Makapuku Forum

Makapuku Forum

Bandiko zuri sana mdau, asante lakini unajua ni kwanini wengine hatuna huo muda wa kukaa tunasoma au kutafuta maarifa mapya kila wakati? Tumeanza majukumu ya familia tukiwa wadogo na hadi tumeweza kununua simu na laptop kuingia JF ni kwa sababu tumeajiriwa na muda wote mwajiri anatutumia hatupi nafasi ya kufanya yale tunayopenda. Kikubwa tunafanya kazi kuhaklikisha watoto wetu waka sawa, hawawi kama sisi. Mungu kumtanguliza ni sawa, lakini si hata kwa Mungu kuna madaraja? bahati mbaya ukiniangalia mtu kama mimi, nyumba zuri zote mjini nilikuwa kibarua, mkono wangu upo kweli kila tofari la pembeni, nilitamani kuweka jina langu lakini mpiga plasta akasema hataki uchafu. Mpiga rangi naye akasema plasta ina harara hivyo akapiga rangi kuondoa harara, hawa wote kama mimi tu nao hawatambuliki na sadaka wanatoa.

Haka katoto ka imam wangu nakaangalia kila siku kanavyotoka chuo kikuu kanakuja na maneno makubwa makubwa, kanachosha akili yangu ambayo matofari na misumali imeichosha, na kakianza kuongelea kuondokana na umaskini nakatizama maana najua kabisa zaka zangu ndo zinakafanya katambe, kanasema kana homuweki wakati mmi na wenzangu homuweki yetu ni kitandani nikirudi home namkuta wifi yako ananisubiri kuniongezea uchovu.

siandiki haya kujitetea na kupotosha lakini natamani uandike wengine ninaowafanyia kazi na wananilipa wanithamini, watambue kabisa nyasi nikifyeka nawaepusha na nyoka.

Sasa umeziona akili zangu za week days
Pole binamu imejitetea sana
 
  • Thanks
Reactions: Obe
...biashara ya simu sijawahi kufanya kwa kweli labda unifundishe. sasa fanya fasta kutuma namba ili nishiriki fursa. Afu unaonekana wewe ni mtu makini sana maana unaongea biashara, sasa mimi nimevuana korosho hapa unaweza kuniunganisha na wafanyabiashara wanunue, mimi narudisha mtaji faida unakula wewe 96 percent
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Pole binamu imejitetea sana

...kujitetea ni uungwana binamu, si unajua mimi ndugu yako ni muungwana ila tatizo nikiomba namba kwa ABJ hataki kunipa, au sio yeye sio muungwana? Au hana simu anipe hata ya uongo
 
...kikaratasi kile nilitaka bili yangu asijumulishe na ya kwako maana nilione heineesy ulizopeleka meza ya karibu na kaunta
Mambo gani tunafanyianaa ankoo binamu ujee wewe ndo umenitoaa ndanii kwamba tuzuge na unajuaa tokea jpili yaliyonikutaaa
 
...biashara ya simu sijawahi kufanya kwa kweli labda unifundishe. sasa fanya fasta kutuma namba ili nishiriki fursa. Afu unaonekana wewe ni mtu makini sana maana unaongea biashara, sasa mimi nimevuana korosho hapa unaweza kuniunganisha na wafanyabiashara wanunue, mimi narudisha mtaji faida unakula wewe 96 percent
waaow tena korosho huku niliko wahitaji ni wengi etii aisee ntakuwaje tajiri mimi namba natuma sasa hivi 96%ya faida ni yangu nakosaje kukugea namba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom