Ni kansa ndo ilimuondoa, hadi mauti yanamkumba mwaka 1981 mwezi Mei tarehe ya leo (Mei 11, 1981) alikuwa akivuta nusu kilo ya bangi kwa wiki. Alifariki akiwa kijana tu ana kwa kuwa aliacha vitu vingi vya kukumbukwa, hajawahi kufa mioyoni na masikioni mwa wote wanaopenda kusikia nyimbo zake.
Namuongelea mwanamuziki na miongoni mwa watu maarufu duniani Robert Nesta Marley, Bob Marley kwa umaarufu. Mzungumzaji wa taratibu aliyeamini katika imani ya kirastafari. Aliingia katika mgogoro na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Jamaica Michael Manley.
Akiwa nyumbani kwake mwezi December 1976 akijiandaa kutumbuiza tamasha la muziki alipigwa risasi, hazikumuua na watuhumiwa hawakupatikana. Bob Marley alimtuhumu waziri mkuu wa wakati huo kwa tukio hili.
Bob Marley, umeondoka lakini muziki wako unaishi na unabeba yote kila mmoja anayotaka kusikia leo na kesho.