Makapuku Forum

Makapuku Forum

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Majaji wateule watatu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika mkoani Arusha mapema Agosti 27, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Imani Aboud naye ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama hiyo.

Majaji wengine wawili ambao ni Jaji Blaise Tchikaya kutoka Kongo na Jaji Stella Isibhakhonem Anukam kutoka Nigeria. Majaji hawa watatu wameapishwa baada ya baadhi ya waliokuwa Majaji wa Mahakama ya Afrika kuachia nafasi zao kwa sababu mbalimbali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamuziki mwanasiasa Bobi Wine ambaye amekuwa akizuiliwa kwa karibu wiki mbili nchini Uganda pamoja na wanasiasa wengine 32 wa upinzani wameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu, kaskazini mwa nchi hiyo.
Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi amepewa dhamana pamoja na wabunge wengine watatu, na watuhumiwa wengine wanane.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.
Kassiano Wadri aliyeshinda ubunge Arua ni miongoni mwa wabunge waliokuwazuiliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Klabu nne za England watatambua wapinzani wao katika awamu ya makundi ya mashindano ya kuwania ligi ya mabingwa Ulaya wakati droo itakapofanyika Alhamisi.
Manchester City itakuwa katika chungu cha kwanza na Manchester United na Tottenham Hotspur katika chungu cha pili huku Liverpool ikiwekwa kwenye chungu cha pili au cha tatu.
Droo inatarajiwa kufanyika Grimaldi Forum huko Monaco mwenda wa saa moja usiku saa ya Afrika Mashariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vilabu 26 vilivyofuzu moja kwamoja kwa awamu ya makundi, huku sita zikitarajiwa kufuzu baada duru ya pili kukamilika Jumatano.
Uteuzi unafanyikaje?
Washindi katika ligi ya Mabingwa na ligi ya Uropa wanafuzu kuingia katika chungu cha kwanza , pamoja na mabingwa katika mataifa sita yalioorodheshwa juu.
Hii ina maana kuwa kuna timu tatu za Uhispania, miongoni mwa timu kuu msimu huu kwasababu Real Madrid ilishinda kwa mara ya tatu ligi ya Mabingwa, Atletico Madrid nayo ilitawazwa washindii wa taji la ligi ya Uropa na Barcelona ilijinyakulia taji la La Liga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom