Makapuku Forum

Makapuku Forum

MITHALI 3

24. Ulalapo hutaona hofu;Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.

25.Usiogope hofu ya ghafula,Wala uharibifu wa waovu utakapofika.

26.Maana Mwenyezi -Mungu ndiye atakayekutegemeza;atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.

USIKU MWEMA DAMU YA YESU ITUFUNIKE
 
TUOMBE:

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi Asante kwa wema na Upendo wako kwetu kwa kutupa neema hii yakuiona siku ya leo JUMATANO 3 JANUARI 2018

Asante Baba unastahili kuabudiwa Mfalme wa Amani

Wapo wengi walitamani kuiona siku ya leo hawakuweza Baba kuamka kama tulivyo sisi leo .

Baba tunakuja mbele zako leo tukiomba toba Baba Utusamehe makosa yetu tuliyotenda kwa mawazo kwa maneno kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu wetu kwa nafasi zetu zote tulizonazo kwa kujua au kutojua
Tunaomba pia kuwasamehe wote waliotukosea walioomba msamaha hata wasioomba msamaha

Tunakuja mbele zako tukiomba Utulinde Utuokoe katika ajali mbalimbali za kimwili na kiroho Uwalinde watu wote wa familia zetu wasaidizi majumbani wake Waume Wanandoa Wachumba watoto Ndugu Jamaa na marafiki

Baba tunaomba Roho Mtakatifu akae nasi atufundishe kukujua kukupenda kukuheshimu na kukutii wewe tu

Baba Waponye wagonjwa majumbani na mahospitali
Baba wewe ndie mponyaji wa kweli waponye wagonjwa wote watie nguvu ndugu wazazi na walezi onekana kwao waamini Uponyaji toka kwako

Baba tunaomba ponya dawa wanazotumia wagonjwa wote wabariki madaktari na manesi watie nguvu wanaoguza wasipungukiwe

Wafariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wapweke Walea pekee wenye mahitaji mbalimbali

Wape utulivu na majibu Baba wanaotafuta watoto ,wenye madeni wanaotafuta kazi, wanaotafuta Ada , wanaotafuta kodi za nyumba wenye mitihani na wote wenye uchungu na kukata tamaa Waliokataliwa Wafungwa waoneshe ukuu wako Baba kuwa unawapenda siku zote za maisha yao wawe na amani wakupende na wakuone wewe katika kila pito.

Tunaomba kila tunapotoka na tunapoenda Uwe dereva na kiongozi wetu tulinde Nchi kavu Majini na Angani Damu ya Yesu itufunike tuangalie kwa wema tufike salama katika safari zote siku ya leo Mfalme wa Amani

Tunaomba uwabariki Viongozi wote wa Dini waweze kutuongoza vema kiroho na tuwe na hofu ya Mungu,epusha migogoro yote amani itawale.

Walinde viongozi wa serikali na wenye mamlaka waweze kuongoza vema na kuwa na mwenendo bora,wawe na hofu yako Mfalme wa Amani Nchi iwe na Amani na Utulivu.

Ponya kazi za mikono yetu Biashara Ajira Ujasiriamali uonekane Mfalme wa Amani tupate riziki kihalali

Baba tunayo mengi unayajua tunaomba uyapokee na utupatie sawasawa na mapenzi yako utupe kuvumilia katika Mapito mbalimbali kwani kwako yapo majibu huchelewi wala huwahi .

Asante Baba kwa kuwa unatupenda na hujawahi kutuacha kila tukuombapo unatujibu

Tunaomba Tunashukuru na kuamini katika jina la Yesu Amen.

DAMU YA YESU ITUFUNIKE,SIKU NJEMA
 
ZEKARIA 2

5.Mwenyezi Mungu asema kuwa yeye mwenyewe atakuwa ukuta wa moto kuulinda mji huo pande zote,naye atakaa humo kwa utukufu wake.

Asante Mungu kwa usiku huu umetulinda mchana kutwa tunakushukuru,
sasa ni usiku tunalala..tunajua ahadi yako itatimia utakuwa ukuta wa moto katika mji huu pande zote na utakaa humu kwa utukufu wako..angalia familia zetu,watoto wetu,majirani zetu,marafiki zetu uwazingire kwa ukuta huu adui asipate nafasi asante maana tutakuwa salama usiku kucha..katika jina la Yesu tunashukuru na kuamini Amen
 
IMG-20180104-WA0013.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom