Farasi ni mnyama anayefugwa na hutumia majani kama chakula chake kikuu, mbali na majani pia ni mpenzi sana wa matunda vitu kama karoti, apple anatumiaga pia, ukiondoa matunda hayo viazi mviringo pia hupendelea sana, Ni mnyama anayebeba mimba kwa miezi 11 mpaka 12 kabla ya kuzaa, mtoto hutanguliza miguu ya mbele kisha kichwa hufuata, Farasi ni miongoni mwa wanyama ambao huhitaji msaada sana pindi wanapozaa, hupata maumivu makali huku akitetema tumbo kwa maumivu makali huku akitoa kilio, hata hivyo muda mfupi tuu baada ya kuzaa ndama wake huanza kuruka ruka kwa fujo akimshukuru Mungu kwa kumleta katika ulimwengu wa tofauti na aliokuwapo awali.
Farasi ni mnyama namba moja kwa faida kuliko mnyama yoyote anayefugwa, mosi nyama yake ni chakula, pili maziwa yake pia chakula, ngozi yake ni dili viwandani, ukiondoa hayo farasi ni usafiri au sio, bado ni mnyama askari kama ilivyo mbwa, panya nk, farasi hutumiwa katika kutawanya maandamano akiinua miguu yake ya mbele umati wote kelele, lakini kama hayo yote hayatoshi farasi ni mnyama anayetumiwa vitani sana nadhani ushahidi upo hata katika baadhi ya filamu.