Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo kama zamani
john-terry-of-chelsea-celebrates-with-the-trophy-after-the-barclays-picture-id474717042.jpg
 
Baba levo aachiwa huru ....

Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Revocatus Chipando ameachiwa huru katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya mashtaka matatu yakiwemo ya kusababisha vurugu, kufanya shambulio na kutoa lugha ya matusi dhidi ya muuguzi Christina Gervas wa Zahanati ya Msufini.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Hakimu Flora Mtalania kusema kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitsha bila shaka mbele ya mahakama hiyo kuhusu ukweli wa tuhuma zote.
Amesema mashahidi namba tatu (3) na tano (5) wa upande wa mashtaka wlijichanganya katika ushahidi wao kuhusu matusi na vurugu zilizodaiwa kufanywa na mshtakiwa huku shahidi namba moja upande wa Jamuhuri (Christina) akishindwa kuthibitisha shambulio alilofanyiwa kutokana na kutokuwa na PF3.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimi mkazi, Flora Mtalania aliyekuwa akisikiliza shauri hilo tangu Mei 4 mwaka huu amesema upande wa mashtaka unaruhusiwa kukata rufaa baada ya hukumu hiyo kama haijaridhishwa.
Kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili msanii na diwani hiyo, ilifunguliwa na mlalamikaji ambaye ni Jamhuri mbele ya mahakama ikiadaiwa kuwa Aprili 12, mwaka huu katika Zahanati ya Msufini mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa muuguzi Christina Gervas.
 
Jaji Mutungi: Vyama vya siasa acheni kujiendesha 'ki-SACCOS'...

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya Siasa nchini kuacha kujiendesha kama vyama vya kuweka na kukopa yaani SACCOS na badala yake vijiendeshe kwa misingi ya uendeshaji vyama vya siasa.
Jaji Francis Mutungi amesema hayo wakati akifungua mafunzo maalum ya siku mbili kwa viongozi wa vyama hivyo yanayofanyika Jijini Dar Es Salaam yakilenga kuwakumbusha majukumu na utendaji wao nyakati za uchaguzi ili kuepusha malalamiko ya hapa na pale.
Mafunzo haya yanafanyika kufuatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza kupitia vyama hivyo ambapo pamoja na mambo mengine watajadili na kuelimishwa pia kuhusu masuala ya mahesabu ya vyama na jinsi ya kusajili bodi ya wadhamini.
 
Moon athibitisha Kim kuzima kituo kikuu cha utengezaji makombora....

Rais wa Korea ya Kusini, Moon Jae-in amesema Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amekubali kuzima moja ya kituo chake kikuu cha kutengeneza makombora sanjari na maeneo yake ya kufanyia majaribio.
Hayo ameyasema huko mjini Pyongyang, baada ya mkutano wao ambao "wamekubaliana kuendelea kutimiza usitishaji wa uzalishaji nyuklia,"
Makubaliano hayo yameelezwa na Kim kuwa ni kama "hatua ya kusonga mbele" kurejesha jeshi la amani katika ukanda wa peninsula.
Kim pia amesema, anatumai "kutembelea Seoul katika kipindi kijacho" ziara inayotazamiwa kuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Korea Kaskazini.
 
MFAHAMU KANGAROO !

Kangaroo ni mnyama mwenye ufanano wa sura kwa mbali na sungura, wanyama hawa huwa na miguu mifupi sana ya mbele, kiasi cha kumfanya hata akimbiapo kutumia miguu miwili ya nyuma huku mkia wake ukimpa msaada mkubwa katika balance ya mwili, pamoja kwamba hukimbia kwa kunesa kama spring, lakini wakati mwingine mnyama huyu hutumia pia miguu yake ya mbele kutembelea hasa anapokula na kucheza na mtoto wake.
Madume wa kangaroo huwa wakubwa kuliko majike, wanyama hawa hufikia uzito wa kilo mpaka 90 na urefu wa futi sita, pia dume hutofautiana na jike kwa kwa muonekano wa rangi ambapo dume huwa kama wekundu kidogo mgongoni na majike huwa wakijivu.

Mnyama huyu ni miongoni mwa wanyama wanaokimbia sana, lakini kwa kuwa hutumia miguu miwili bahati yake huwa mbaya anapowindwa na wanyama walao nyama kama simba, kwakuwa hukosa uwezo wa kushindana nao mbio.

Kangaroo ni mnyama mpenda amani na si mkorofi hata kwa mtoto wake, isipokuwa madume tuu ndio hupigana hasa wanapopenda sehemu moja, na mapigano yao ni ya kustaajabisha miguu ya mbele hutumia kwa kushikana huku wakitumia miguu yao kupigania na hurusha mateke yake kwa miguu yote, huku mkia wake mrefu ukimpa sapoti ya kuweka sawa mwili wake.

Wanyama hawa hutumia pua zao vyema kunusa, na huwatambua maadui kwa kunusa tuu, maadui wake wakubwa ni wawili yaani simba pamoja na ndege tai, ambaye mara kwa mara hufanya majaribio ya kutaka kuiba watoto wa kangaroo.

Kangaroo jike ana mfuko ambao hutumia kubebea mtoto wake, mara zote ahisipo hatari humuingiza mtoto wake katika mfuko huo, na kisha kutoweka maeneo hayo na hata mtoto pia hujihami kwa kuingia katika mfuko wa mama aonapo kuna tatizo.

Jike limvutia dume kwa ajili ya mahaba, dume hunusa kwanza mkojo wake kutambua kama jike huyo yu salama au anataka kumuuzia kesi ya Mimba, hata hivyo jambo la kustaajabisha ni kwamba kangaroo endapo atapata mimba wakati mtoto wake bado ananyonya huweza kuzuia mimba hiyo isikue mpaka hapo atakapo muondoa mtoto aliyenaye kwa wakati huo.

Kama sisi tunavyomuheshimu twiga ndivyo hivyo hivyo anavyoheshimika kangaroo nchini Australia, Ni alama ya utambulisho wa taifa lao, pia amewekwa katika ngao ya taifa lao pia, ni mnyama anayependwa sana nchini humo.

Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna kangaroo kabisa, lakini cha kufahamu ni kwamba wanyama hawa hupendelea kuishi maeneo kame, na chakula chao kikuu ni majani tuu, alapo majani chakula kingine huweka akiba tumboni mwake, hivyo muda apumzikao hucheua na kuanza kula upyaa kama wafanyavyo mbuzi au ng'ombe.

Sifa zake.

1. Ana uwezo wa kukimbia km 22 kwa saa moja.
2. Kuogelea kwake sio ishu na akimbiapo anaweza katisha katika maji.
3. Wakati wa jua Kali hupumzika, jioni asubuhi ndio mida ambayo hupendelea kula.
4. Ana uwezo wa kuzuia mimba yake isikue.
5.huishi katika makundi yanayozidi kangaroo kumi.
6.kusalimiana kwa kangaroo ni kitu cha kawaida kama ilivyo kwetu.
7.ujanja wote kangaroo hawezi kutembea kinyume nyume.
8.katika mfuko wake anaweza kuwaingiza hata watoto wawili.
9. Ukimshitua au ikitokea hatari anaweza kuruka zaidi ya foot kumi na tano, kwahiyo hizo fensi za nyumba kwa kangaroo sio ishu kuruka pasina kugusa ukuta.

Baadhi ya nchi hujaribu kuwakuza wanyama ambao hawapo katika nchi yao, kwa kuwatafutia mazingira rafiki na watokako, kwa mfano kuna chura wetu wa kihansi walishawahi pelekwa nchi flani flani hivi, achilia mbali twiga aliyepanda ndege, na wengineo wengi walioondoka kabla.
 
MFAHAMU NGAMIA

Ngamia ni mnyama anayekula majani tuu, ni mrefu na mwenye ufanano na twiga kwa kiasi fulani, tofauti yao ni kwamba wakati twiga akiwa mrefu zaidi, ngamia ni mnene zaidi, pia twiga makazi yake ni mbugani lakini ngamia ni mnyama anayefugwa, kwa uzito hawaachani sana pia, mnyama huyu hubeba mimba kati ya miezi 12 mpaka 14 na huzaa mtoto mmoja au pacha kwa bahati sana, na mtoto huwa na kilo zipatazo 50 huku mgongoni akiwa hana Nundu kabisa.

Kwa Kimombo Ngamia anaitwa Camel, lakini neno hilo asili yake ni Latin likibeba maana ya respectively, ukiondoa jina hilo pia anafahamika kwa jina la Meli ya jangwani, ni mnyama mwenye faida lukuki sana, kwanza maziwa yake hutumiwa na binadamu, mnyama yake pia, wakati vinyweleo vyake na ngozi hutumika kuzalisha bidhaa kadha wa kadha, lakini kama haitoshi Ngamia pia ni usafiri, kwa ambao wamefika Sudan au Misri jambo hili wala halitawashangaza.

Maisha yao ni kati ya miaka 40 mpaka 50, kimsingi ngamia wapo wa aina Mbili, mwenye nundu moja ndio maarufu sana hapa Africa, wakati aina ya pili ambao hubeba nundu mbili na vinyweleo vingi wakipatikana huko Asia, waone na miili yao vile vile na mwendo wao wa taratibu lakini ukitaka kumuharakisha yawezekana pia, akishika njia haswaa hukimbia km 40 na zaidi kwa saa moja tuu.

Kwa urefu huwa na futi 6 mpaka 7, na uzito wao ukicheza kati ya kg 300 mpaka 1000 endapo matunzo mazuri atapewa, mtoto wa ngamia hupevuka anapotimiza miaka 7, Ngamia jike ni kiumbe ambaye kwa mapozi na malingo amebobea, humzungusha sana dume pindi anapotaka wastarehe, mpaka jike akubali na kujilaza chini dume hutumia mbinu nyingi sana, ikiwa ni pamoja na kumlamba, kumchezea shingo, kumkuna na anapokuwa mkaidi dume huchukia na kumuuma kabisa, hapo jike ndio kidogo atamfikiria fikiria kuwa jamaaa alipofikia sasa hakuna namna ! Na apewe tuu huduma !

Na kwa usumbufu huo jike akipitisha tuu jambo hilo, Dume hufidia akiingia hatoki mpaka afanye ejaculation zaidi ya mara tatu, ndipo aanze kutafuta pumzi ya round nyingine, hapo ndio atatoka huku jike wake akimkwepeshea macho kwa aibu ya usumbufu alioufanya !

Ukiondoa hayo Ngamia ni mstahimilivu sana katika mazingira ya ukame, anaweza akadumu kwa muda mrefu sana pasina ya kula wala kunywa, Na siri ya kuwa hivyo ni ile Nundu aliyonayo pale juu, huweza kubeba kiasi kingi cha wanga kinachomsaidia kujimudu anapokuwa katika mazingira kama hayo, hunywa maji zaidi ya lita 110 na si mwepesi kupata kiu .

Sifa zake za upekee.

1. Ni mnyama msikivu, mtulivu na mwenye nidhamu.

2. Ni mnyama mtii.
Huko uarabuni nasikia akisomea dua tuu analala tayari kwa kuchinjwa.

3.ukiwatumia kama usafiri we muharakishe jike tuu, dume atafanya haraka huwa hapendi kushindwa kwa jike.

4.madume huwa wakubwa na warefu kidogo kwa majike.

5. Ni mnyama mwenye heshima yake Uarabuni, kama ilivyo twiga Tanzania au Kangaroo kwa Australia.

6.hupendelea kuishi kifamilia

7. Ukiwa naye jangwani na kukiwa na uhaba wa maji anaweza kukuongoza mpaka sehemu mtayopata maji.

8. Ngamia jike hutoa maziwa kuanzia Lita 15 na zaidi.

8. Ni mnyama mpenda amani na rafiki sana kwa binadamu.

Wakati hapa Tanzania wajasiriamali wakihamasishwa kufuga kuku kwa ajili ya chakula na biashara, huko Sudan mwaka Jana walikuwa wanafanya campaign ya kufuga ngamia kwa sababu kama za sisi kufuga kuku.

Hata hivyo imefahamika kwamba wanyama ambao huwa hawapatikani katika jamii fulani, kitoweo chao ukipeleka katika jamii hiyo watu wake hupata tabu sana katika matumizi, sasa nakuacha na swali je waweza kunywa maziwa ya ngamia na kuila nyama yake !
 
#Kakakuona (Pangolins), Ni mnyama mwenye mwili ulio zungukwa na magamba, chakula chake kikuu ni mchwa (ant eater), na hupatikana karibu au kwenye vichuguu na kipindi cha ukame huranda sana kutafuta vichuguu ili apate chakula.

Mwili wa kakakuona umefunikwa na magamba magumu, yaliyofunika mgongo wote na ubavuni na sehemu za miguu, magamba hayajafuka sehemu za chini ya mwili wa mnyama pamoja na kichwa.

hivyo hujilinda kwa kujizungusha (roll) kama tairi akificha sehemu laini pamoja na kichwa katika kujilindana maadui zake.

Kichwa cha Kakakuona ni kidogo lakini kirefu Pia mkia wake ni mrefu na mpana (broad tails).

Ni mnyama asiye na meno na hawana masikio yaliyo jitokeza nje Kiasi ya kwamba unaweza kudhani kuwa hawezi kusikia sauti yoyote, lakini ni mnyama mwenye uwezo mkubwa sana wa kusikia.

Ni mnyama mwenye uwezo wa hali ya juu sana kwenye kuhisi harufu, ila si mwenye kuona vizuri (poor sight) kwa ajili hii basi mnyama huyu hutembea kutafuta chakula usiku (noctunal) huweza kutembea maili chache kila usiku na kutumia shimo kama nyumba yake kwa takribani mwezi mmoja.

Kakakuona anaulimi mrefu sana ukilinganisha na mwili wake(16") unaomuwezesha kula mchwa kwa kupenyesha ulimi kwenye tunnels za kichuguu kupata mchwa.

Pia tumbo lililo kama filigisi analotumia kusagia chakula pamoja na mchanaga na vimawe anavyokula, hii ni kwa ajili ya kukosa meno.

Kakakuona huishi maisha ya kujitenga au mmoja mmoja( solitary) ingawa pia hutokea dume likawa na jike nyumba moja kwa muda, pia mama hukaa na mtoto wake mpaka miezi minne.

Mtoto huzaliwa amepauka (pale) na magamba laini ambayo huanza kukomaa ndani ya siku ya pili ya maisha yake. na hutembea na mama yake juu ya mgongo na wakati wa hatari kujiviringisha ndani ya mama yake.
 
Simba kama afahamikavyo kuwa ni mfalme wa pori anasifa mbalimbali ambazo nyingi unaweza ukawa unazijua kulingana na uelewa wako, lakini kwa sifa kabambae na za uhakika juu ya hayawani huyu ni kama ifuatavyo:-

1. Simba ni miongoni mwa jamii ya paka wakubwa akiwa ni wapili kwa ukubwa nyuma ya chui.

2. Simba dume katika ‘group’ la simba huwa ndiye wa kwanza kula windo kabla ya wengine kula,tofauti na inavyoelezwa kuwa jike ndiyo huwa wa kwanza.

3. Jina lingine la Simba dume ni Tom, wakati jina la simba jike ni lioness.

4. Kuna aina saba za Simba ambao ni Simba wa kiafrika,simba wa marekani, simba wa milimani, simba weupe, simba wa kiasia na simba aina ya cave.

5. Simba ana uwezo wa kutembea zaidi ya siku nne au tano bila kunywa maji.

6. Familia ya simba inaitwa ‘pride’na inaundwa na dume mmoja na jike mmoja huku watoto wakiwa kuanzia wawili hadi watatu huku miongoni mwa watoto hao mmoja akiwa ni dume.

7. Uzito wa simba kijana ni kati ya pound 330 hadi 500,kwa kawaida simba dume kijana anakuwa mrefu kuliko simba jike kijana.

8. Kwa kawaida Simba hutumia zaidi ya saa 16 hadi 20 kwa ajili ya kulaa na kupumzika kila siku.

9. Endapo katika famila ya Simba,akapatikana dume jipya,dume huyo huwauwa simba wadogo na kuwala.

10. Kiumbe pekee ambacho kinaogopwa na Simba ni binadamu.
 
Maisha Ya Simba Dume Ni Ya Misuko Suko Sana.

Simba ni mnyama anayesifika kwa ukali mpaka kubatizwa jina la mfalme wa nyika.

Cheo cha ufalme wa nyika hauendi kwa simba jike bali cheo hicho ni mahususi kwaajili ya simba dume.

Wapo wanaodhani simba dume ni mzembe sababu mara nyingi hashiriki kwenye kuwinda na kuleta kitoweo bali simba jike ndiye anaye hustle sana kuwinda na kuua kitoweo,wengi wanaowaza hivi hawaelewi vizuri majukumu na kazi ya simba dume.

Simba hupendelea kuishi kwa mtindo wa familia pale simba wanapozaa watoto hutambulika kwa jina la pride tuseme kwenye familia kuna simba dume ,jike na wadogo zake sasa huyu jike akipewa mimba na akizaa sasa rasmi kikundi hicho cha simba hujulikana kama pride.

Kwa kuwa makala yetu imejikita kuzungumzia maisha ya simba dume basi tujikite kwenye mada husika ,mara nyingi simba akijifungua jike wanakuwa wengi na dume wachache.

Hawa watoto watalelewa vizuri kwa kupatiwa maziwa mpaka pale watakapofikia hatua ya kula nyama maisha ya watoto hawa wote jike na dume huwa ni ya furaha wanacheza ,wanakula na kufanya kila kitu na hata kuchezea sharubu za baba.Maisha huanza kubadilika baada ya watoto hawa kufikisha miaka 2 kamili au kasoro ,jike wataishi kama awali kula ,kucheza ,kufanya utundu nk lakini simba dume akifikisha umri huo huwa anakuwa makini sana hata fujo ,utundu huwa hafanyi na pindi mnyama akiuliwa kwaajili ya kitoweo simba huyu huwa hagombanii chakula na endapo baba yake akitaka kipande kikubwa cha nyama na kuleta ubabe mtoto huyu wa kiume hujisogeza pembeni ila watoto wa kike wanaweza kudinda .

Maisha ya mtoto wa kiume akishafikisha umri huo huwa hamjaribu kabisa baba yake na pia mzee simba huwa anamvutia sekunde ,dakika ,saa ,siku ili amvae mwanaye na amchane ukweli.Endapo mtoto huyu wa kiume aki test uvumilivu wa mzee kwa kugombania msosi ,kufanya mautundu ,kucheza na shangazi zake basi mzee simba uvumilivu utamshinda.

Simba dume akishafikisha miaka 2 huwa anasubiria sekunde ,saa au siku atimuliwe na baba yake kwenye familia aende kujitegemea huku watoto wa kike wakibaki kwenye familia kupata msosi wa bure.

Siku mzee simba frustrations zikimjaa humvaa mwanaye wa kiume na kumfukuza kwenye eneo lake na simba dume huwa ana miliki eneo mpaka mile 10,na simba kijana lazima asepe na hapa mzee simba huwa ni mkali hana msalia mtume anamfukuza kwa ukali kama vile hamjui mwanaye kama vile sio damu yake hapa simba kijana husepa zake na mzee simba humfukuza huyu kijana mpaka ahakikishe kashaondoka katika eneo lake la mile 2,3 ,10 nk .

Hapa simba huyu kijana mwenye miaka 2 au 2 kasoro akiwa ndio anaingia kwenye balehe ila bado hayupo fiti anajisepea zake huku akitizama nyuma haamini anaachana na mama yake ,ndugu zake.simba huyu huanza maisha mapya akiwa pekee yake.

Simba huyu atakutana na vikwazo vingi njiani kwanza fisi ,inatambulika fisi na simba ni maadui na fisi huishi kwa ukoo..koo moja ya fisi inaweza kufikisha idadi ya fisi 18 .

Sasa simba huyu kijana akikutana na fisi hawa ataweza kushambuliwa tu na meno ya fisi ni makali kuliko mnyama yeyote yule sasa simba huyu akiwekwa kati na fisi wakamzunguka kama akinusurika basi ni majeraha na simba akipata majeraha ina maana atashindwa kuwinda na kifo kitamsogelea.

Pili simba huyu ataingia eneo la simba dume na hakuna jambo hatarishi kama kupita au kuingia eneo la simba dume hapo lazima kiwake na kwakuwa simba huyu aliyefukuzwa kwao bado mdogo lazima ataumizwa vibaya kama sio kuuliwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom