Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,282
- 35,645
Tafasiri Unavyoweza: Kutembea, Fungua Macho na Masikio
Leo nitaweka ufafanuzi wa kauli yangu kuhusu kutembea namaanisha nini, maana usijedhani ninaongelea utembezi unaohusisha kusogeza mguu, la, nina maana zaidi ya hapo. Wengi tunapenda kutembea na kufika sehemu tofauti tofauti na wengine kama khali ingekuwa inaruhusu basi tungedandia midege mikubwa na kuzuru maeneo mengi duniani kama siyo yote ulimwenguni.
Kutembea kuna faida, ndiyo na hasara zipo lakini faida ikiwa kubwa zaidi ya hasara kama ni biashara basi unafanya bila kuangalia hasara. Tafasiri unavyoweza. Mark Twain, mwandishi nguli ananukuriwa akisema Travel is fatal to prejudice, bigotry, and narrow-mindedness (tafasiri isiyo sahihi, ni kuwa kutembea huongeza ufahamu, huleta kuvumilia wengine). Maarifa hayaongezeki kwa kukaa eneo moja tu, tembea na ukitembea fungua macho na masikio ili ukirudi nyumbani ukakutana na sisi tumerudi toka matembezini basi tusimuliane nini tunafanya kujenga jamii yetu.
Tafasiri unavyoweza, kutembea huku, nasisitiza tena, namaanisha zaidi ya kunyanyua miguu, pata maarifa kupitia vitabu. wengi tunajijua hatupendi kusoma vitabu, hii ni mbaya sana na hasa pia ukiwa huna uwezo wa kutembelea sehemu nyingine. Shika kitabu, ongeza maarifa, kitabu kitakutembeza sehmu nyingi tofauti na utajiona mwenyeji wa maeneo hayo. Ndo uzuri wa kitabu, kinakuongezea ufahamu, kinakufanya ufikiri na zaidi kinakutofautisha na wanyama wengine wanaoweza kuongea, kutembea ila hawawezi kusoma.
Wikend Njema