Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farasi ni mnyama mwenye nidhamu sana ukiwa mgongoni kwake ukaanguka hawezi kuendelea na safari mpaka utapozinduka kama ulizimia, lakini pia ni mnyama mwenye upendo hawezi kukupeleka sehemu yenye hatari ukiona anagoma kusonga mbele tambua kama hakuna nyoka basi pana hatari ambayo wewe huioni, Macho yake ni makubwa sana na yana uwezo mzuri wa kunasa matukio vyema mbele na nyuma kwa umakini sana.
Mbali na uwezo huo wa kuona vyema lakini pia farasi yupo vizuri katika kunusa, hamuwezi kukamatwa kizembe na wanyama wakali hasa wale wanaovizia kwa kujificha ukiwa na farasi, unapomfunga ukiona anapiga kelele na kuinua inua miguu kama anapasha ili atimue mbio, haraka sana mtii na mtoke eneo hilo, vinginevyo ataka kamba na kuondoka mwenyewe kisha umalizane na hatari hiyo mwenyewe kama ni simba,chui au mbwa mwitu.
Farasi hula kilo tano mpaka 12 za majani kwa siku, hapa hutegemea sana na umri pamoja na uzito wake, mnyama anayekula nyama anayeweza kumkamata kwa kumfukuza ni duma na mbwa mitu wa kizungu (wolf) pekee, hawa akina simba, sijui fisi nyama yake wataishia kuisikia tuu, mbali na uwezo huo wa kuchanja mbuga farasi pia hupatwa na hisia pamoja na maumivu ukimtendea ubaya usichangae akidondosha machozi na akikushusha kuanzia juu mpaka chini, hapo ujue amekudharau tuu.
Wanyama hawa huuzwa ghari sana, farasi mmoja kwa hapa kwetu hufikia million 5 na ushee, na bei ya farasi hupangwa kutokana na rangi, usitegemee kabisa ukafikiri mkubwa ndio atakuwa bei, rangi ambazo ni adimu ndio huwa ghari zaidi hivyo basi kwa ukijua nyeupe na nyeusi si rangi ghari kumnunua farasi, labda ziwe na mngaro wa kipekee.
 
Farasi ni mnyama ambaye anavutia sana kwa wapendanao, inasemekana wapenzi ambao humtumia farasi kama usafiri huwa ngumu sana kutengana, kwani mnapokosana farasi nao hukosa raha, nchi zingine watu hutumia farasi kuendea kazini, maharusi hutumia farasi kama usafiri wao pindi wanapokwenda kufunga ndoa na mambo hufaana sana, hivyo hata wewe unayesoma kama una harusi karibuni badala ya kukodi gari tumia farasi kujitofautisha na wageni ndio mambo yanavyokwenda digital, tena hakikisha katika kadi za michango mmepiga picha juu ya farasi, utashangaa michango itavyo miminika.
 
****SIFA ZAO ZA KIPEKEE ****
1. Mbali ya kuwatizama jinsia zao unaweza kumjua jike na dume kwa kuhesabu meno, dume huwa na meno manne zaidi ya jike. (40 kwa 36)
2. Akikubeba anapokimbia sehemu za kupita hupiga hesabu mwili wake tuu, hivyo ni jukumu lako kujirinda.
3. Kama walivyo mbwa humtii boss wake tuu, hivyo ukimpiga kama hakufahamu naye atakupiga.
4. Si wapenzi wa ngono kabisa farasi, ila ni wapenzi wa upendo.
5. Dume la farasi huweza kusisimuliwa kimahaba na mwanamke, ukimpitisha kavaa chupi tuu na akalishika shika ubavuni hudondosha mate na ndio mbinu ambayo hutumiwa kulishawishi likampande jike wake.
6. Harufu ya uke wa farasi jike pia humpa mshawasha dume kumpanda.
7. Farasi kwa taarifa yako hutomasana kabla ya kuanza kupendana.
8. Ana uwezo mzuri wa kunusa na kusikia kuliko binadamu.
9. Jicho lake ni kubwa kuliko wanyama wote wa ardhini.
 
10. Dume la farasi huweza kumpanda punda na pundamilia na akazaliwa mtoto chotara.
11. Farasi hawapendi kabisa punda wakikutana wa sehemu tofauti huweza sababisha kifo cha punda kutokana na kipigo.
13. Farasi ni miongoni mwa wanyama wenye kumbukumbu.
14. Ukiwatunza vyema huishi miaka 28 mpaka 32.
15. Ni mnyama ambaye hutumika kama chanzo cha mapato, kukodishwa, kulimia nk.
16. Wakati wanawake wanasuka kichwani, farasi husukwa mkiani na hii ni kwakuwa vinyweleo vyake vimechanua kwa kiasi kikubwa.
Farasi ni mnyama wa fahari sana ni vyema serikali kwenye hifadhi kama kitulo ingeongeza nguvu katika ufugaji,
 
Tembo ni mnyama aishie mbugani, ndio mnyama pekee ambaye ni mkubwa kuliko wanyama wote katika uso wa dunia, mnyama huyu ni mrefu pia mnene, ana wastani wa kilo zaidi ya elfu saba, kwa lugha nyepesi namaanisha tani saba, mbali na uzito huo lakini ana urefu wa futi kumi na tatu ni kimo kikubwa sana, miguu yake ya mbele ni mirefu kidogo kwa miguu ya nyuma, mnyama huyu hula majani, mizizi, matunda nk, chakula chake hutokana na mimea tuu.
Kichwani kwake ana viungo vyote alivyo mwanadamu, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya viuongo vyake huwa havionekani kwa urahisi, mfano watu wengi huwa hawajui mdomo wa tembo upo eneo gani ! na wanaoweza kukuonesha mdomo wanaweza shindwa kabisa kuonesha pua ya tembo ilipo, masikio yake ni makubwa sana ukiyafanya sahani unaweza kuweka msosi hata wa watu kumi, kama wakila pamoja.
Tembo ndio mnyama pia ambaye ana kichwa kikubwa, ambapo ndani ya kichwa chake kuna sehemu kubwa iliyobeba ubongo wake, Tembo wa Africa ndio tembo wakubwa na wenye mvuto sana, hubeba mimba kwa miezi 22 yaani mwaka mmoja na miezi kumi, baada ya hapo huzaa mtoto mmoja au wawili, watoto wa tembo huzaliwa wakiwa na kilo zaidi ya 100.
 
Katika mbuga za wanyama tembo ndio kiumbe pekee ambaye hawindwi na mnyama yoyote, isipokuwa watoto wake tuu, lakini kwa bahati mbaya adui yake mkubwa ni jangiri yaani binadamu, na kinachomponza ni meno yake ambayo mwayaita pembe.
Upana wa ngozi yake ni zaidi ya nchi moja, na ndio maana hata wawindaji haramu hutumia silaha nzito kuwawinda, na hata anapokufa mzoga wake huwapa tabu sana wanyawa wanaokula nyama kumtafuna.
Tembo ni mnyama anayeamini sana katika amani, lakini ni mtata sana anapohisi kuwa unataka kumdhuru hata kama yeye ndiye aliyekukosea, wanyama wanyonge huamini sana kukaa naye jilani kwakuwa ukiwa naye ni ngumu kuwindwa.
Tembo ni miongoni wa wanyama ambao wanaishi kwa muda mrefu sana, hata binadamu anaweza akaachwa huishi miaka 50 hadi 80.
 
***********************SIFA ZAKE ZA KIPEKEE******************
Ni mpenzi sana wa kula hutumia chakula zaidi ya kilo 130.
Tembo ni mnyama mwenye akili sana, baadhi ya mambo hufanya kwa ustadi kama binadamu kama yafuatayo.
Wanapokutana wana namna yao ya kusalimiana, kwa kuinua mkonge wao.
Ana kumbukumbu vibaya sana anaweza kukumbuka tukio hata la mwaka mmoja uliopita, kwahiyo usijemfanyia ubaya sehemu ukafikiri atakusahau, wanyama ambao hufanya matukio ya kukamata mtoto wake, huwa anawasave kila wanapokutana ni bifu tuu.
Ni msafi anapendelea kuoga sana kila anapokutana na maji, hapendi kunuka harufu ambayo hunuka viumbe wa jamii yake kama nyati,twiga nk.
Wana lugha ya mawasiliano kama bianadamu ambao hufanya mawasiliano kwa kugusana, ishara pamoja na kuunguruma.
 
Wanapokuta tembo mwenzao kafa, hukusanyana na kufanya msiba ambapo majike hutoa machozi kabisa, na husimama eneo hilo kwa masaa kadhaa kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuufunika mwili wa mwenzao huyo kwa miti na majani.
Tembo ndio mnyama pekee ambaye anaweza akafa akiwa amesimama na watu mkajua ni mzima tuu.
Mletee mzaha wowote yeye lakini usimchezee mwanaye, ana mapenzi ya kweli.
Anapovuka sehemu ambayo ina barabara ambayo hupita viumbe wengine, hutangulia umbali kiasi kisha huenda kukaa katikati ya barabara mpaka hapo mwanaye atakapovuka, kwahiyo nyie na magari yenu ni jukumu lenu kusubili mtoto wake avuke wakati mkiwa mmesimamisha gari zenu, ole wako ukaidi au upige honi au ulete jeuri yoyote.
 
Huweza kuelewa lugha ya mwanadamu kwa kusoma ishara ya mwili wake pindi aongeapo, mfano akivamia mashamba ya wanadamu wanapotokea na kuanza kupiga kelele hutambua kuwa wanatangaza ubabe hivyo hufanya balaa na balaa lake huisha akiamini amekumaliza kabisa.
Akianza kukimbia kadri anavyokwenda mbele ndio huongeza spidi.
Hawezi kukimbia umbali mrefu sana.
Hutumia vichuguu vikubwa katika kujikuna sehemu zinazowasha, kwakuwa vichuguu hivyo hugusa sehemu kubwa ya mwili, lakini inapokosekana mti ndio huwa mbadala japokuwa miti huchubua ngozi zao.
Anatumia masaa manne tuu kulala, hupendelea sana kusimama, maana akilala kuamka huwa shughuli.
Anapoamka hujichochea kwanza, hawezi kuamka moja kwa moja ni lazima ajitingishe kwanza na hujitingisha zaidi ya mara tano.
 
Anapokwenda mtoni mambo wakikosea step kumkamata mtoto wake, basi ujue eneo hilo wote watapote, na maji yatabadilika rangi maana eneo hilo atalitifua na mpaka mtoto aonekane.
Wanapotembea watoto hupewa ulinzi maalumu kutokana na mazingira, wakati wote mama hutangulia mbele na dume huangalia upande wa kukaa kutokana na sehemu wanayopita ina wanyama wa aina gani wanaowinda.
Bado hajatokea mnyama mwenye uwezo wa kumdondosha tembo, tena sio mzee, hata kijana tuu, samba na nguvu zake zote hata wakiwa sita hawawezi kumpeleka chini.
Mimea anayopenda inayolimwa na binadamu ni pamoja na ndizi.
 
UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI ***************
Bahati nzuri ni kwamba tembo sio mnyama mkorofi, ila unavyokuja ndivyo anavyokupokea, na suala la kukuamlia ni vile atakavyo kusoma yeye, hivyo kukuumiza au kutokuumiza ni vile atakavyokuwa ameamua, kwa hiyo kivyovyo ni jukumu lako kuchukua tahadhari, jamaa hawa hawatabiriki.
 
Makapuku itaingia kila chaka na italeta kile ambacho kinatokea kwenye jamii, tutakuwa tofauti na wao wanaoomba ushauri kwa vitu ambavyo havina maana.. Wale wanaoamini ubora wao wakati bado hawapo kwenye viwango.. Kila Jukwaa litatikisika na kukubali kuwa sisi ni makapuku ambao tunawasha kama U.P.U.P.U
KWELI MKUU NDIYO MAANA LEO NIMEKUJA KUWACHEKI


MADOGO NILIOWAACHA PRE-FORM 1 WAKO CHUO
 
Huweza kuelewa lugha ya mwanadamu kwa kusoma ishara ya mwili wake pindi aongeapo, mfano akivamia mashamba ya wanadamu wanapotokea na kuanza kupiga kelele hutambua kuwa wanatangaza ubabe hivyo hufanya balaa na balaa lake huisha akiamini amekumaliza kabisa.
Akianza kukimbia kadri anavyokwenda mbele ndio huongeza spidi.
Hawezi kukimbia umbali mrefu sana.
Hutumia vichuguu vikubwa katika kujikuna sehemu zinazowasha, kwakuwa vichuguu hivyo hugusa sehemu kubwa ya mwili, lakini inapokosekana mti ndio huwa mbadala japokuwa miti huchubua ngozi zao.
Anatumia masaa manne tuu kulala, hupendelea sana kusimama, maana akilala kuamka huwa shughuli.
Anapoamka hujichochea kwanza, hawezi kuamka moja kwa moja ni lazima ajitingishe kwanza na hujitingisha zaidi ya mara tano.
Mambo yako numbisa

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Bila shaka umewahi kusikia mtu akisema, wacha nicheke niongoze siku za kuishi. Kama umewahi kusikia nataka nikuongezee kitu ya kwamba wataalam wa saikolojia wanasema kuwa kucheka au kufurahi ni moja ya tiba kwa afya ambayo huifanya miili yetu kubaki na afya bora zaidi.

Naomba leo nikwambie haya mambo kadhaa ambayo utayapata endapo utakuwa ni mtu wa kucheka na kufurahi.

1. Kwanza kabisa kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo na kumfanya mhusika kuwa vizuri kiakili.
 
2. Husaidia kuimarisha afya ya mapafu
Unapocheka husaidia mapafu yako kutanuka na kuingiza ndani hewa ya safi yaani oxygen. Hivyo unapocheka zaidi tambua kuwa unasaidia kiwango cha hewa kuingia cha kutosha ndani ya mwili na kusaidia damu kusambaa vyema mwilini.

3. Husaidia kuboresha utendaji kazi wa moyo
Kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kukuweka mbali dhidi ya shinikizo la damu la kushuka, kwa sababu husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na pia kusaidia mishipa ya damu kutenda kazi vizuri.

4.Huboresha kinga za mwili
Kucheka ni muhimu kwani husaidia kuongeza homoni za hisia ndani ya mwili. Kutokana na mabadiliko hayo huenda.

Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo mtu akiwa nazo zinamsaidia pia hata kuishi miaka mingi.
 
KAMA UMEWAHI KUSIKIA NENO "NGEKEWA" BASI LIMETOKANA NA MNYAMA HUYU

1.Mnyama anayefahamika kwa jina la kigeni Capybara ambapo kwa kiswahili huitwa Ngekewa ni mnyama mwenye ukubwa wa sentimita 134 na uzito unaokadiliwa kuwa kilo 66 anapokuwa mkubwa na mnyama huyu asili yake ni nchi ya America ya kusini.

2. Ni mnyama ambaye anapenda kukaa karibu na maji na anapojisi hatari hulazimika kukimbilia ndani ya maji na ana ujuzi mkubwa wa kuogelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom