Makapuku Forum

Makapuku Forum

UKIJIZOEZA TABIA HIZI KUMI, NI NGUMU SANA KUZIACHA

1.Kung’ata kucha.

2.Kuliza viungo vya mwili (Cracking joint) kama vidole nk.

3.Kuvuta maneno “ummm” au “aaaaah” kila unapotaka kusema jambo. Mfano aaaah unajua… ummm sio kweli…

4.Kulamba kidole kabla ya kufanya kazi au kufungua ukurasa wa kitabu.
5.Kuchezea chezea nywele.(akina dada)

6.Kutawaliwa na mitandao ya kijamii.

7.Kuvuta wa sigara, Ugoro nk.

8.Kula ovyo, ofisini, nyumbani, njiani, Au wengine huamka usiku wa manane kula.

9.Umbea(gossiping). Kuna watu hawawezi kujizuia kutunza Siri.

10.Kujichua (Kupiga punyeto.)
 
MAMBO KUMI YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUACHA POMBE

1.Kama ni mlevi uliyebobea na unahisi huwezikuacha kwa siku moja, anza kwa kupunguza kiwango cha kunywa, yaani kama unakunywa bia tatu kwa siku, anza kunywa moja, baadae moja kwa siku mbili mpaka utakapozoea kuishi bila pombe.

2.Epuka kuweka kilevi au pombe nyumbani au sehemu ya kazi ili kuepuka majaribu.

3.Usipende kuruka mlo, kula chakula mara 3 mpaka nne (4) kwa siku ili kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu.
 
4.Ondoa dhamira potofu kwamba huwezi kuishi pasipo kunywa pombe. Kumbuka mwili wako umeumbwa kikamilifu kukabili hali zote za Maisha hivyo usihisi kuwa pombe ndio kichocheo chako kila unapotaka kufanya jambo Fulani.


5.Zingatia mlo kamili, na jifunze kula matunda kwa wingi.

6.Anza kufanya mazoezi na upange ratiba hii muda ambao ulikuwa ukitumia kunywa pombe.

7.Kumbuka mambo mabaya ambayo yalikutokea kutokana na pombe katika maisha yako. Hii itakusaidia kutothubutu tena kunywa pombe.

8.Ongeza unywaji wa maji jenga mazoea ya kunywa angalau glasi tano (5) za maji kwa siku.

9.Jenga mazingira ya kujizawadia kutokana na uamuzi wako mzuri wa kutokunywa pombe.

10.Washirikishe ndugu, jamaa na mrafiki wa karibu kuhusu uamuzi wako wa kuacha pombe na pia usijione mjinga kwa wale watakao kucheka.
 
USILIKATIE TAMAA JAMBO ULILOPIGANIA KWA MUDA MREFU FUATA HATUA HIZI KUMI KULIKAMILISHA.
1.Kaa Chini Na Uangalie Lengo Hasa La Wewe Kulianza Jambo Hilo. Zikumbuke Sababu Ulizojiwekea Mwanzoni Kwamba Ni Kwanini Unataka Lengo Lako Litimie. Itakufanya Ujione Mpya Na Uhisi Kwamba Ndio Kwanza Unalianza!

2. Kabla Hujakata Tama Jiulize Ni Kwa Nini Ulianza? Na Ni Kwanini Umelipigania Kwa Muda Wote Huo?

3.Andika Vitu Vyote Vizuri Utakavyovipata Ukishalimaliza Jambo Hilo, Vipitie Kila Mara Unapotaka Kufanya Jambo Hilo.
 
4.Elewa Kwamba, Vikwazo Na Changamoto Ni Muhimu Wakati Mwingine! Kikubwa Ni Kujipa Moyo, Kuboresha Mipango Yako Kulingana Na Muda Na Mabadiliko Ya Dunia, Na La Muhimu Zaidi Ni Kujifunza Kutokana Na Vikwazo Na Changamoto Ulizozipata!

5.Tafakari Ni Kipi Unakiweza Zaidi? Kitilie Mkazo Na Usijali Unakosea Kiasi Gani Bali Fikiria Umepiga Hatua Gani!

6.Punguza Vitu Kichwani Hasa Vile Usivyovihitaji Zaidi. Pia Punguza Idadi Ya Marafiki Wasiokuwa Na Msaada Kwako Ambao Wengi Wao Hawatakupa Msaada Wowote Zaidi Ya Kuangalia Unakosea Wapi.
 
7.Kuwa Na Muda Wa Kupumzika, Fanya Matembezi,Na Kulala Usingizi Wa Kutosha.

8.Tambua Kuwa Hauko Peke Yako! Hili Pengine Ndilo Zuri Kuliko Yote.. Hakuna Aliyefanikiwa Bila Kupitia Kipindi Fulani Kigumu Ambacho Pengine Kilimfanya Afikirie Kukata Tama! Never Give Up.

9.Kumbuka, Ukijaribu Njia Kumi Ukashindwa Kufika Unapokwenda, Ukaweza Mara Ya Kumi Na Moja, Hujapoteza Kitu Bali Umegundua Njia Kumi Zisizofanikisha! Hivyo Wakati Mwingine Hutapitia Njia Hizo.

10.Soma Vitabu Au Historia Ya Watu Waliofanikiwa Duniani Uone Wamepitia Magumu Mangapi! Pia Unaweza Kutafuta Mshauri (Mentor).
 
EPUKA KUTUMIA MANENO HAYA UNAPOMFARIJI MTU ALIYEFIWA

1.Usijali, Utapata mtoto mwingine (unasahau kuwa kila mtu ana nafasi yake duniani)

2.Jifunze kusahau bwana, Mbona umepita muda mrefu toka atutoke

3.Tulimpenda ila Mungu Kampenda zaidi (Hili neno halizoeleki jamani, yaani unahalalisha kuondoka kwake)

4.Shukuru aliishi Maisha Marefu, wengi wanakufa mapema

5. Najua inavyouma, ila usijali utamsahau tu
 
TUMIA MANENO HAYA

1.Pole sana, Nashindwa hata nitumie neno gani ili ujue nilivyoguswa na suala hili zito

2. Hatutomsahau Kamwe/ Pengo lake halitazibika

3.Mpe pole na Kumuahidi utakuwa nae kipindi chote hiki kigumu, akihitaji kitu utakuwepo kwa ajili yake

4.Mkumbatie bila kusema chochote

5.Kaa nae karibu tu na umpe mahitaji Muhimu, kumuomba ale nk.
 
Nitapandishwa kwa kubebwa binamu


...ha hahahaha, inabidi tulete kile chombo cha kunyanyua mizigo

tenor.gif
 
YAJUE HAYA KABLA YA KUAMUA KUJICHORA TATTOO (Share Na Wenzako)

1.Hazifutiki milele, swali linakuja je, miaka kadhaa ijayo utaendelea kukipenda kitu ambacho umekipenda leo nakukichora? Mfano, unadhani unakipenda Ulichokuwaukikipenda kufanya miaka 10 iliyopita? Kazi


2.Ili kuweza kuzoea tattoo unashauriwa kuchora tattoo ya muda mfupi kabla hujaamua kuchora tattoo ile itakayobaki milele.


3.Huwezi kuchangia damu katika baadhi ya mataifa. Ni vema kujua sheria za nchi yako kwanza kabla ya kufanya uamuzi huo.



4.Usikurupuke kuchora tattoo, kuwa na wazo la aina ya tattoo ya kitu unachokihitaji sio tu kwa kuwa uliiona kwa mtu Fulani.
5.Huharibu muonekano wako katika jamii kwani kuna badhi ya sehemu unaweza usishirikishwe kwa kuonekana hufai katika jamii ile (hasa jamii za Kifrika)
 
6.Kuchora tattoo ni gharama, kabla ya kujichora tattoo lazima ujipange kwanza ili upate kitu unacho kihitaji kwa gharama sahihi na kuepuka tattoo ya ubora wa chini na kutokuwa na muonekano unaoutaka.

7.Ni hatari labda tu uchorwe na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuchora kwani kuna miili ina ‘aleji’ na wino utumikao kuchora tattoo. Yaani eneo ulilochora mchoro wa tattoo, linaweza kudhurika kwa namna mbalimbali.

8.Tattoo itakufanya ukose baadhi ya kazi kwani kuna baadhi ya sehemu tattoo huonekana kama ni ukosefu wa nidhamu. Mfano Jeshini, baadhi ya Mashirika ya Kidini nk!

9.Usidhani unajua sana undani kuhusu tattoo kwa kuwa tu uliona watu kwenye tv wakiwa na tattoo na wewe ukatamani kuwa nayo, Hakikisha una elimu ya kutosha kuhusu tattoo unayotaka kuichora ndipo ufanye maamuzi.


10.Kuwa makini katika uchaguzi wa mahali sahihi katika mwili wako ambako unahitaji uchore tattoo hiyo.
 
UKIJIZOEZA TABIA HIZI KUMI, NI NGUMU SANA KUZIACHA

1.Kung’ata kucha.

2.Kuliza viungo vya mwili (Cracking joint) kama vidole nk.

3.Kuvuta maneno “ummm” au “aaaaah” kila unapotaka kusema jambo. Mfano aaaah unajua… ummm sio kweli…

4.Kulamba kidole kabla ya kufanya kazi au kufungua ukurasa wa kitabu.
5.Kuchezea chezea nywele.(akina dada)

6.Kutawaliwa na mitandao ya kijamii.

7.Kuvuta wa sigara, Ugoro nk.

8.Kula ovyo, ofisini, nyumbani, njiani, Au wengine huamka usiku wa manane kula.

9.Umbea(gossiping). Kuna watu hawawezi kujizuia kutunza Siri.

10.Kujichua (Kupiga punyeto.)
No 1 inanihusu kabisa kucha zangu za mkono wa kulia kila siku zinabaki vibubutu
 
Jamani napenda beer mm acha niendelee kujinywea tu waachaji mnaitwa hapa
MAMBO KUMI YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUACHA POMBE

1.Kama ni mlevi uliyebobea na unahisi huwezikuacha kwa siku moja, anza kwa kupunguza kiwango cha kunywa, yaani kama unakunywa bia tatu kwa siku, anza kunywa moja, baadae moja kwa siku mbili mpaka utakapozoea kuishi bila pombe.

2.Epuka kuweka kilevi au pombe nyumbani au sehemu ya kazi ili kuepuka majaribu.

3.Usipende kuruka mlo, kula chakula mara 3 mpaka nne (4) kwa siku ili kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom