Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Pole Akwilina

Sitaandika mengi leo, nitaandika machache tu na kukuachia wewe nafasi ya kutafasiri Unavyoweza. Kila uhai wa raia wa nchi hii unathamini ya kulindwa kwa kila hali. Ndiyo maana ya kuwa mwananchi, utalindwa na jeshi, polisi , family, jamii na utalindwa na Mimi na wewe.

Wapo madhamana tuliowapa jukumu la ulinzi wa raia na mali zao, hawa tunawaita kwa jina zuri, jina lenye kukuhakikishia usalama likitamkwa. Lakini imekuwa sivyo, matukio mengi kadhaa ya kiuhalifu wa damu za raia yana mkono wa polisi. Tuna polisi wanaofurahia kufyatua risasi kwa watu wasio tishio kwao. Maandamano yaliyosababisha kifo cha mtanzania Akwilina ni moja ya maandamano ambayo hayakuwa na madhara si tu kwa raia na mali za serikali bali kwa polisi pia.

Tunaweza kuwalaumu watu kadhaa, blame game, lakini haitakuwa na suluhu kama tutaendelea kuruhusu Uhuru wa maoni , taarifa, maandamano ushikiriwe na watu wachache. Kukaa mbali na kujitenga hakukuweki salama hata siku moja. Akwilina ameenda, kapigwa risasi akiwa ndani ya daladala, hakukuwa na maandamano ya daladala kiasi kwamba risasi kulenga kuua irushwe.

Usidhani uko salama kwa polisi wa aina hii wanaoongozwa na kamanda Mambosasa ambaye tafasiri yangu kwake ni kiongozi mbovu asiyejua anafanya nini ofisini. Lakini hebu jiulize, kanzu ikichafuka baraghashia itakuwa safi kweli!? Pole Akwilina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom