Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kwenye suala la uwindaji simba hupenda kuwinda nyati kwakuwa nyati hana spidi sana na ni kitoeo kikubwa na nyati mmoja hukalishwa chini na simba 4,5...sasa simba huyu anayeanza kubalehe ataweza kumkalisha nyati ? La hasha

Simba hawindi swala ni aghalabu sana simba kuwinda swala sababu swala ana mbio sana na simba hana mbio za kumkimbiza swala huwa inatokea simba anavizia kwa kunyata mpaka ahakikishe amefika mita 3 au 2 ndio amstukize swala..chakula kingine cha simba ni nyumbu na pundamilia

Kwakuwa simba huyu alikuwa anashiriki na mama ,shangazi ,Dada zake kwenye kuwinda basi instincts za kuwinda anazijua ila simba huwa wanapenda kuwinda kwa ushirikiano na yeye yupo pekee yake hapa ndio shida ilipo.

Kama simba dume walizaliwa 2 basi hufukuzwa pamoja na simba ndugu huwa wanapendana sana hivyo inakuwa bahati simba hawa watashirikiana kwa kila kitu kwenye kuwinda ,kupigana na adui nk na kama yupo pekee yake basi ataishi maisha yake kwa uangalifu na ugumu kiasi labda itokee akutane na simba dume mwingine aliyefukuzwa na mzee wake na wataunda timu moja na sababu kubwa ni kwaajili ya kuwinda ,ushirikiano wao utakuwa umekutanishwa na lengo moja kuwinda na watakaa pamoja kwa muda kidogo na baada ya muda kila mmoja atachukua hamsini zake.

Maisha yataenda hivyo mpaka atakapofikisha miaka 5 hapo atakuwa shababi haswa na atakuwa na misuli mikubwa na nywele nyingi hata ukimuona lazima utetemeke ,akikutana na koo ya fisi wapatao 15 lazima fisi hao watimue mbio wote ,mngurumo wake husikika kwa umbali wa mile kadhaa.

Kwa umri huu aliofikisha simba huyu anakuwa kivuruge chochote humwambii yupo kwenye peak yake ,akimuona simba jike pekee yake ataenda kumtongoza na simba jike huyo hatomkubalia kirahisi kwanza atampima ubavu je yupo fiti ,je ataweza kumlinda yeye na watoto ,akisha thibitisha hilo ndio ataruhusu kuwa nae na hapo watafanya mapenzi sana hata mara 35 kwa siku .

Simba huyu asipopata jike maana ni aghalabu sana kumuona simba jike awe pekee yake basi atatakiwa aingie kwenye eneo linalomilikiwa na simba na hapo watapigana na akishinda atalimiliki hilo eneo na jike waliokuwepo na kama jike atakuwa na watoto basi atawaua wale watoto wake ili aweke damu yake na genes zake na endapo akipigwa basi atapigika kiukweli na kuumizwa vibaya na kutimuliwa.

Endapo akishinda pambano simba anayemiliki eneo ataondoka na simba huyu atajitawalia eneo hilo na ataweka alama ili simba yeyote mvamizi akitokea apate onyo hii sehemu ni hatari hupaswi kuwepo.,endapo wakizaa watoto na jike basi wataitwa pride na simba jike huwa wanaenda kuwinda huku dume akiondoka zake kwenda kutizama mipaka na hutembea mile kuhakikisha hakuna mvamizi yeyote anaingia kwenye ardhi yake kisha ana nguruma na mngurumo huo husikika kwa umbali wa mile kadhaa kama kutoa tahadhari kwa madume wengine kuwa eneo fulani kuna mfalme hivyo haipaswi kuingia na kama kuna dume karibu haswa wadogo au wasio tayari kupambana basi huondoka zao ,simba dume huyu akishafanya patrol ya eneo lake huweka alama ili hata dume yeyote akikatiza kwa bahati mbaya apate tahadhari na onyo hilo kisha hurudi kwa familia yake na jike wakishawinda wa kwanza kula ni dume na ukiwa mbishi utakutana na kisago sababu huyu dume hufanya kazi kubwa hivyo lazima ale ashibe

Simba dume maisha yake yote hutegemea nguvu ,ndio maana kila siku anakagua eneo lake na kutoa tahadhari kwa simba wengine lakini lazima akumbane na misukosuko wapo simba dume ni mabachelor nao wanataka familia na msosi wa bure na njia rahisi ni kuvamia eneo la pride na kupigana na dume mpaka kieleweke ,simba hutofautiana wapo wanaotembea kindugu wawili wawili haswa waliozaliwa tumbo moja hawa wanapovamia eneo linalomilikiwa na simba mmoja ni rahisi wao kushinda na eneo linalomilikiwa na simba dume 2 ni vigumu kupokwa na wavamizi.

Siku zote mapambano ya simba dume kugombea na kulinda eneo huleta maafa makubwa;

1.simba wanapopigana hukimbilia kung'ata na kunyofoa mapumbu na simba aliyenyofolewa mapumbu hushindwa tena kuzalisha na kusambaza damu yake ,

2.simba anayeshindwa huwa anaumizwa vibaya sana mithili ya mtu aliyegongwa na fuso na wengi hufa sababu simba ni mbishi,hakati tamaa kwenye kupigana

3.endapo simba mvamizi akishinda pambano basi vitoto vyote huuliwa labda mama simba akiona mumewe kazidiwa hukimbia na watoto na kuwaacha majike wengine ambao watatawaliwa na simba mpya huyo

Haya ndio maisha ya simba dume hakuitwa mfalme wa nyika kwa bahati mbaya ,simba humiliki mile kadhaa za eneo wanyama wote nyati,nyumbu,pundamilia,twiga na hata tembo ni wa kwake sasa ole wake simba mwingine au fisi ajipendekeze kwenda kuwinda eneo lake atauliwa kama sio kujeruhiwa

Simba maisha yake mengi hutawaliwa na hofu ya kupinduliwa ndio maana mwanaye wa kiume akifikisha miaka 2 humfukuza ,jihadhari sana kuingia kwenye territory ya simba hautobaki salama bora ukutane na jike kuliko dume utararuriwa tu.
 
MFAHAMU NGAMIA

Ngamia ni mnyama anayekula majani tuu, ni mrefu na mwenye ufanano na twiga kwa kiasi fulani, tofauti yao ni kwamba wakati twiga akiwa mrefu zaidi, ngamia ni mnene zaidi, pia twiga makazi yake ni mbugani lakini ngamia ni mnyama anayefugwa, kwa uzito hawaachani sana pia, mnyama huyu hubeba mimba kati ya miezi 12 mpaka 14 na huzaa mtoto mmoja au pacha kwa bahati sana, na mtoto huwa na kilo zipatazo 50 huku mgongoni akiwa hana Nundu kabisa.

Kwa Kimombo Ngamia anaitwa Camel, lakini neno hilo asili yake ni Latin likibeba maana ya respectively, ukiondoa jina hilo pia anafahamika kwa jina la Meli ya jangwani, ni mnyama mwenye faida lukuki sana, kwanza maziwa yake hutumiwa na binadamu, mnyama yake pia, wakati vinyweleo vyake na ngozi hutumika kuzalisha bidhaa kadha wa kadha, lakini kama haitoshi Ngamia pia ni usafiri, kwa ambao wamefika Sudan au Misri jambo hili wala halitawashangaza.

Maisha yao ni kati ya miaka 40 mpaka 50, kimsingi ngamia wapo wa aina Mbili, mwenye nundu moja ndio maarufu sana hapa Africa, wakati aina ya pili ambao hubeba nundu mbili na vinyweleo vingi wakipatikana huko Asia, waone na miili yao vile vile na mwendo wao wa taratibu lakini ukitaka kumuharakisha yawezekana pia, akishika njia haswaa hukimbia km 40 na zaidi kwa saa moja tuu.

Kwa urefu huwa na futi 6 mpaka 7, na uzito wao ukicheza kati ya kg 300 mpaka 1000 endapo matunzo mazuri atapewa, mtoto wa ngamia hupevuka anapotimiza miaka 7, Ngamia jike ni kiumbe ambaye kwa mapozi na malingo amebobea, humzungusha sana dume pindi anapotaka wastarehe, mpaka jike akubali na kujilaza chini dume hutumia mbinu nyingi sana, ikiwa ni pamoja na kumlamba, kumchezea shingo, kumkuna na anapokuwa mkaidi dume huchukia na kumuuma kabisa, hapo jike ndio kidogo atamfikiria fikiria kuwa jamaaa alipofikia sasa hakuna namna ! Na apewe tuu huduma !

Na kwa usumbufu huo jike akipitisha tuu jambo hilo, Dume hufidia akiingia hatoki mpaka afanye ejaculation zaidi ya mara tatu, ndipo aanze kutafuta pumzi ya round nyingine, hapo ndio atatoka huku jike wake akimkwepeshea macho kwa aibu ya usumbufu alioufanya !

Ukiondoa hayo Ngamia ni mstahimilivu sana katika mazingira ya ukame, anaweza akadumu kwa muda mrefu sana pasina ya kula wala kunywa, Na siri ya kuwa hivyo ni ile Nundu aliyonayo pale juu, huweza kubeba kiasi kingi cha wanga kinachomsaidia kujimudu anapokuwa katika mazingira kama hayo, hunywa maji zaidi ya lita 110 na si mwepesi kupata kiu .

Sifa zake za upekee.

1. Ni mnyama msikivu, mtulivu na mwenye nidhamu.

2. Ni mnyama mtii.
Huko uarabuni nasikia akisomea dua tuu analala tayari kwa kuchinjwa.

3.ukiwatumia kama usafiri we muharakishe jike tuu, dume atafanya haraka huwa hapendi kushindwa kwa jike.

4.madume huwa wakubwa na warefu kidogo kwa majike.

5. Ni mnyama mwenye heshima yake Uarabuni, kama ilivyo twiga Tanzania au Kangaroo kwa Australia.

6.hupendelea kuishi kifamilia

7. Ukiwa naye jangwani na kukiwa na uhaba wa maji anaweza kukuongoza mpaka sehemu mtayopata maji.

8. Ngamia jike hutoa maziwa kuanzia Lita 15 na zaidi.

8. Ni mnyama mpenda amani na rafiki sana kwa binadamu.

Wakati hapa Tanzania wajasiriamali wakihamasishwa kufuga kuku kwa ajili ya chakula na biashara, huko Sudan mwaka Jana walikuwa wanafanya campaign ya kufuga ngamia kwa sababu kama za sisi kufuga kuku.

Hata hivyo imefahamika kwamba wanyama ambao huwa hawapatikani katika jamii fulani, kitoweo chao ukipeleka katika jamii hiyo watu wake hupata tabu sana katika matumizi, sasa nakuacha na swali je waweza kunywa maziwa ya ngamia na kuila nyama yake !
Ameeeeiijingiiii
 
Sababu 6 za kutafakati katika kuendelea kusonga mbele na kutokata tamaa.
Usikate tamaa; kabla ya kukata tamaa kwanza jiulize ni kwanini ukate tamaa. Unapokata tamaa hutaendelea kujaribu bahati yako na jitihada zote ambazo umefikia zifikirie unaenda kuziacha na kukubali kushindwa.
Hata kwenda mbele taratibu ni hatua. Unaweza kukata tamaa kutokana na kuwa unahisi mwendo wako ni taratibu na ungetamani ungeenda mbele kwa haraka zaidi. Kumbuka kuwa hata hatua za taratibu ni mwendo, cha msingi haujasimama sehemu moja na unaendelea kusonga mbele.
Kumbuka kuwa maisha sio mashindano. Usikubali kujilinganisha na mwendo wa wengine katika maisha na kutimiza malengo. Kila mwanadamu ana hatma yake na wewe weka umakini kwenye nia yako na jitazame mwenyewe, epuka kujilinganisha na watu wengine.
Kuwa na mtazamo chanya (Positive thinking). Kabla ya kukata tamaa tazama machache uliyoweza kuyafanikisha katika mipango yako na weka mtazamo wa kushukuru kwa ulipofikia na kwa kujipongeza hata kwa madogo ambayo umeyafikia. Jifunze kushukuru hata mambo madogo ambayo umeyafikia na usijione hujafanya chochote mpaka ulipofikia.
Jifunze kupumzika na kuruhusu muda kufanya kazi yake. Sio kila saa lazima ujipe mawazo na wasiwasi, kuna muda unatakiwa kupumzika na kutuliza akili kidogo kabla hujakata tamaa au kuhisi kuwa hausogei mbele katika malengo yako. Sio kila muda unatakiwa uwaze sana, ukiona jambo unaliwaza sana jipe hata muda mfupi wa kupumzika kutafakari kisha utarudi kuendelea kutafuta hatma yake kabla ya kukata tamaa.
Jifunze kukua na changamoto. Unapokata tamaa inamaanisha umekubali changamoto zikushinde na hutoendelea mbele. Kwanini ukubali changamoto zikushinde? Changamoto zipo kwa ajili ya kutukuza kifikra na kujifunza mengi katika maisha yetu. Usitazame changamoto kwa moyo mwepesi, weka msisitizo kushinda changamoto zako na endelea kupambana kuhakikisha unazishinda
 
Ni ukweli ambao haupingiki kuwa ulimwengu wa nje ni mfano wa ulimwengu uliopo ndani mwetu. Hii ni kwa maana kuwa maisha na kila kitu ambacho mtu anakiona kinatokea nje ya maisha yake ni kutokana na taswira iliyopo ndani yake. Tunaposema ndani yake, ni kwa maana ya kilichopo katika akili yake, imani, nia, upande wa ndani wa ufahamu na kumbukumbu kwa ujumla. Kwa wahenga hapo kale walisema "Aliwazalo mjinga ndilo linalomtoke" kuhusiana na kuunganisha mawazo na fikra kuwa ni chanzo kikuu cha matokeo katika maisha yetu.

Kwanza matendo yetu ni matokeo ya mawazo yetu, matendo yetu yanakuwa mazoea yetu, mazoea yetu ndio yanayotengeneza tabia zetu, na tabia zetu ndizo zinazochagua aina ya maisha kila mmoja anaishi. Hivyo basi kuanzia kwenye mawazo yetu mpaka kwenye matendo yetu, ni dhahiri kuwa matokeo yake hufika mbali sana na kutuchagulia matokeo mengi kwenye maisha yetu.

Hata katika vitabu vya dini mfano Zaburi inasema kama mwanadamu awazavyo ndicyo itakavyomtokea; na hata Yesu alipokuwa anatibu na kufanya maajabu kwa yule mtu aliyekuwa anamuamini kuwa akishika joho lake atapona na akapona kweli alimjibu, Imani yako imekuponya. Kwa upande wa Budha na imani za Asia nazo zinasema kwenye Dhammapada kuwa "Imani ya mwanadamu ndio mzizi mkubwa wa matokeo mengi katika maisha" ni kama kivule na mwanga.

Katika tafakari ya leo tujichunguze na kutambua ni nini ambacho tunakiamini, tunakifahamu, na tunachokitenda ili kujua matokeo tunayoyazalisha. Imani na Akili ni kama shamba, upandapo chochote, utavuna kile kile unachokipanda. Je unapanda upendo, amani, tabia sahihi? Au unapanda Hasira, chuki, masengenyo na uvivu katika maisha yako?
 
Ni ukweli ambao haupingiki kuwa ulimwengu wa nje ni mfano wa ulimwengu uliopo ndani mwetu. Hii ni kwa maana kuwa maisha na kila kitu ambacho mtu anakiona kinatokea nje ya maisha yake ni kutokana na taswira iliyopo ndani yake. Tunaposema ndani yake, ni kwa maana ya kilichopo katika akili yake, imani, nia, upande wa ndani wa ufahamu na kumbukumbu kwa ujumla. Kwa wahenga hapo kale walisema "Aliwazalo mjinga ndilo linalomtoke" kuhusiana na kuunganisha mawazo na fikra kuwa ni chanzo kikuu cha matokeo katika maisha yetu.

Kwanza matendo yetu ni matokeo ya mawazo yetu, matendo yetu yanakuwa mazoea yetu, mazoea yetu ndio yanayotengeneza tabia zetu, na tabia zetu ndizo zinazochagua aina ya maisha kila mmoja anaishi. Hivyo basi kuanzia kwenye mawazo yetu mpaka kwenye matendo yetu, ni dhahiri kuwa matokeo yake hufika mbali sana na kutuchagulia matokeo mengi kwenye maisha yetu.

Hata katika vitabu vya dini mfano Zaburi inasema kama mwanadamu awazavyo ndicyo itakavyomtokea; na hata Yesu alipokuwa anatibu na kufanya maajabu kwa yule mtu aliyekuwa anamuamini kuwa akishika joho lake atapona na akapona kweli alimjibu, Imani yako imekuponya. Kwa upande wa Budha na imani za Asia nazo zinasema kwenye Dhammapada kuwa "Imani ya mwanadamu ndio mzizi mkubwa wa matokeo mengi katika maisha" ni kama kivule na mwanga.

Katika tafakari ya leo tujichunguze na kutambua ni nini ambacho tunakiamini, tunakifahamu, na tunachokitenda ili kujua matokeo tunayoyazalisha. Imani na Akili ni kama shamba, upandapo chochote, utavuna kile kile unachokipanda. Je unapanda upendo, amani, tabia sahihi? Au unapanda Hasira, chuki, masengenyo na uvivu katika maisha yako?
Asantee aunt
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom