Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kwenye jiji la San Fransisco nchini Marekani unaweza ukalipwa dola 21,250 (milioni 48 za kitanzania) / mwezi kwa kufanya kazi ya kuondoa vinyesi kwenye mitaa ya jiji hilo.

Jiji la San Fransisco kwa sasa linakabiliwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira kutokana na watu kujisaidia hovyo kwenye njia za watembea kwa miguu na inaripotiwa tangu mwaka huu uanze zaidi ya watu 15,000 wametoa malalamiko ya kukutana na vinyesi kwenye mitaa ya jiji hilo ambapo imepelekea meya wake kuunda timu ya watu sita inayofahamika kama 'Poop Patrol' ambao wao kazi yao itakuwa ni kuondoa vinyesi mitaani kwa mshahara wa dola 21,250 (milioni 48 za kitanzania)
Screenshot_20180906-151348.jpeg
 
Utafiti mpya unaonesha kwamba mwanga wa bluu unaotoka kwenye simu maizi (smart phone) na kompyuta bapa (tablet) ndio chanzo kikubwa cha upofu wa macho.

Watafiti kutoka chuo cha Toledo walisema kwamba kama mtu anatumia muda mwingi kukodolea mwanga wa bluu ambao mara nyingi unatoka kwenye luninga, simu maizi, kompyuta na vitu vingine vinavyoendana basi kuna uwezekano mkubwa mtu huyo kuwa kipofu kwa sababu mwanga huo huwa unatengeneza molekuli za sumu kwenye seli ambazo kazi yake kuhisi mwanga kwenye macho.

Watafiti hao pia walishauri ni vizuri kuepuka kutumia simu, kompyuta na vitu vingine vinavyoendana nyakati za usiku kwa sababu mwanga huo wa bluu huwa unatokea sana nyakati hizo.
Screenshot_20180906-151406.jpeg
 
Kampuni moja kutoka nchini Japani wanatengeneza mwamvuli ambao hautokuwa na haja ya kuushika.

Mwamvuli huo unaofahamika kama 'Free Parasol' utakuwa unatumia akili bandia ya kompyuta (AI) kuweza kupaa usawa wa kichwa cha mtu huku akiwa anatembea na unategemewa kuingia sokoni mwaka 2019 kwa dola 275 (zaidi ya 600,000 za tz), na mtu atakuwa na uwezo wa kutembea nao kwa saa moja kabla ya kuuchaji tena.
Screenshot_20180906-151438.jpeg
 
NASA wanaanda mpango wa kwenda kutembelea 16 Psyche jiwe lenye thamani ya dola quadrilioni 10,000 - yaani kama binadamu wakiweza kwenda na kurudi na sehemu ya jiwe hilo basi watayumbisha uchumi wa Dunia kwa sababu uchumi wa Dunia kwa sasa ni dola trilioni 78 sasa waingize kitu chenye thamani ya dola quadrilioni 10,000 haitokuwa vizuri.

Safari hii kama ikifanikiwa basi itafungua njia kwa makampuni ambayo yanataka kuanza kuchimba rasilimali zilizokuwa nje ya Dunia.
Screenshot_20180906-151505.jpeg
 
Hii ni picha mpya ambayo imepigwa na darubini inayofahamika kama Hubble. Kwenye picha hii kwa kila kidoti unachokiona hapo ni galaksi, nyingi zikiwa na nyota ambazo ni changa na unaambiwa eneo hilo pekee kuna zaidi ya galaksi 15,000 nyingi zikiwa na nyota ambazo zipo katika hatua za ukuaji miaka bilioni 3 iliyopita hatujui sasahivi zitakuaje kwa sababu mwanga umetumia miaka bilioni 3 mpaka kutufikia sisi hivyo hakuna anayejua leo zipoje.

Kwa kukuonesha tu kwamba ulimwengu ni mkubwa sana na wewe si kitu, hebu fikiria Jua letu ikiwamo na sayari, miezi, mawe na vitu vingine vyote vinavyolizunguka vipo ndani ya galaksi inayofahamika kama Milkyway, hii galaksi imebeba zaidi ya nyota bilioni 400 ikiwamo na Jua letu zidisha hiyo idadi mara 15,000 ndipo utapata namba ya nyota na sayari ambazo zipo kwenye hii picha.

Swali ambalo limekuwa kwenye vichwa vya wengi ni juu ya uwepo wetu kwenye huu ulimwengu kwamba sisi tupo peke yetu au kuna viumbe wengine huko kusiko fikika na kama jibu ni ndio kuna viumbe wengine kwa nini hawaji kututembelea na kama hakuna viumbe wengine kwa nini sisi tuwe peke yetu kwenye ulimwengu mpana ambao unatanuka kwa kasi kubwa kuliko mwanga.

Kumbuka idadi ya nyota ulimwenguni ni kubwa kuliko idadi ya michanga yote ambayo ipo Duniani na baadhi ya nyota inasemekana zinazungukwa na sayari ambazo zinafanana kabisa na Dunia yetu ikiwa na maana kuna uwezekano wa maisha.




Screenshot_20180906-151518.jpeg
 
NASA watoa tahadhari dhidi ya jiwe kubwa sawa na piramidi za mistri, ambalo linategemewa kupita karibu na Dunia yetu usiku wa leo.

Jiwe hilo linalofahamika kama 2016 NF23 ni moja kati ya mawe makubwa matatu (2001 RQ17 pamoja na 2015 FP118) ambayo yanayotegemewa kupita karibu na Dunia yetu mwanzoni mwa mwezi wa tisa.

Screenshot_20180906-151537.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom