Makapuku Forum

Makapuku Forum

Naomba nyimbo mie niliyochagua
tenor.gif
 
Muziki: Wikend ya Sikukuu

...habari za Ijumaa Makapuku wenzangu, sijambo na kadri mwaka unavyoelekea kuisha ndo najiona hikma (wisdom) nazo zinazidi kuongezeka kwa hiyo kwa wote wenye kutaka ushauri nasaha basi ninawakaribisha kwa a very reasonable fee, yeah, utalipia hekima utakazokutana nazo kwenye ushauri wangu. Hakuna cha bure, kama vyuma vimekaza tafuta plastic yenyewe inafuata unavyoielekeza.
TGIF na kama unavyojua huwa ni wakati wa kujirusha bakulutu kidogo, kusikiza story za wadau na zaidi kulichangia kodi taifa letu kwa kunywa na kula. Sio unakula nyumbani Monday to Sunday, siku nyingine unavamia kwa friends mida ya msosi na unawaharibia ratiba zao. Ndo utamaduni huo. Na Ijumaa unakaa sehemu na friends unaangusha moja moja pamoja mmojammoja. Kama una mpango wa kutegemea mfuko wa mwenzako basi mjulishe mapema usijekutana na wasio na haya kama anko wangu ambaye yeye anaweza kuagiza bia mbili kwa mkupuo na akazinywa huku anakuangalia kwa tabasamu ambalo ni kama linasema 'mhudumu huyu hapo, muite uagize mbili kwa hela yako'.

Muziki sasa, ninakukumbuka wakati wote kapuku mheshimika na sitochoka kukwambia kuwa bila wewe jukwaa hili linabaki kuwa debe tupu, lakini kwa uwepo wako hapa, tumekuwa sio mfano tena bali original. It's furahiday and wishing you a happy almost Christmas with love

 
Muziki: Mdhamini Anamsubiri Fundi Nguo

...kama kuna watu watata basi kofia nawavulia mafundi nguo, sio wote ila wengi wao ni vimeo mbaya yaani wanaweza kukupa ahadi huku wanatabasamu kabisa kuwa ' bhanaweee njoo uchukue nguo yako jioni nitakuwa nimeimaliza' sasa fika jioni, unakuta anakukaribisha na uso wa kilio huku anakata nguo nyingine kabisa. Kitakachoendelea ndo utamalizia maana Shunie ndo kanikumbusha kuhusu sikukuu na nguo mpya

Furahia chaguo la mdhamini wetu ambaye kwa bahati nzuri katokea kuwa ni mke wa anko wangu mdogo wa Lyon Lee

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom