Makapuku Forum

Makapuku Forum

Joshua 1:9
Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Mungu anataka mahali popote unapopitia uwe hodari hata kama mazingira magumu mtangulize yeye.

Tafuta sana kuwa hodari na moyo wa ushujaa kumtazama Mungu kwa kila jambo.

Mungu anataka akushindie katikati ya ushujaa uliouinua kwenye changamoto yako.

SHALOM FAMILY..GOD BLESS YOU.
 
Mhubiri maarufu kwenye luninga (Televangelist) Billy Graham amefariki dunia leo hii siku ya Jumatano 2/21/2018 akiwa na miaka 99.

29599.jpg

The Rev. Billy Graham, Who Reached Millions, Passes Away - Positive & Encouraging K-LOVE
 
Tafasiri Unavyoweza: Kosoa, Onyesha, Pongeza Tusonge

Hakuna ambaye kwa namna moja ama nyingine anaweza kusema amekamilika na yupo sahihi kwa kila kitu. Sisi ni watu/binaadamu na tuna mapungufu hata kama tutajiona tuna akili kushinda wengine, hata kama tutajiona tumefanikiwa kushinda wengine na au tutajiona tuna usalama kushinda wengine. Lazima ipo 'engo' ambayo itauanika udhaifu wako tu kwa wengine. Tafasiri unavyoweza.

Ukosoaji ni namna nzuri ya kufanya kitu kikubalike na wengi na ukae ukijua kabisa ukiwa na ndoto, hiyo ni yako usilazimishe wote wawe naye na hata ukifanya wengine waijue ndoto yako basi usidhani nao hawalali, hawaoti na kuwa hawana ndoto zao, wanazo. Tena wanaweza kuwa nazo bora zaidi zinazowaangazia wengi si kama yako na mto wako kitandani.

Ukosoaji hauji tu kwa minajili ya kukosoa, anayekosoa anajua, amefanya rejea na ndiyo maana anakosoa onaonesha mapungufu yako wapi na nini urekebishe ili mwende sawa. Hivi ndivyo tunavyofanya kwa watoto darasani, tunatakiwa kufanya kwa viongozi madarakani, tunatakiwa kufanya kwa wenza sebuleni na chumbani, tunatakiwa kufanya kwa wageni ugenini na tusisahau kukosoa kwa wenyeji nyumbani.

Tafasiri unavyoweza, kukosolewa isiwe sababu ya kukufanya ujihami, mpe nafasi anayekukosoa ili uweze kusikia mawazo yake na unaweza kupata kitu kizuri cha kuboresha katika kile anachokosoa. tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Salamu

Ninakusalimia Kapuku mheshimika, na ujue tu leo ndo wiki imekatwa katikati na wewe endelea tu kukatika mikatiko ya kukufanya uifikie siku ya kesho ukiwa na tabasamu usoni. Nilikuwa na wakati mzuri mchana wa leo na niseme tu ukweli, kuja kwangu hapa jukwaani ni kwa sababu wewe upo.

Sichoki kuandika japo aya mbili tatu kila siku mahali hapa maana najua kadri ninavyopenda kusoma na kuandika basi nawe unapenda kusoma na kuandika na muziki unatukutanisha na kutufanya tuwe pamoja mmojammoja.

Muziki sasa, mjomba wangu kafanya jambo zuri sana kwa jamii na ukoo wetu, baada ya kuamua kusilimu kwa muda Lyon Lee kaamua kutimiza ahadi yake kwa chama kaongeza mke wa tatu japo huyu hajalipa mahari

Binamu shukranii kwa taarifa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom