Muziki: Wiki Njema
Nikutakie wiki njema mdau wa Jukwaa hili zuri na nikusalimie kwa kujiaminisha kuwa ulikuwa na wikend nzuri. Binafsi nilikuwa na wakati mzuri na familia yangu yote. Ulikuwa ni wakati mzuri kutembelewa na ndugu mnaopendana. Ujue kwenye undugu kuna urafiki pia? Inawezekana usiwe wewe lakini mimi nina ndugu ambao sijawasiliana nano miaka kumi sasa, sijafanya juhudi kuwatafuta wao kwa bahati nzuri hawajajisumbua kunitafuta. Hii si sawa, najua unajua
Muziki sasa, tengeneza amani na walio ndani kabla hujapeleka maua kwa jirani