Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Moja Kujifunga, Mbili Kuona Mbali.

...msomi Kilatini Thomasi Aquinas (St. Thoams Aquinas) aliwahi kueleza kuwa ana hofu kubwa juu ya mtu mwenye kitabu kimoja (a I fear the man of a single book) kwa tafasiri ya sisisi. Katika mazingira ya sasa, msemo huu haumaanishi kitabu kimoja kwa maana ya idadi au aina. Hapa tuuangalie msemo huu kama changamoto ya kuwa na kiongozi wa jamii ambaye anaamini ni yeye peke yake ndiye ana uelewa wa mambo kuliko wengine. Aina hii ya kiongozi ni ya kuogopwa maana hakuna asehemu ambayo ataifikisha jamii pana yenye watu wenye mahitaji tofauti. Tafasiri unavyoweza.

Ufahamu sahihi huja baada ya kuwa umetafuta maarifa na ukachanganya na zako, mawazo ya wanaokukosoa huwa si mabaya hata kidogo na ndiyo yamefanya jamii nyingi kuendelea na watu kufurahia kuwa sehemu ya jamii yenye tofauti. Kwa sasa aina ya viongozi na watawala tulionao inaundwa na watu wenye kitabu kimoja kichwani. Wanaamini na kujiaminisha kuwa wao wana mawazo sahihi kuliko wengine na pale wanapopingwa basi hoja ya nguvu hutangulizwa dhidi ya nguvu ya hoja.

Ni changamoto ya kawaieda tu ambayo naamini unaijua, mawazo mgando hayawezi kukusaidia katika chochote unachoamua kufanya, sikiliza wengine wanaamini nini na hapo kama kuna mazuri yachukue. Tafasiri unavyoweza
 
TUOMBE:Baba Asante kutuamsha salama tukiwa wazima leo Jumanne tarehe 7 Agosti 2018.Tunaomba Toba tusamehe..Tunajikabidhi mikononi mwako endelea kutupigania Mfalme wa Amani.Tuponye,Tubariki,Tuhuishe.
Tunajikabidhi sisi na kila tunalopitia Baba mikononi mwako..wafariji wafiwa wote wape mahitaji na tumaini wajane,wagane ,yatima watie nguvu waliipondeka mioyo.
Damu Takatifu ya Yesu Kristo inene mema makazini,safarini,katika masomo,kwa watoto na wahitaji wote wakutafute wewe .Hesabu hatua zetu Roho Mtakatifu kaa nasi.Ni katika jina la Yesu Kristo naomba na kuamini Amen

JUMANNE NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
Muziki: Siku Mpya Ya Zamani

Sitaandika mengi sana, ninakusalimia tu na kukuambia leo ni siku yangu ya kipekee ambayo kila nikikumbuka naona ninawiwa kukusalimia wewe Kapuku unayelifanya Jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Asante kwa kuweka tabasamu usoni kila mara ninapokuja hapa na hata usipokuwepo bado sichoki kupitia na kukumbuka mazuri unayochangia hapa, ya karaha na karaha yote yanafaa kuendana na HALI ya wakati nilionao.

Muziki, leo naweka muziki naoupenda mimi zaidi, ikitokea bahati mbaya ukaupenda basi nitaona nimeweka muziki mzuri

Tafasiri Unavyoweza: Waziri Na Mimba Ya Rushwa

...waziri wa mambo ya ndani kabeba mimba ya rushwa, na ni muda si mrefu mimba itazaa. Ndiyo, usijedhani naandika kumdhalilisha waziri wa mambo ya ndani, waziri ambaye badala ya kukaa chini na kuangalia namna nzuri ya kuboresha sera za usalama wa raia na mali zao amekuwa ni mtu wa kutangatanga, huku na kule, kama kala miguu ya kuku au miguu yake imelambwa na mbwa. Hatulii aseme ya msingi, hakai chini kusema ya kusaidia serikali inayojinasibisha kupambana na rushwa. Hajifungii ndani kuteta na wasaidizi wake namna ya kulifanya jeshi la polisi na idara zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa ufanisi, tija na weledi. Matamko ya kukatisha tamaa, matamko ya kutisha, matamko ya kuua na kutoa matumbo eti 'watapata tabu sana' ujinga na ulevi wa madaraka na mimba anayojitungia itahitaji mkunga wa tofauti, mkunga wa kuhakikisha mimba ya rushwa aliyoibeba haikui. tafasiri unavyoweza.

Angalia matamko anayoyatoa, mara kumuita Lugumi ofisini kwake, tangu lini serikali inajadiliana na wahujumu (kama kweli Lugumi and co) wamehujumu kiukweli? Tangu lini waziri anasimama kadinda kabisa, tumbo mbele kwamba hakuna kibali cha mtu kusafiri nje ya nchi kwenda kutafuta ajira halali! Waziri asiyejua tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wanaohangaika kila kukicha kutafuta kazi nje ndani, vijana waliosoma na kumaliza masomo yao ila waliofaulu ni watoto wa vigogo. Tafasiri unavyoweza.

Ninakuandikia wewe unayechekelea mimba ya waziri, wewe unayedhani uko salama kisa tumbo la waziri liko karibu na wewe linakupa kivuli, mkunga anakuja na sio wa kutumbua majibu bali kutumbua mimba za rushwa. tafasiri unavyoweza
 
TUOMBE:Baba Asante kutuamsha salama tukiwa wazima leo Jumanne tarehe 7 Agosti 2018.Tunaomba Toba tusamehe..Tunajikabidhi mikononi mwako endelea kutupigania Mfalme wa Amani.Tuponye,Tubariki,Tuhuishe.
Tunajikabidhi sisi na kila tunalopitia Baba mikononi mwako..wafariji wafiwa wote wape mahitaji na tumaini wajane,wagane ,yatima watie nguvu waliipondeka mioyo.
Damu Takatifu ya Yesu Kristo inene mema makazini,safarini,katika masomo,kwa watoto na wahitaji wote wakutafute wewe .Hesabu hatua zetu Roho Mtakatifu kaa nasi.Ni katika jina la Yesu Kristo naomba na kuamini Amen

JUMANNE NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
Amen
 
Tafasiri Unavyoweza: Waziri Na Mimba Ya Rushwa

...waziri wa mambo ya ndani kabeba mimba ya rushwa, na ni muda si mrefu mimba itazaa. Ndiyo, usijedhani naandika kumdhalilisha waziri wa mambo ya ndani, waziri ambaye badala ya kukaa chini na kuangalia namna nzuri ya kuboresha sera za usalama wa raia na mali zao amekuwa ni mtu wa kutangatanga, huku na kule, kama kala miguu ya kuku au miguu yake imelambwa na mbwa. Hatulii aseme ya msingi, hakai chini kusema ya kusaidia serikali inayojinasibisha kupambana na rushwa. Hajifungii ndani kuteta na wasaidizi wake namna ya kulifanya jeshi la polisi na idara zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa ufanisi, tija na weledi. Matamko ya kukatisha tamaa, matamko ya kutisha, matamko ya kuua na kutoa matumbo eti 'watapata tabu sana' ujinga na ulevi wa madaraka na mimba anayojitungia itahitaji mkunga wa tofauti, mkunga wa kuhakikisha mimba ya rushwa aliyoibeba haikui. tafasiri unavyoweza.

Angalia matamko anayoyatoa, mara kumuita Lugumi ofisini kwake, tangu lini serikali inajadiliana na wahujumu (kama kweli Lugumi and co) wamehujumu kiukweli? Tangu lini waziri anasimama kadinda kabisa, tumbo mbele kwamba hakuna kibali cha mtu kusafiri nje ya nchi kwenda kutafuta ajira halali! Waziri asiyejua tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wanaohangaika kila kukicha kutafuta kazi nje ndani, vijana waliosoma na kumaliza masomo yao ila waliofaulu ni watoto wa vigogo. Tafasiri unavyoweza.

Ninakuandikia wewe unayechekelea mimba ya waziri, wewe unayedhani uko salama kisa tumbo la waziri liko karibu na wewe linakupa kivuli, mkunga anakuja na sio wa kutumbua majibu bali kutumbua mimba za rushwa. tafasiri unavyoweza

IMG-20180807-WA0020.jpg
IMG-20180807-WA0016.jpg
 
SHIMBA YA BUYENZE asante kwa hiyo doc, ina maana waziri hakuwa analijua hili kabla ya kuanza kusema! na ujue baadhi ya watendaji wa uhamiaji wanaofuata maneno ya waziri watayatumia kujipatia rushwa na kusumbua raia wenye sifa halali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom