Makapuku Forum

Makapuku Forum

Umejikuta tu uko bussy siku nzima katika mipangilio yako ya kazi? Umekuwa ukivuta muda mara nyingi?

Kama jibu kako ni ndio, Hutumii muda wako vizuri. Inaonekana kwamba umefungwa akili yako kwenye hio hali uliyonayo sasa. Na kazi hio ndio inakula muda wako na nguvu zako nyingi.

Kwa mfano. Unaamini kwamba kucheki emails zako zinakupa matokeo mazuri au kukaa kwako kwenye mikutano mingi? Unaweza kufikiria hivyo. Lakini mwisho wa siku ni kiasi gani cha kazi yenye faida kwako umekamilisha?

Kwa bahati nzuri , umeona kabisa kwa kifupi tu kwamba , inawezekana kupunguza vitu visivyo na umuhimu ambavyo vinajaza nafasi yako na kukosa kufanya vitu vinavyokuletea mafanikio . Ingawa kila mtu kabla alipitia huko na kupoteza muda mwingi kwenye kazi za watu wengine.

Unaweza ukawa ni moja ya watu ambao wanaona kupungua katika utendaji wao wa kazi kutokana na kujali sana mambo ya mitandao , Ni kweli lakini usijisikie vibaya. Kila mtu huwa anapotea karibu kila mara kwenye maisha. Na hii ni kwa sababu , kama tutaweza kuwa wakweli ni rahisi kuweza kufanya vitu vya muhimu zaidi kuliko kufanya mambo yasio na msingi katika maisha yetu.

Ni jumamosi asubuhi na unajisikia kuchoka , Na ndio kwanza hutaki kwenda kazini kumalizia kazi ambazo ni za muhimu. Mara unaamua kwenda kupata kahawa nje ya ofisi yako. Ingawa umeingia kwenye mtego mbaya ambao haukuwezeshi kufanikisha malengo yako, umeshindwa kufanya kitu chako kiwe na kipaumbele kwako. Kwa sababu hio , nakuambia kuwa bado unafanya kazi ambayo sio muhimu katika maisha yako.

Kwa mfano ni mara ngapi unafanya kitu chako mwenyewe asubuhi unapoamka kama sio kuchungulia meseji kwenye smart phone yako, kucheki instagram, facebook na vingine. Jibu hapa ni ndio , unafanya hivyo kabla ya kazi zako za muhimu. Kwa kesi hio unajikuta unapoteza saa nzima kwa kupitia hivyo vitu visivyo na maana katika maisha yako, unajikuta hujacheki malengo yako. Wakati mwingine unajikuta vijiweni kuongea umbea wa wanawake au wanaume , na hio ndio unaiita mikutano yako. Ukijakukumbuka muda umepita hujafanya chochote kinachohusu malengo yako.

Sifahamu kuhusu wewe, lakini mimi nimeona baadhi ya watu wanapenda kukusanyika kwa ajili ya kudiscuss, kuwepo, ili kutatua matatizo .

Lakini kuna kesi nyingi ambazo nimeona watu wakipoteza muda kwenye hio mikutano bila ya sababu za msingi. Unapoteza muda wako na muda wa wengine.

Ingawa kuna mikutano mingine ya muhimu , lakini mingi sio ya muhimu. ni kupotezeana muda tu.

Kila kitu katika maisha kina matatizo yake. na hii inatokana na jinsi unavyofanya kazi zako.

Kama unatumia muda mwingi katika kufanya kazi ambazo sio za muhimu, Hutaweza kuona matokeo makubwa. Kusema kweli, Uzalishaji wako utakwama. Kwa sababu muda wako umekuwa ukiliwa kwa kujaribu kufanya kazi ya mtu mwingine kusubiri ulipwe mshahara. Sehemu mbaya zaidi ni hii, utajikuta umepoteza muda wako , umri umeenda, hujafanya chochote katika malengo yako

Utafanyaje kuondokana na hili tatizo?

Tafuta ujasiri wa kuondoka katika mtego huo. Haijalishi una kazi gani, hutaweza kutumia muda vizuri, masaa yako utatumia kwenye kazi ya mwanaume mwenzako au mwanamke mwenzako. utashuka thamani kila siku, hutakamilisha lengo lako.

Ukiweza kupata ujasiri tu wa kufanya kitu chako mwenyewe, tayari utakuwa umeokoa muda wako. Utafanya kitu kilicho sahihi, kitu ambacho tunakiita KAZI sio Kibarua.

Kumbuka kama umekwama mahali huelewi kitu cha kufanya. Unaona kabisa kazi uliyonayo huna furaha nayo, Una malengo hujayafanyia kazi, Ongea na bosi wako kuhusu kazi yake. Fanya kwa masaa 6 tu na kwa uhakika na kwa juhudi zote. kisha uwe na lengo, fanya kwa mkataba . jiwekee mipango ya kufanya kazi. Ukifanya kwa uaminifu, muda wa miaka mitatu tu, Utapata kazi yako mwenyewe.
 
Uchumi wako una masaa mangapi? Wewe ni mtu unayeandika kitu unapofundishwa? unasoma vitabu ? Unafikiri kwa muda gani? Unatafuta taarifa za kutosha? Unatafuta wazo ndani yako?

Kitu gani unaweza kuonyesha ambacho tayari umekifanya kipindi chote cha maisha yako mpaka hapo ulipo sasa hivi? Mungu huwa hampi mtu yeyote ambaye ni mjinga miujiza mikubwa zaidi ya uponyaji mdogo.

Muda ukitumika vibaya lazima utakuwa mtu wa madeni mengi, utakopa sana. Anza sasa kujiuliza tangu mwaka ulipoanza ni kitu gani umekifanya cha Mungu.

Uchumi wa Mungu ni masaa 24. Huenda kuna mtu amebeba majibu ya maisha yako, anza kuuliza maswali. Kama ukichezea muda wako ni ngumu sana kufanikiwa.

Kazi ya Muda.

1.Kufikiri. jiulize umewahi kupata nafasi ya kukaa mahali na kufikiri kwa dakika kadhaa? kama hujawahi wewe hujaanza kuishi bado.

2.Wazo. Mawazo yako unayopata , unayaandika au kuchora mahali ili Mungu aone nia yako akusaidie kuvuka mahali ulipo?

3.Kutafuta Taarifa sahihi. Unatafuta semina mbalimbali ili kujifunza, unasoma vitabu gani ambavyo vinaweza kukupatia ufahamu wa kutosha, Unasisikiliza kitu gani ili ujifunze , unatazama nini, kitu gani unakipenda na nini hukipendi.

Unataka kuwa na kampuni kubwa anza kutengeneza maneno kwanza. hakuna kitu kinachotokea kabla ya Neno. Simu inatengenezwa kwa kutumia kitabu chake. Mungu aliumba Ulimwengu kwa neno. Gari inatengenezwa kwa kuanza na maneno ya kwenye karatasi kwanza. Mwanadamu ni kitabu chake cha imani.

Kama muda wako umejaa masaa 24, tazama huo muda unaufanyia nini? Muda una nguvu, Heshimu muda. Mtu anayeheshimu muda huheshimika, huonekana kuwa ni wa thamani . Ukitumia muda vizuri utakubalika na Mungu pamoja na wanadamu.

Unachotakiwa kufanya leo ni kuandaa list yako ya 2018. Nimetamani nikusaidie kitu gani cha kuanza kwanza.

Kabla hujaandika mambo yako yote, Anza kuandika mambo ya Mungu. Andika vitu ambavyo utamfanyia Mungu , Kazi ya Mungu mwaka 2018. Ukimaliza hayo, Anza kuorodhesha ya kwako.

Put God First.

1.

2.

3.

4.

5.

…………

Andika ya kwako.

1.

2.

3.

4.

5.

Unaweza kuandika list ndefu sana ya kukutosha wewe. Nakutia moyo fanya hivyo utaona mambo mapya yakitokea katika maisha yako.

Mungu Akubariki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom