Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Gitaa La 2018

....nikusalimie kwa mara ya kwanza kabisa katika mwaka huu 2018, ni mwaka mpya, hili halina ubishi. Tumesheherekea na kwa wewe kuwa hapa na kuweza kusoma hiki ninachoandika ninaweza kujisemea kwa kujiamini kabisa kuwa umeupita na kuuanza mwaka vizuri.
Wakati naanza kuandika kipengele hiki mwaka jana, nilijikita kwenye utamu wa gitaa, maana ndicho kifaa muhimu kwenye muziki. Mara nyingi nilichagua nyimbo mwenyewe na baadaye wadau na hasa wewe ukaanza kuchagua muziki na nikawa naucheza. Chaguo lako bila kumung'unya maneno lilinifanya nijisikie kuthaminiwa sana. Kwangu, heshima ni njia mbili, kwangu kwako na sio vinginevyo.

Kwa mwaka huu 2018 kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo lakini kaa ukijua kabisa hiki kipengele kwa huu mwaka mpya sitakimiliki mimi, kitakuwa ni chako pia kwa maana ya kwamba utakuwa na nafasi kubwa ya kuleta muziki na kuucheza. Tutakuwa tunacheza muziki wa aina tofauti, tutatambaa mabara karibu yote inapowezekana na Furahiday nitajitahidi kucheza bakulutu zaidi.

Muziki sasa, nikutakie mwaka 2018 wenye mafanikio, ni namba tu zimebadilika lakini wewe na mimi tunabaki kuwa wale wale na kama hujakumbwa na bomoa bomoa na vyuma kukaza basi bado una nafasi ya kupiga hatua kwenda mbele na inapotokea unapiga hatua kurudi nyuma basi iwe ni kwa ajili ya kufanya masahihisho kwa yale tuliyoshindwa kutatua mwaka ukiopita. Ninaandika sana eeeeh! Basi ninkuache na gwiji wa muziki na mpiga ala maarufu Tanzania Mzee Kitime akicharaza gitaa lake. Huyu mkongwe analijua gitaa na ukimjumlisha na komandoo Kalala bila kumsahau Dekula Vumbi basi utaupenda muziki.

 
Ayoo ndo manenoo na mm sitafutii tena mchepukoo

....anko tunajuana bhana, wewe kama Mmasai tu, kukuwekea dhamani ni kutafuta kukonda tu.

Anko wangu baada ya kumaliza tofauti zake na ABJ

giphy.gif
 
....anko tunajuana bhana, wewe kama Mmasai tu, kukuwekea dhamani ni kutafuta kukonda tu.

Anko wangu baada ya kumaliza tofauti zake na ABJ

giphy.gif
Anko so sorry kitumbua sio andazii najua nimekumoseaa sana ila naamini mambo yakooo supaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom