Muziki: Heri ya Mwisho wa Mwaka 2017
..nilisema juzi na nitasema tena leo. Sitaacha kusema hata kama inabore kurudia kile kile kila wakati, na uzuri ni mmoja tu, ninachopenda mimi sio lazima uwe unakipenda (relativity). Lakini angalau wengi wetu tunakubaliana kuwa uwepo wako hapa, mimi na wewe pamoja na yule unalifanya Jukwaa hili kuwa sehemu bora kabisa ya kuwepo. Ninakushukuru sana kapuku wewe kwa namna ambavyo umekuwa ni wa kipekee hapa jukwaani.
Leo ni jumapili ya mwisho kwa 2017 na nikitazama tangu mwaka ulipoanza hadi leo, kuna mengi nimejifunza. Mengi nimefanya ya kufurahisha, kuelemisha, kukarahisha. Nimejifunza mengi, nimepata mengi ya maana toka kwako, mazuri mengi na mabaya machache ya kuhesabu nikashindwa kumaliza. Sitachoka kusema asante kwako.
Kwako
shululu na
Tumosa ninyi ni watu wema sana mwaka 2017 kwangu ulikuwa poa kwa sababu mlikuwepo humu. Anko wangu
Lyon Lee na
Shunie niseme nini kwenu, mnajijua ninavyowapenda na mlinifanya niwe na tabasamu kwa zawadi bila kujali karaha zangu ambazo siwezi kusema kama zitaisha maana mkigombana mkapatana nakasirika ila sina jinsi inabidi niwafurahie. Kwako
husna muba mpenzi wangu mwenyewe na sina mwingine zaidi yako wewe, asante kwa kuwa na mimi bila kunihakikishia kama utanivumilia mwaka mwingine.
BlessedHope , sijui niandike nini juu yako, ningependa niwe juu yako lakini style ziko nyingi sana, utabaki unashangaa nikisema asante mno kwa wewe kuwepo hapa. Namna ulivyolipendezesha Jukwaa sina la kusema zaidi ya kukuombea mazuri mengi wakati wote. Halafu ujue nini, siri yako lakini,
nakupenda mno najua unajua. Vimaandishi vidogo ni vyako peke yako.
Hakuna wadau wa muhimu mliolinogesha jukwaa kwa nondo za ukweli, falsafa, elimu na maujuzi yasiyo ya juzi kama wewe
SHIMBA YA BUYENZE ,
makaveli10 ,
Mndali ndanyelakakomu ,
Sakayo ,
Transcend , Gentries (wewe nawe punguza kubadili majina, unayo mengi sana kama mwanafunzi mtoro).
Antonio Conte ,
Jimena ,
Bitoz ,
Bailly5 ,
Werrason ,
Madame S ,
demi ,
ABJ ,
mzeewakungoa ,
dumejeuri ,
Mkushi wa kusi ,
Nyagei ,
EMMYGUY ,
eden kimario ,
Niliowataja hapa na wewe ambaye nimesahau kukutaja ila uko hapa, tambua kitu kimoja. Mwaka 2017 tunaoufunga leo, ulikuwa mzuri sana kwangu kwa sababu uliufanya uwe mzuri, well, kuna mahali tulikwazana. Binadamu kukwaza, kukwazana si jambo baya, maisha ndo yako namna hiyo. Pamoja na kutofautiana kwetu bado tulisimama na kuendelea kuwa hapa kwa raha na karaha zinazounganisha tofauti zatu. Asante
Muziki sasa, tunachonuia leo kwa ajili ya kesho basi kiwe ni kwa ajili ya kujenga daraja na si kulibomoa. Na unalijua daraja letu ni hili, Makapuku Forum