Makapuku Forum

Makapuku Forum

TUOMBE:Baba yetu na Mungu wetu tuna kila sababu ya kukushukuru kwa sababu umekuwa mwema mnoo kwetu na umetuamsha tena leo JUMANNE tarehe 18 Septemba 2018 wako watu wengi hawajaweza kuamka kama tulivyo Baba Sifa Shukurani Heshima na Utukufu ni kwako tu Mfalme wa Amani.
Tunakuja kwako tena kuleta shukurani zetu na mahitaji yetu ..hatuna mahali pengine popote pa kuyapeleka ...Asante Baba maana tunajua siku zote uko upande wetu..Asante kwa faraja idumuyo hata kama tunalia bado unatukumbatia na unatukumbusha kuwa yote ni mapenzi yako na tukushukuru .Asante kwa ajili ya familia zetu,wenza wetu,marafiki zetu na umoja wetu ..hujawahi kutuacha katika yote..bado tumaini letu unalifanya lijenge imani kuu ipitayo yale tuwazayo kibinadamu.Roho Mtakatifu
Tunaomba endelea kutusimamia,kutupigania,kutufundisha na kutuongoza,kutufariji katika kila hatua.
Ponya wagonjwa Baba ,waliopondeka mioyo,wenye changamoto mbalimbali Baba wape suluhisho.Angalia watoto wetu waongoze katika kweli na kila hatua ya maisha yao tupe utu wema ,kiasi na kila kitu tutende kwa sifa na utukufu wa jina lako.tuliza dhoruba katika familia,katika jamii na makazini ili tuishi maisha ya utulivu na ya kukupendeza .Tunaomba faraja yako endelea kutusimamia hesabu hatua zetu zikupendeze siku zote tuwe nawe Baba..Asante Baba kwa yote maana ni mema .Tunaombea wasafiri wasafiri salama damu Takatifu ya Yesu Kristo iwafunike,angalia wafiwa wajane,wagane ,yatima wote waweke tumaini kwako wape makazi wasio na makazi,imarisha upendo katika familia maana ndio mahali umeweka kwa ajili ya kuimarisha utu wa kila mmoja wetu.saidia wote ambao hawajakujua wewe Baba wakujue,wakupende na wakutumainie maana kwako ipo furaha,ipo amani ipo nguvu,ipo afya..Asante Baba maana unaendelea kutuonyesha na kutufundisha matendo yako makuu na kutukumbusha wajibu wetu tukiwa hapa duniani safari ambayo wewe ndie kiongozi wetu ambaye tunapaswa kuleta mizigo yetu yote kwako maana PEKE YETU HATUWEZI..tunaleta upweke wetu,magonjwa yetu,kupungukiwa kwetu,fadhaa zetu,mioyo yetu ,mawazo yetu,miili yetu ,dhiki na taabu zetu,familia zetu Baba shughulika na kila kimoja tupate Amani mpya.
Baba tunayo mengi ya kusema lakini twafahamu unajua hata hesabu ya nywele zetu endelea kuhesabu siku zetu na huruma yako iwe kwetu daima.
Naomba yote katika jina la Yesu Kristo Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen

JUMANNE NJEMA YA FARAJA NA MATUMAINI DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya winga wa Manchester City Raheem Sterling na klabu yake yamegonga mwamba Sterling, 23, huku mkataba wa raia huyo wa England ukielekea ukingoni. (Guardian)
 
Crystal Palace imeulalamikia Uongozi wa Ligi Kuu Uingereza kwa kushindwa kumlinda staa wao Wilfred Zaha, 25, ambaye pia ni raia wa Ivory Coast anaokuwa uwanjani akicheza. (Telegraph)
 
Mkurungezi wa michezo wa Roma Monchi amesema walilazimika kumuuza mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 26, kwenda Liverpool kwa sababu ya Sheria ya Uchezaji Haki Kifedha michezoni. (El Mundo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom