Makapuku Forum

Makapuku Forum

Hivyo hivyo bwana mm nakupenda tu T the Don urudi tulewe zetu Heineken majuzi nililewa mm sijui Heineken 9 sijui 10 mpaka nilikuwa nagombana na dereva wangu wa bajaji alinifata ananiambia lasivyo nakuacha beba beer zilizobaki tuondoke imebidi nijibebee beer mbili zilibaki
Hahahaa! Umenza sasa..

Mimi ni mtoto wa mkulima wa mzee Sharubukuwasha
 
Hivyo hivyo bwana mm nakupenda tu T the Don urudi tulewe zetu Heineken majuzi nililewa mm sijui Heineken 9 sijui 10 mpaka nilikuwa nagombana na dereva wangu wa bajaji alinifata ananiambia lasivyo nakuacha beba beer zilizobaki tuondoke imebidi nijibebee beer mbili zilibaki
Aiseee! Polee sana..!
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Rau wilayani Moshi, Emmanuel Tarimo (18) amejinyonga hadi kufa baada ya kuhojiwa zaidi ya saa 5 na walimu akituhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake. Emmanuel alijinyonga jana kwa mkanda, nyumbani.
Screenshot_20180906-124222.jpeg
 
Serikali ya Benin imepitisha pendekezo la kuanzishwa kwa kodi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

Wanaharakati na waandishi wa habari wamepinga kusudio hilo huku wakiwashinikiza wananchi kutofuata (unfollow) kurasa zote za wizara na mawaziri, na kupinga kuanzishwa kwa tozo hiyo.
Screenshot_20180906-124356.jpeg
 
Rais Dkt MagufuliJP akiangalia dawati lililotumiwa na Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere wakati akisoma katika Shule ya Msingi Mwisenge mkoani Mara.

Mwl. Nyerere alipata elimu yake ya msingi shuleni hapo kati ya 20 Aprili 1934 hadi 1 Oktoba 1936.
Screenshot_20180906-124457.jpeg
 
Idara ya Maafa imesema hakuna tishio la tsunami katika Bahari ya Hindi na kwamba taarifa inayosambazwa si ya kweli.

Mkurugenzi wa idara hiyo amesema, taarifa za tsunami zinapotolewa wananchi hawachukulii uzito, hivyo leo walilenga kuangalia wananchi watalichukuliaje tishio hilo.
Screenshot_20180906-124559.jpeg
 
Mahakama nchini Myanmar imewahukumu waandishi wawili wa habari za kiuchunguzi wa shirika la Reuters, Wa Lone (32) na Kyaw Soe Oo (28) kifungo cha miaka 7 jela kila mmoja kwa kuandika habari za mauaji wa Waislamu wa eneo la Rohingya, ikieleza ni kuvunja sheria ya siri za taifa.
Screenshot_20180906-124702.jpeg
 
Idara ya Maafa imesema hakuna tishio la tsunami katika Bahari ya Hindi na kwamba taarifa inayosambazwa si ya kweli.

Mkurugenzi wa idara hiyo amesema, taarifa za tsunami zinapotolewa wananchi hawachukulii uzito, hivyo leo walilenga kuangalia wananchi watalichukuliaje tishio hilo.View attachment 858921
Ambao pressure zilipanda na kulazwa hospitali je??
 
Mahakama ya Juu nchini DRC imemzuia kiongozi wa upinzani Jean-Pierre Bemba kuwania kiti cha urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Disemba, kufuatia kutiwa hatiani na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kosa la kuwahonga mashahidi katika kesi inayomkabili.
Screenshot_20180906-124806.jpeg
 
Hivyo hivyo bwana mm nakupenda tu T the Don urudi tulewe zetu Heineken majuzi nililewa mm sijui Heineken 9 sijui 10 mpaka nilikuwa nagombana na dereva wangu wa bajaji alinifata ananiambia lasivyo nakuacha beba beer zilizobaki tuondoke imebidi nijibebee beer mbili zilibaki
Angalia usije angusha gari, vijana hawana maana.. Kuja kuamka asubuhi watu wamevunja mayai km trei tatu vile.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom