Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Kundi Letu, Maoni Yetu

Maoni ya kundi yana nguvu, huwa hayaji hivi hivi tu au kwa bahati mbaya. Huja baada ya mazungumzo na mijadala mipana ambayo wakati mwingine kabla hujasikia hitimisho unaweza kudhani kundi husika hataelewana. Kwa taarifa yako tu ni kuwa, kundi ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye malengo waliyokubaliana. Bila malengo basi kundi linabaki kuwa mkusanyiko wa watu.

Kwanini ninaandika haya ili wewe utafasiri unavyoweza, kumekuwa na dhana tofauti kuhusu Makapuku Forum, kundi hili limekuwa, bora sasa, likishambuliwa bila ya washambulizi kuchukua japo nafasi kidogo ya kulifahamu. Kiuhalisia kulianzishwa hadi nyuzi kadhaa kuwa kundi hili uzi wake ufutwe na wengine walipoona umoja unaooneshwa na Makapuku waliamini Makapuku inapaswa kuwa Jukwaa linalojitegemea. Tafasiri Unavyoweza.

Siku zote, kama unataka kujua maana ya kitu basi jipe nfasi ya kutokuwa na upande, itakusaidia kujua zaidi na hapo ndipo utaweza kuwa na nafasi ya kuchagua upande. Ukiwa na maoni yako tayari, kutafuta maoni ya mwingine ni kupoteza muda. Humu ndani tumo watu wa kila namna, kada, na jinsi. Tunatofautiana kwa mwengi sana na tunajijua kuwa tunatofautiana lakini siku zote tofauti zetu ndiyo umoja wetu.

Mijadala ya makapuku kama kikundi huwa haiwi rahisi, hujadiliwa na majadiliano aidha ya siasa, uchumi, falsafa, muziki, utamaduni au maisha ya kila siku huwa sio rahisi. Na kwa ugumu huo, majadiliano huzaa hitimisho na kuelewana au kukubaliana kutoelewana (our discussions as a group enhance majority opinion). Watu hujadiliana, hutofautiana na hukubaliana kutofautiana lakini mara nyingi Makapuku forum katika JF ni kama hadithi ndani ya hadithi. Tafasiri Unavyoweza
 
6027ee2385ae15b244854c041b3ab7d8.jpg
 
Asantee binamu ndio mana nakupenda mimi
 
Muziki: Sogo Sogozo

...kama hujaelewa maana ya sogo sogozo basi sio jukumu langu mimi kukueleza maana, hii inaweza kuwa ni sawa na jukumu lako kumtafuta mwalimu Gugo au mwalimu mkuu maktaba na ukatafute maana yake. ni vizuri kila siku kuongeza neno moja au zaidi. Ninakusalimia Kapuku mheshimika usiku huu nikiamini kabisa ulikuwa na wakati mzuri siku ya leo na sasa unaitafakari siku ya kesho.

Nikushukuru sana Nyagei mtaasisi kwa kutuonjesha kidogo ladha ya soka ambayo tuliikosa kwa muda tangu mwaka huu umeanza. Asanteni sana Transcend , Shunie , Sakayo kwa sogozi ambayo imevutia kuifuatilia. BlessedHope asante kwa asubuhi ya neno na sala, ni namna gani nzuri ya kuianza siku kwa sala na salamu za heri.

Muziki sasa, mjomba wangu Lyon Lee hajambo sana, Valentine na Valentina wa kilombero ilimuachia michubuko kutwa nzima anavaa kanzu. Ndo mjomba wangu huyu, akirudi atakuja kukana haya na mimi akiuliza kama mimi ndo nimesema nitakana, mambo ya ukoo haya

Similar Discussions

Back
Top Bottom