. hizi ndio sifa ambazo zitakusaidia kuishi mahali pagumu.
 
TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi asante kwa siku ya Jumanne Oktoba 2, 2018 Baba Tunaomba toba kwa makosa yote turehemu twakusihi.
Siku ya leo anza nasi na simamia ratiba zetu zote.Tunaomba ponya wagonjwa,majumbani na mahospitalini,fariji wafiwa wape tumaini yatima wajane na wagane ..tupiganie tuijue kweli yako.Bariki kazi ya mikono yetu inua uchumi wetu Mfalme wa amani.Endelea kuwalinda watoto na wajukuu zetu wasimamie katika masomo yao na maisha yao ya kila siku.Walinde wasafiri nchi kavu,majini na angani waende na kurudi salama.tujalie Amani na umoja katika nchi yetu epusha maafa,ajali za mwili na roho zishindwe katika jina la Yesu Kristo.Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen
JUMANNE NJEMA NA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi asante kwa siku ya Jumanne Oktoba 2, 2018 Baba Tunaomba toba kwa makosa yote turehemu twakusihi.
Siku ya leo anza nasi na simamia ratiba zetu zote.Tunaomba ponya wagonjwa,majumbani na mahospitalini,fariji wafiwa wape tumaini yatima wajane na wagane ..tupiganie tuijue kweli yako.Bariki kazi ya mikono yetu inua uchumi wetu Mfalme wa amani.Endelea kuwalinda watoto na wajukuu zetu wasimamie katika masomo yao na maisha yao ya kila siku.Walinde wasafiri nchi kavu,majini na angani waende na kurudi salama.tujalie Amani na umoja katika nchi yetu epusha maafa,ajali za mwili na roho zishindwe katika jina la Yesu Kristo.Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen
JUMANNE NJEMA NA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom