Makapuku Forum

Makapuku Forum

3. Akiwa ndani ya maji anaweza kutumia dakika tano bila kuibuka ambapo hubana pumzi ndani ya maji anapokwepa hatari ya kushambuliwa na adui yake.

4. Huyu Ngekewa ndio mnyama anayependwa na viumbe vingi vya porini na majumbani.
Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.

5. Kwenye kamusi ya lugha ya kiswahili neno Ngekewa mbali na kumzungumza huyu mnyama pia limetafsiliwa kama bahati au yenye bahati na ndio maana hata mtaani mtu mwenye bahati huambiwa ana ngekewa.
Asili ya maana ya neno ngekewa ipo katika kupendwa kwa huyu mnyama na viumbe mbali mbali hata vile vya hatari.
 
Habari wana JF
Habari Makapuku wenzangu
Matumaini yangu wote mko poa kabisa.

Uzi huu ni kwaajili ya makapuku wote. Lengo ni kujadili changamoto zinazotukabili, pia Kupeana support katika mambo yetu hapa JF. Tupeane mbinu za kukabiliana na mambo yote humu.

Makapuku natumaini nyote tutashirikiana katika jambo hapa JF. Bila kumsahau founder wa makapuku Bitoz shukrani kwake

Karibu sana makapuku katika mjadala. Wengine nitawaongeza hapo baadae.

Karibu sana

Bitoz
JF Makapuku Founder

Jimena
JF Makapuku assistant Founder

Th Name JF Makapuku assistant Founder
Warembo mpo
 
Asante Numbisa kwa makala nzuri, nazisoma zote kwa ufasaha timamu kabisa.

Tumosa nipo sana, nilikuwa nalinda wikend kimyakimya. Transcend hiyo pensi kwenye picha nadhani sio mimi, sababu mimi huwa navaa pensi ndiyo ila navaa na Tshirt maana nina kakitambi kalikogoma kutoka kwa mazoezi so nakarutubisha na bia na mchemsho.

Anko Lyon Lee pamoja sana, asante kwa salamu zako nimezipata sawia bila shida na unasalimiwa sana.

Shunie, mtu chake , omarion5 , SHIMBA YA BUYENZE , makaveli10 , dingimtoto , Clkey , ABJ , Da'Vinci , sweetlee , Nyagei , shululu , Wick , Slim5 , The Book na wewe kapuku unayenisoma hapa, ujue nini, ninyi ni wadau wa ukweli na mara zote ni fahari kusoma chochote mnachoshare hapa jukwaani, sharing is caring na hasa life knowledge na siasamaisha kwa ujumla.

Okay, tuyaache haya, Kuna Jipya?
 
TUOMBE:Baba yetu na Mungu wetu asante kwa ajili ya siku ya leo Jumanne tarehe 25 Septemba 2018 Tunaomba toba kwa kika tulichoenda kinyume na mapenzi yako uturehemu twakusihi.Tusaidie tuweze kutambua namna unavyo tupenda na kutupigania katika kila jambo.Tunakabidhi kazi zetu,watoto wetu,wajukuu wetu,familia zetu,rafiki zetu mikononi mwako endelea kuonekana kwetu Mfalme wa Amani.Tunaomba ponya wagonjwa wote,ponya majeraha yote watie nguvu wanaouguza na waongeze kila panapopungua wasipungukiwe katika kutoa huduma,wafariji wafiwa yatima wajane na wagane endelea kuwapa tumaini.
Baba wasafirishe salama wasafiri wote waende na kurudi salama Angani,nchi kavu,majini damu Takatifu ya Yesu Kristo iwafunike.Bariki kazi zamikono yetu zizae matunda mema na tuendelee kukutolea kwa moyo wa upendo na furaha.
Asante Baba maana utaendelea kutuongoza na kutupigania tunaomba Roho Mtakatifu awe nasi sote na tukinge na ajali zote za mwili na roho Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen

JUMANNE NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
Amen! Ubarikiwe mama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom