Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Pumzika Salama

Ninakuandikia Jumatatu ya leo, ndiyo, siku inaishiria na siwezi kuizuia kuisha maana ikiisha leo ndo mwanzo wa siku nyingine kuchipua. Ninakuandikia pia Kapuku wewe nikiwa na imani kubwa kabisa ulikuwa na wikend njema sana japokuwa haimaanishi kwamba wikend yote ilikuwa msalazo.

Wengine mapumziko ya juzi tumeyatumia kufariji ndugu na jamaa zetu waliofiwa, wanaouguza na tumewatembelea na kutoa msaada kwa wahitaji. Hili ni jambo jema sana kufanya kipindi hiki na kipindi chote na kama Transcend anavyosema maisha ni mafupi bora kukulana, hongera sana tuliokulana na kusaza tukijua kabisa kuna viporo havichachi na harua haina makombo. Hii ndo misemo inayompa kichwa anko wangu Lyon Lee yeye kwake shombo la samaki ndo ulevi wake. Sasa kakutana na aunt yangu maji ya shombo hajui kuyaandaa imebidi aende kwa ABJ Ashura Bint Jumong

Muziki sasa, oh, ujue kichwa cha habari leo kinahusu kupumzika salama lakini ndo hivyo nimekumbushwa maneno ya kina Shunie yamenitoa mstarini. Pumzika salama Akwilina na wengine wote mliotangulia na kutangulizwa mbele ya haki. Pole kwetu sote.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom